WAWINDAO ROHO ZA WATU

 
Na:  STEVEN NAMPUNJU (AP), Ufufuo na uzima , Morogoro.
Utangulizi: Wapo  watu  wanaowinda maisha ya watu wengine katika hii dunia tunayoishi. Ukienda nyikani utawaona wanyama walio  hodari wakiwinda wale walio  dhaifu. Na kwa wanadamu ndivyo ilivyo. Mwindaji ni mtu au mnyama anayetaka kunasa maisha ya mwenzake kwa kutumia nyenzo zinazosaidia uwindaji wake.
Imeandikwa  katika YEREMIA 5:26…[Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.]… Utaona leo wanadamu wa nchi mbali mbali wakitengeneza silaha mbalimbali,  siyo kwa ajili ya kuwindia wanyama wa porini, bali kwa ajili ya kuwindia wanadamu wenzake. Mwindaji hutengeneza tukio kwenye  hayo mawindo yake ili iwe rahisi kwake kutega mtego wake. Shida ya mtu hufanyika  kuwa mtego wa kukunasa na adui zako. Pengine hauna kazi, na shida ya aina hii yaweza kukupelekea kunaswa na mtego wa  boss ambaye atakuahidi kukupatia kazi lakini  kwa sharti  la kufanya naye mapenzi!!! 

Imeandikwa katika EZEKLIEL 13:18…..[useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?  19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.]….. Hirizi ndizo silaha wanazotumia kuwindia vipawa vya mtuili  wavikamate. Mungu hakumuumba mwanadamu akawe mtawaliwa,  bali mtawala. Shetani anapofusha macho ya wengi ili wasifanikiwe  kama alivyopanga Mungu. Hata shetani, katika kuutega mtego wake,  alimfuata mwanamke kule bustanini na alipomkuta yu peke yake paophapo akafanikisha kumtegea mtego naye akanaswa!!!
Mara zote anayewinda huvaa mavazi au umbile lisilo la asili yake, na kujificha ili usimgundue. Wanyama porini hubadilisha hata miondoko yao, na kujifanya hajui wakijifanya hawajui kukimmbia. Hata hivyo, anapofanikiwa hudhihirisha umbile lake la asili.
Kwa  wanadamu vivyo hivyo,wapo wanaotembea na mitego yao hadi makanisani ili kunasa wengine. Pengine huko mtaani ameshakuona, lakini  ikawa ngumu kukupata.  Njia rahisi atakayotumia ni kuja kanisani,  na baadae atatumia silaha ya kuokoka. Mwishowe, akeshampata wa kumuoa, biashara ya wokovu inaishia hapo hapo.

Upo wakati wa kuwinda. Katika kuutega,  mwindaji hutengeneza namna za kupata mawindo yake. WAGALATIA 4:4…[Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,]… Kumbe hata Mungu alipokuwa akiandaa wokovu wetu, ulikuwepo wakati wa kusubiria ili ufike. Kwenye mawindo,utulivu hutawala.  Mwindaji hutulia sana akiwa anawinda. Mathalani, endapo ni mnyama wa porini, hata kupumua kwake hupungua.
UKIRI
Leo nauondoa utulivu wowote wa kishetani, uliowekwa ili mimi ninaswe, Leo nauondoa kwa Jina la Yesu. Ninakataa leo, utulivu wowote aliouweka adui yangu ili anase maisha yangu, niachie leo kwa Jina laYesu. Amen.

KWA NINI WANAWINDA?
Lengo kubwa la mwindaji  kuwinda na kuweka mitego  yake ni KUHAMISHA mtu au kitu kutoka sehemu moja hadi nyingine. Anayewinda, anataka akutoe kwenye ndoa/hatima/kazi/ biashara ili akupeleke sehemu nyingine. Mathalani yupo atakayekushauri usiolewe na mtu fulani wakati yeye binafsi hajaolewa. Yupo anayewinda maisha yako,  siyo akakutunze, bali akakuchinje na kukumaliza siku hiyo hiyo.
Mungu alivyowatoa wana wa Israeli kuiendea nchi ya maziwa na asali, wale  watu hawakujiuliza maswali, je hao ng’ombe wa kutoa hayo  maziwa wapo wapi au wanafugwa  na nani?! Na hata walipoikaribia Bahari ya Shamu, Mungu alimwamuru  Musa aigawanyishe Bahari kwa kuitumia fimbo yake mkononi mwake
Mwindaji hulenga piakuchukua vitu kwa nguvu. Imeadikwa katika EZEKIEL 22:23-25 [Neno la Bwana likanijia, kusema, 24 Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyosafika, wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu. 25 Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza hesabu ya wajane wake ndani yake.]….Biblia pia inasema mtu mwenye  nguvu alindapo  vitu  vyake vinakuwa salama,lakini endapo atatokea  mwingine mwenye nguvu  zaidi hutumia nguvu  na kuviteka.
ISAYA 42:22…[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]…. Mungu anawaona watu walioibiwa na kutekwa. Ni watu ambao walipaswa wakae mahali fulani waitumikie serikali,  lakini kwa sasa wapo sehemu  tofauti. 
UKIRI
Nakataa kwa Jina la Yesu, ewe shimo uliyeandaliwa ili  kuyakamata masiha yangu,  ninakataa kwa Jina la Yesu. Kila gereza lililoandaliwa ili kushika uzao wangu leo nakuagiza unikatae kunishikilia,  na uniachie kwa JIna la Yesu. Amen
Ipo taarifa mbaya kwa kila aliyetega mtego kwa maisha yako. Leo hii kila aliyeandaa mauti juu yako, tunawataarifu kuwa, kila aliyetega mtego mtego utamnsas kwa Jina la Yesu. Mungu ndiye shujaa wa kuokoa.Mwanadamu hawezi kukuokoa.
UKIRI
Kuanzia leo, nakuanzia sasa, enyi watu waovu mliojipanga kuotea maisha yangu, leo ninawapiga  kwa Damu ya Yesu. Mahali popote ambapo iblisi ametegea mitego  ili kuyanasa maisha yangu, nakataa kwa Jina la Yesu. Amen.

Mwindaji mmoja,  Mfalme wa Misri asiyemjua Yusufu alipogundua kuwa wana wa Israeli wanaongezeka kwa kasi, alibuni mpango mkakati wa kuwapunguza idadi yao kwa kuwaendea wazalishaji  ili kwamba watakapokuwa wakiwazalisha wanawake wa Kiebrania, basi "wawatendee kwa akili" – kwamba wawaue watoto wa kiume tu, lakini wale wa kike waachwe waishi.  Kwa nini wawaue wa kiume tu? Ni  kwa sababu wanaume baadae ndiyo washika silaha na wapiganaji. Kwa hiyo wangeongezeka zaidi wangeungana na maadui  wa Misri katika kufanya vita.
Imeandikwa katika YEREMIA 5:26-29…[Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. 27 Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. 28 Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. 29 Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?]… Kutokana na andiko hili, tunafika mahali pa kujiuliza maswali:
 
KWA NINI WAWINDE ROHO TU?
Ahadi yoyote ambayo Mungu aliwahi kumuahidi  mwanadamu, ipo  katika roho. Mungu anaposema, “Ujapopita katika  maji mengi hayatakugharakisha”,  siyo kwa ajili ya mwili wako bali roho yako. Wawindaji nao  wanafahamu haya. Kwamba hawawindi mwili, bali huwinda roho.  Hata silaha zeetu hazipo  katika mwili,  bali katika roho zetu.  Mwindaji anafahamu kuwa akikamata roho,  ameukamata na mwili pia. Ukiiteka roho umeuteka na mwili  pia. Silaha za Mungu wetu hazipo mwilini, bali  katika roho. Imeandikwa “Roho ndiyo itiaayo uzima, mwili  haufai kitu”. Roho  ikiondoka mtu anakufa, roho ikirudi mtu anafufuka na ndicho tunachokisoma katika (1WAFALME 17:17) na kuendelea kuhusiana na ufufuo wa yule kijana.
Kimsingi roho ndiyo imebeba mafanikio ya mwili. Imeandikwa katika 3 YOHANA 1:2… [Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.]… Yohana anamuombea Gayo afanikkiwe mwilini, kama ambavyo  roho yake Gayo ilivyokwisha kufanikiwa. Wawindaji ndiyo maana huwinda roho. Wanafahamu kuwa mafanikio ya mtu yanaanzia katika roho yake. Ndiyo maana Mungu alimpa sharti shetani,  kwamba “vyote vipo mikononi mwako,  ila roho yake Ayubu usiiguse”. Unafahamu kwa nini Mungu alimzuia shetani kutoigusa roho ya Ayubu? Ni kwa sababu hatima ya Ayubu ilikuwa katika roho yake, na siyo  mwili wake.

Roho inaweza ikasafiri na kwenda mahali ilikumfungua mtu. Wakati Petro alikuwa maefungwa gerezani, penye ulinzi mkali sana, Petro mwenyewe alijikatia tamaa. Hata hivyo kanisa lilipokuwa likiomba, wale waombaji hawakuamini kuwa ingewezekana Petro kuwekwa huru.  1PETRO 3:18…[Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 22 Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.]. Maandiko haya yanatuambia kuwa, Baada ya Yesu kufa msalabani, roho ya Yesu  ilisafiri hadi kuzimu  kufanya kazi. Yesu aliwaendea waliokufa zamani zile za enzi ya safina ya Nuhu akawahamisha baada ya kuwahubiria. Kumbe roho  ina uwezo wa kuhubiri. Kama roho  inaweza  kusafiri na kumtoa mtu kwenye gereza/ au shida, vivyo hivyo roho za waovu zinaweza kusafiri na kuleta shida na matatizo kwa watu wengine
Hivi unafahamu kuwa Goliath ndiye aliyempa ufalme Daudi? Bila Goliath, hakuna ufalme kwa Daudi. Shida au taabu iliyopo maishani mwako ndiyo itakayokupa ufalme kwa Jina la Yesu. Daudi hakuwahi  kupata mafunzo ya kijeshi. Daudi aliuliza swali, akitaka kujua kwamba ni kitu gani ambacho mtu  atapewa baada ya kumshinda Goliath? Baadae, Daudi alilazimika kujitambulisha mbele ya Goliath kuwa “mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana”.  Ukilibeba Jina la Bwana wa Majeshi, utapata ushindi wako  dhidi ya adui zako wanaokuwinda.
Ili uupate  muujiza wako lazima uwe na kitu. Yule mama mjane vivyo hivyo, alipoulizwa na Elisha ana nini nyumbani  mwake alisema ana mafuta kidogo sana yamebakia nyumbani  mwake. Hicho kidogo ulicho nacho kitumie,  na ukeshafanya hivyo utapokea muujiaza wako kwa Jina la Yesu. Zipo roho zinazotokea mahali fulani, labda ni shimoni au baharini ili kuikamata roho yako.  Silaha  kubwa ya iblisi ni kukupiga akitokea ndani. Pengine mtu alikuwa muombaji mzuri, lakini  leo hii haombi tena, ni  kwa sababu shetani ameingia ndani ya huyo mtu!!
UKIRI
Kwa Damu yaYesu, kuanzia leo, na kuanzia sasa, yeyote anayewinda roho yangu aniachie, kila roho iliyo ndani yangu au nje yangu leo niachie kwa Jina la Yesu. Ewe mwindaji unayewinda roho yangu, leo niachie kwa Damu ya Yesu. Ninaikata kila kamba ya mtego iliyonifunga, Uliyetumwa ukae ndani yangu ili uniwinde, leo kwa Jina la Yesu achia, kwa Jina la Yesu.  Amen

Wapo waoteaji, wanatazama na kusema huyu mtu hana wa kumsaidia. Ni heri leo ukamuamini Yesu, atakuwekea alama ya Damu yake na kukusajili kuwa mmoja wa watu wake.

Comments