ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA!. Sehemu ya ishirini na nne!.

Na Mwl Nickson Mabena.

Bwana Yesu asifiwe, namshukuru Mungu wa Mbinguni kunipa nafasi tena ya kuandika ujumbe wa Neno la Mungu kupitia somo hili!.
Tunaelekea Mwishoni mwa somo hili, maana tupo kipengele cha mwisho, ambacho tunakaribia kukimalizia!!.
8.JINSI YA KUNGIA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO, KUPAMBANA NA UFALME WA GIZA NA KUUSHINDA!.
Nilikupa jambo la kwanza na la Msingi kwa mtu unayetaka kupambana na Ufalme wa Giza, nilikuambia huwezi kupambana na Ufalme wa Giza ukiwa ndani ya Ufalme wa giza alafu ukaushinda ufalme wa Giza!.
Nilikwambja ni lazima UOKOKE, yaani Uhamie Ufalme wa Yesu, ili uweze Kuushinda ufalme wa Giza!.
Jambo la pili: KUVAA SILAHA ZOTE ZA MUNGU!.
Biblia inasema hivi, "Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho." WAEFESO 6:11-12
Biblia inasema, Tuvae silaha Zote za Mungu, ili tupate KUWEZA kuzipinga hila za Shetani,
Maana yake ni hii, kwamba unaweza ukataka kuzipinga hila za Shetani, lakini USIWEZE kuzipinga, (UKIJARIBU, HUTAPATA USHINDI),
Ili upate KUWEZA kuzipinga, lazima Uvae silaha ZOTE za Mungu!.
Jambo la tatu; LAZIMA UWE NA NGUVU ZA MUNGU ZA KUTOSHA!.
Shetani ananguvu kuliko Mtu, Mungu ana nguvu kuliko Mtu na Kuliko Shetani.
Kwa hiyo, kama Unataka Kumpinga Shetani, lazima Uwe na Nguvu za Mungu, ukiwa na nguvu zako Pekee hutaweza!.
Luka 11:21-22, biblia inasema
"Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake ni salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokua akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake."

Vitu vyako kama vimeibiwa na Shetani, alafu anavilinda visichukuliwe, wewe utakapochukua hatua ya kwenda kuvupora, lazima uwe na NGUVU KULIKO YEYE!.
Pia, hata wewe kama Ukivilinda vitu vyako (ndoa, elimu, huduma, n.k), huku umejifunga silaha zako vizuri, lakini huna nguvu za Kutosha, akija Adui, akiwa na NGUVU KULIKO WEWE, anaweza akakushinda!.
Ndio maana Mungu anasema, "Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote." ZABURI 105:4
NITAISHIA HAPO KWA LEO, SEHEMU IJAYO ITAKUA SEHEMU YA MWISHO, ITAKUA NDEFU KIDOGO, LAKINI UJITAHIHI KUISOMA,
Ahsanteni kwa Kunisikiliza!. Mungu awabariki sana!!.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#).

Comments