AINA ZA SADAKA!.

Na Mwalimu Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe, karibu tujifunze Somo hili, ambalo nimelipa Kichwa AINA ZA SADAKA, lakini ndani ya Somo hili, tutaangalia Mambo yafuatayo:
MWANZILISHI WA SADAKA
KWA NINI TUNATOA SADAKA!?.
THAMANI YA SADAKA
AINA ZA SADAKA

Najua kwa Vipengele hivyo vinne, ntaweza kupitia Maeneo Mengi yanayohusu Matoleo!.
MWANZILISHI WA SADAKA
Mwanzilishi wa Sadaka ni Mungu mwenyewe, baada ya Adam kutenda Dhambi, Mungu akamchinja Mnyama (Mwanzo 3:21), IKAWA NDIO MWANZO WA UTOAJI WA SADAKA, ingawa kwa wanadamu suala hilo, lililetwa kwenye Sheria ya Musa!.
KWA NINI TUNATOA SADAKA!?.
Unajua, Mambo haya yalikuja baada ya Dhambi, kabla hakukua na Suala la Sadaka, wala Maombi!.
Baada ya Dhambi, imekua inahitajika gharama flani ili kuupenya Ulimwengu wa roho, gharama hizo, ni Maombi, na Sadaka!.
Kama unavyojua, Mungu ni Roho, hana Mwili, kwa hiyo ukitaka uwasiliane naye lazima uingie rohoni, na daraja Mojawapo la kuingia rohoni, ni SADAKA!
Mimi nimeziandaa sababu kuu mbili, za kwa nini tunatoa sadaka!.
1.AGIZO LA MUNGU
Mungu Mwenyewe ndiye aliyetuagiza kutoa Sadaka (lakini hatulazimishi), ni hiari yako. Unaweza utoe, au Usitoe!.
(KUTOKA 25:1-2)

2.UPENDO.
Hii sababu ya pili, ndio Msingi wa Utoaji katika Agano jipya, Bila Msingi huu, chochote unachokitoa hakiitwi Sadaka, bali Msaada!.
Kwa nini nakwambia hivyo?,
Ukisoma, Yohana 3:16
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele"
Sababu ya Mungu kumtoa Yesu kama Sadaka, ilikua ni UPENDO wake kwa ulimwengu, naweza nikathubutu Kusema hivi, kama Mungu asingeupenda Ulimwengu, asingemtoa Yesu kama dhabihu ya Kuteketezwa!.
Ukisoma tena, Kutoka 25:1-2, Pamoja Mungu alitoa Agizo, lakini alitaka watu watoe kwa Moyo wa Kupenda!.
Neno la Mungu linasema, "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu". 2KOR 9:6-7
UPENDO NDIO MSINGI, WA UTOAJI, NA HALI YA MOYO WAKO NDIYO INAWEZA KUDHIHIRISHA KIWANGO CHA UPENDO ULIONAO KWA MUNGU!.
Tunamtolea Mungu, si kwa sababu tunavyo vingi, bali kwa Sababu, ya UPENDO tulionao kwa Mungu wetu!!.
Naomba, niishie hapo, lakini Somo litaendelea!.
By Mwalm Nick.
0712265856
(WhatsApp#)

Comments