BIBLIA NI NENO HAI LA MUNGU LILILOVUVIWA NA NGUVU YA MUNGU.


 
Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu nikujuze mambo muhimu ya kukuimalisha kiroho.
Leo naizungumzia Biblia.
Biblia Ni Neno La MUNGU Lililovuviwa Na MUNGU. 
Ndani Ya Biblia MUNGU Huwafunulia Watu Mapenzi Yake

2 Petro 1:20-21 '' Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa MUNGU, wakiongozwa na ROHO MTAKATIFU.''

-Kwa andiko hilo tu linaonyesha kwamba;
=Biblia hakuandika mtu kwa akili zake ila ROHO wa MUNGU ndie mwandishi wa Biblia akiwatumia wanadamu watumishi wake kama chombo tu.
=Ili tuifahamu vizuri Biblia inatakiwa tuwe tunamuuliza Mwandishi wa Biblia ambaye ni ROHO MTAKATIFU.
Watu wengi wamechanganyikiwa kwenye kuifahamu Biblia kwa sababu tu wanataka Biblia iyafuate  majira na nyakati  wanazoishi wao wanadamu na sio Majira na nyakati kuitii Biblia.

Biblia Ni Kanuni Yenye Hakika Ya Imani. 
Biblia Ni Mwongozo Wa Kuwaongoza Wateule Wa BWANA YESU Katika Maisha Yao Yote Ya Duniani.

Zaburi 119:11''Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. '' 

=Neno La MUNGU Linatakiwa Liwekwe Moyoni Na Si Pengine.
= Neno La MUNGU Ni Taa Ya Kummulikiwa Mwanadamu Ili Apite Salama. 
Kuliamini Neno La MUNGU Katika Ukweli Wake Na Kulitii Ni Lazima Kupata Uzima Wa Milele.
 BWANA YESU anasema juu ya jambo hilo kwamba
 ''Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.-Yohana 5:24 ''

Mwaka 2008 baada ya kupata ajira, wazazi wangu kule Misungwi Mwanza waliniandalia sherehe maana baada ya sherehe hiyo nilitakiwa kwenda Zanzibar kuanza ajira.
Nilikuwa sijaokoka lakini naamini kwamba siku hiyo ilizaa jambo kubwa kwangu. Katika sherehe hiyo walialikwa wachungaji watano. Baada ya chakula zilianza nasaha mbalimbali kutoka kwa Baba, Mama, ndugu na wachungaji wote. Nilikuwa siamini kilichotekea siku hiyo, hakika nilikuwa na furaha sana. Mama alikuwa wa mwisho kusema na baada ya kusema alitamka neno hili ''Peter Mwanangu nakuza zawadi ya Biblia ili ikusaidie katika maisha yako mapya na ya peke yako ukiwa Zanzibar''.
 Kesho yake Niliondoka Mwanza na kwenda Zanzibar kuanza maisha.   Neno hilo la mama nililiongea ndani yangu kwa siku kadhaa, hata maneno ya wachungaji pamoja na Baba yaliongea ndani yangu lakini hili neno la mama liliongea zaidi ndani yangu kwa sababu ya Biblia. Nilijiona nina mzigo mkubwa wa kuisoma Biblia na kufahamu kilicho ndani yake. 
Biblia ni muhimu sana kwa kila mwanadamu.
Kuisoma tu Biblia hakutoshi bali kuitii Biblia ndio ukamilifu wako.
 Kanisa Linatakiwa Lifuate Neno La MUNGU Na Sio Neno La Watu Ambao Ni Viongozi Wakuu. 
Kiblia wakati tuliopo unaitwa Wakati Huu Ni Wakati Wa Kanisa. 
Ngoja nikupe siri hii wewe msomaji wa Biblia, Ni kwamba,Ni Muhimu sana Kulifuata Agano La Jipya Na Huku  Agano La Kale Tukilisoma Kwa Jinsi Ya KRISTO. 
Kulisoma agano la kale kwa jinsi ya KRISTO ndiko kunakowatatiza wengi. Kuna wakati unaweza ukadhani Biblia inapishana lakini kwa sababu tu ya kutokumuuliza Mwandishi wa Biblia ambaye ni ROHO wa MUNGU mwenyewe unakwama. 
ROHO MTAKATIFU humushuhudia KRISTO(Yohana 15:26) na hivyo tunatakiwa tuisome Biblia katika Agano la kale kwa jinsi ya KRISTO.

Angalizo ni hili, Ni Marufuku Kuliacha Agano La Kale Na Haitakiwi Kwenye Mafundisho Yetu Tuwe Tunahubiri Agano Jipya Tu Huku Agano La Kale Tukichagua Mithali Na Zaburi Tu. 

Lengo La Biblia Ni Tumwamini YESU Ili Tupate Uzima Wa Milele; Yohana 20:31 ''Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba YESU ndiye KRISTO, Mwana wa MUNGU; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.''

Biblia ni muhimu sana na ndio kitabu cha zamani zaidi kuliko vitabu vyote duniani.
Biblia ndio kitabu pekee cha kweli na wengine wote walifuata baade na kukopi tu baadhi ya maandiko ya Biblia na kuyageuza ili wapate nafasi ya kuituhumu na kuishambulia Biblia lakini hata siku moja hawajawahi kuishinda Biblia.
Biblia ni kongwe katika vitabu lakini kwa sababu Biblia ni Neno hai la MUNGU, Biblia huwa mpya kila siku  
''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. -Waebrania 4:12''
-Japokuwa Biblia ni kongwe lakini ukweli ni kwamba vyote vitapita ila Biblia kama neno hai la MUNGU litadumu milele.
Mwenye Biblia anasema 
'' Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.-Mathayo 24:35''
Ndugu yangu unayesoma ujumbe huu nakuomba; 
- Lijue Neno la MUNGU.
-Litafakari Neno la MUNGU.
-Litendee Nazi Neno la MUNGU.
-Liishi Neno la MUNGU na litii Neno LA MUNGU.
ukifanya hivyo utaitwa heri.


 Yohana 6:63 ''Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.'' 
-Maneno ya YESU ni roho tena ni uzima.
Maneno ya YESU yako katika Biblia tu hivyo Biblia Ni Neno MUNGU tena neno la MUNGU ni roho tena ni uzima.
 
 Wanadamu wengi katika kizazi hiki wana njaa ya chakula cha mwili(Msosi) na sio chakula cha roho zao(Neno la MUNGU).
 MUNGU tusaidie ili tusome BIBLIA.
Mathayo 4:4 '' Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha MUNGU''

 Kuwa na Neno la MUNGU ndani yako ni zaidi ya kukariri maandiko mengi au machache kichwani mwako.

Hatuna Ruhusa Ya Kuongeza Wala Kupunguza Chochote Katika Biblia.
Ufunuo 22:18-19 ''Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, MUNGU atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, MUNGU atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.'' 


Kumbe ni muhimu sana kila mtu kulitumia Neno la MUNGU kwa halali.
Kuna baadhi ya makanisa waibadili Biblia ili tu iwasapoti katika uongo wao, naomba walisome hilo andiko hapo juu.
Kuna watu kwa sababu ya uongo wanaouamini ambao uko kinyume na Biblia husoma maandiko ambayo tu hayawakemei katika kile ambacho wanakikosea.
Mtumishi ni vizuri kulitumia kwa halali neno la MUNGU.

2 Timotheo 2:15 ''Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli''

Neno la MUNGU ni la MUNGU tu hivyo hatutakiwi kuligeuza kwa vivyote.
Neno Ni La Milele 
1 Petr 1:25 ''Bali Neno la BWANA hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.''

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments