JE MAISHA UNAYOYAISHI NDIO MAISHA YAKO HALISI MUNGU ALIYOKUANDALIA?(1)


Na Mtumishi Samwel Kibiriti


Namshukuru Mungu kwa nafasi hii ambayo kanipatia kukuletea masomo mbalimbali kwenye page Yangu hii.
Somo hili nimeliweka kwenye mfumo wa swali nikikuuliza kwamba je hayo maisha unayoyaishi Leo ndio maisha yako Mungu aliyokuandalia uyaishi? Au unaishi maisha ambayo sio yakwako?.

Leo hii ukimuuliza kila mtu kwamba hayo maisha anayoishi ndio Mungu kampangia atasema ndio na wengine watasema hawajui, ila unaposoma Neno la Mungu Biblia linatuonyesha maisha yetu halisi tunayotakiwa tuyaishi tukiwa hapa duniani ambayo Mungu ametupangia na kutuandalia.
Nataka nikuulize swali hili je wewe unafikiri maisha ya MTU yanaanzia kipindi gani kabla hajatungishwa mimba? Au akiwa tumboni mwa mama yake? Au akizaliwa? Au akimaliza shule?
Nitahitaji majibu yako ila Mimi nitakupatia majibu ya swali hii katika sehemu ya pili ya somo hili ambapo nitakuonyesha kwamba maisha ya MTU huanzia wakati gani.


Ukisoma Neno la Mungu unaona likiweka wazi kabisa kwamba maisha ya mwanadamu hayaanzii akizaliwa bali Mungu huyaandaa maisha ya mwanadamu hata kabla hajatungishwa mimba tumboni mwa mama yake.
Ukisoma Biblia kitabu cha YEREMIA 1:4-5 Neno la Mungu linasema. "Neno la BWANA lilinijia kusema kabla sijakuumba NDANI ya tumbo la mama yako nilikujua, na kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa". Umeona hapa Mungu anamwambia Yeremia kwamba alimjua hata kabla hajaingia ndani ya tumbo la mama yake na akamwandalia maisha atakayoyaishi hapa duniani akizaliwa.
Hata wewe fahamu kwamba Mungu alikuandalia maisha yako ya kuyaishi hapa duniani hata kabla hujatungishwa mimba tumboni mwa mama yako, na lengo la Mungu kuruhusu Uzaliwe hapa duniani niili wewe uyaishi maisha yako aliyokuandalia, lakini je wewe Leo hii unayaishi hayo maisha Mungu aliyokuandalia au unaishi maisha ya kopi yasiyo halisi?
Ukisoma pia kitabu cha WAEFESO 1:4 Inasema "Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu......" Kwahiyo Mungu alikuchagua hata kabla hajaumba hii dunia. Tusome pia WARUMI 8;29 Inasema "Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake......".
Umeona bado Mungu anasema alituchagua tokea asili, kwahiyo nataka ufahamu tu kwamba maisha yako Mungu alikuandalia hata kabla hujaingia tumboni mwa mama yako na amekuleta hapa duniani ili uyaishi hayo maisha yako aliyokuandalia umeelewa?

Nasikitika kusema kwamba wanadamu wengi sana sana waliopo duniani hawaishi maisha yao halisi ambayo Mungu kawaandalia wayaishi hata kabla ya kutungishwa mimba Bali wanaishi maisha yasiyo yakwao au wanaishi maisha ambayo ni photocopy Yale maisha halisi yameibiwa kwao.
Je wewe rafiki Yangu unaishi maisha yako halisi au unaishi maisha ya photocopy?

Utaniuliza kivipi mtumishi ngoja nikusaidie kama unaishi maisha kama haya yafuatayo ujue umenyanganywa maisha yako halisi mfano: kuishi maisha ya mateso, maisha ya magonjwa, maisha ya kuhangaika na kusumbuka kupata mahitaji, maisha ya kukosa kazi pamoja na kusoma, kupata hasara kwenye biashara NA kazini, kuishi maisha ya huzuni, kuonewa, masikitiko, n.k
Sasa najua swali lako unajiuliza kwamba kama Mungu kaniandalia maisha Yangu hata kabla sijaingia tumboni mwa mama Yangu mbona hayo maisha siyaoni? 


Jambo la kwanza:
Kuishi kwenye maisha ya dhambi.

Kumbuka kwamba dhambi ni roho kwahiyo unapoishi kwenye dhambi nikwamba hiyo roho ya dhambi itakutoa nje ya maisha yako halisi uliyotakiwa na Mungu uyaishi.
Mfano (Mwanzo 4:6-7,12-16)
Kaini alipofanya dhambi ya kumuua ndugu yake Habili alijikuta anatoka nje ya maisha yake halisi na kujikuta anaishi maisha ya kutangatanga yasiyo na baraka za Mungu.

Mfano (Mwanzo 2:8-9,15-17, 3:23-24)
Mungu alikuwa amemwandalia Adamu maisha mazuri kwenye bustani yaEdeni, lakini alipofanya dhambi akajikuta Mungu anamfukuza atoke nje ya maisha yake halisi na kujikuta anaishi maisha ya mateso.
Nataka ufahamu kwamba dhambi unapozifanya utajikuta unaishi nje ya maisha yako hailisi uliyopangiwa na Mungu na kujikuta unaishi maisha ya mateso na matatizo mbalimbali.
Kumbuka Bwana Yesu alisema katika Yohana 8:34 kwamba kila atendae dhambi ni mtumwa wa dhambi, akiwa na maana kwamba dhambi inaweza kumtumikisha mtu anayeifanya.

Ushauri kwangu kwako nikwamba kama unaishi maisha ya dhambi achana nayo sasa na umgeukie Mungu wako na kuishi maisha ya Utakatifu kila siku. Nakama unaona kuacha dhambi huwezi basi tafuta msaada kwa watumishi wa Mungu watakuombea na kukufungua kwenye hicho kifungo cha dhambi inayokutumikisha.


Jambo la pili;
Kufanya ibada za Miungu mingine na kuomba wafu.

Wako watu ambao wamejikuta hawaishi maisha yao halisi kutokana nawao kuabudu Miungu mingine na kuwaomba wafu au wametokea kwenye familia na koo zinazofanya hivyo.
OK utaniuliza kivipi mtumishi kibiriti?

Ukisoma Biblia kitabu cha KUTOKA 20:3-5 Utaona Mungu amekataza mwanadamu asiabudu Miungu yoyote ile au kitu chochote kile zaidi yake , unajua nikwanini Mungu kaweka Amri hiyo?
Jibu nikwamba mtu au familia au ukoo wakiabudu Miungu mingine zaidi ya kumuabudu Yeye Mungu aliye hai kinachotokea kwenye ulimwengu wa roho nikwamba hizo roho za Miungu zinazoabudiwa zinawapokonya hao watu maisha yao halisi walioandaliwa na Mungu nakujikuta wanaishi maisha yasiyo yao kabisa Bali huishi maisha ya photocopy.

Ukisoma kitabu cha WAAMUZI 6:11-26 Utamkuta MTU anayeitwa Gidioni wakati Malaika wa Mungu anamtokea alimkuta anapepeta ngano, sasa nikuulize Yale maisha ya Gidioni ya kupepeta ngano yalikuwa maisha yake aliyopangiwa na Mungu?
Jibu nikwamba hayo maisha Gidioni aliyokuwa anaishi sio maisha yake halisi bali alikuwa anaishi maisha yasiyokuwa yakwake, na Yale maisha yake halisi yalifichwa na madhabahu za Miungu zilizokuwa nyumbani kwao.
Ndio maana nilikuambia unaweza kujikuta unaishi maisha yasiyo yako halisi kama kwenye familia na ukoo wenu wanaabudu au waliabudu Miungu mingine Mnajikuta maisha yenu halisi yamefichwa na roho hizo za Miungu.

Hebu angalia maisha yako naya ndugu zako ndani ya familia na ukoo yanafanana, kwa mfano watu wote kila mmoja analalamikia maisha, au kukosa ajila, kuteseka n.k hayo mazingira yanaonyesha kwamba maisha hayo unayoishi sio yakwako.
 Jambo laTatu
Nafsi yako kufungwa kwenye ulimwengu wa Giza.

Wako watu ambao hawaishi Yale maisha yao halisi walioandaliwa na Mungu hata kabla ya kutungishwa mimba matumboni mwa mama zao kwasababu kwenye ulimwengu wa roho upande wa Giza wamezishika na kuzifunga Nafsi zao
Ngoja nikueleze rafiki Yangu kama Nafsi yako imefungwa kwenye ulimwengu wa Giza utajikuta unaishi maisha ambayo sio Yale Mungu aliyokuandalia Bali utaishi maisha ya mateso na mahangaiko huku kila siku ukiwa unalalamikia hali ngumu ya uchumi na maisha.
Siunajua kwamba Nafsi ya mwanadamu ndio iliyobeba maisha yake? Yaani kwamba Kiwango chako cha maisha Mungu aliyokupangia uyaishi kiko ndani ya Nafsi pia Nafsi ndio inayoamua uwe na aina gani ya maisha.

Sasa ukisoma ZABURI 121:7 Inaeleza kwamba chanzo cha mambo mabaya ni nafsi. Ukisoma pia ZABURI 124:7 Inaeleza kwamba shetani kazi yake ni kuweka mitego ya kuzinasa Nafsi za watu. Soma pia ZABURI 142:7 Inaeleza kwamba Nafsi inaweza kuwekwa KIFUNGONI. soma tena ZABURI 143:3,12 Inaeleza kwamba Maadui wanazifuatilia Nafsi za watu na kuziweka gizani. Pia ukienda kusoma ZABURI 7:5 Inasema Nafsi inaweza kukamatwa.
Sasa hiyo ni baadhi tu ya mistake ndani ya Biblia inayoonyesha kuhusu kitu gani kinaweza kufanywa kwenye nafsi ya mwanadamu na ulimwengu wa Giza.
Nataka nikuulize je wewe Nafsi yako iko sawa au tayari imefungwa kwenye ulimwengu wa Giza?. Kama imefungwa haijalishi utafanya kazi sana lakini mafanikio hutayaona.

Ngoja nikusaidie utajuaje kama Nafsi yako imefungwa mambo haya yafuatayo ni ishara kusoma bila kupata kazi, kufanya kazi sana bila kuona mafanikio, kuchukiwa na watu bila sababu, kutoolewa au kuoa kwa muda muafaka, kufeli kwenye mitihani pamoja na kusahau na kutoelewa, kuahidiwa ahadi lakini hazikamiliki
Kuota unafanyishwa kazi na watu, kuchukuliwa na watu ndotoni, kutopandishwa cheo kazini pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuanzisha jambo lakini halifikii mwisho, kuteseka na magonjwa, n.k
Kama mambo hayo yako maishani mwako tafuta haraka msaada wa maombi.
Itaendeleeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Pia unaweza kuwasiliana nami 

+255 765 867575 au Email samwelikibiriti@ gmail.com

Comments