JE MAISHA UNAYOYAISHI NDIO MAISHA YAKO HALISI MUNGU ALIYOKUTAKA UYAISHI?(2)




Na Mtumishi Samwel Kibiriti.

Kutoka na vitu visivyofaa tumboni mwa mama yako.

Wako watu ambao hawayaishi maisha yao halisi kutokana na kutoka na vitu visivyofaa matumboni mwa mama zao, pia wengine maisha yao halisi yalibadilishwa wakiwa matumboni mwa mama zao.
Ukisoma kitabu cha YEREMIA 1:4-5 Utaona Mungu akimtakasa Yeremia akiwa ndani ya tumbo la mama yake, unafahamu nikwanini Mungu amtakase akiwa tumboni?
Mungu kumtakasa Yeremia akiwa tumboni mwa mama yake alikuwa anafanya kazi ya kumtenga na vitu visivyofaa ambavyo angetoka navyo ndani ya tumbo la mama yake, na vitu hivyo vingemtesa Yeremia katika Utumishi ambao Mungu amempatia.

Soma pia WAGALATIA 1:13-16 Utamuona Mtume Paulo nayeye anasema Mungu alimtenga tokea tumboni mwa mama yake, kwanini Mungu alimtenga? Nikwasababu kuna vitu visivyofaa angetoka navyo.
Soma pia MWANZO 25:20-26 Utaona kwamba hapa maisha ya Yakobo na Esau ndugu hawa yalibadilishwa wakiwa tumboni mwa mama zao.
Kwahiyo unaweza kujikuta umenyanganywa na shetani maisha yako halisi uliyotakiwa uyaishi ulipokuwa tumboni mwa mama yako.

Soma pia MATENDO YA MITUME 3:1-2, 14:8-10 Hawa watu walipata shida ya ukiwete wakiwa matumboni mwa mama zao. Ukisoma YOHANA 9:1-2 Utamuona huyu mtu alikuwa kipofu tokea tumboni mwa mama yake.
ZABURI 58:3 Biblia inaeleza wazi kwamba mtoto akiwa tumboni mwa mama yake anaweza kujifunza kusema uongo, kwahiyo huyo mtoto utamkuta anaishi na roho aliyoipata tumboni mwa mama yake
Nimalizie kwa kukuuliza swali hili je wewe ulipozaliwa ulitoka na vitu gani visivyofaa tumboni mwa mama yako? Pia je shetani hajakunyanganya maisha yako ulipokuwa tumboni mwa mama yako?
Sikiliza kama kuna vitu ambavyo Mungu hakutaka uzaliwe navyo lakini ukajikuta umezaliwa navyo vitakutesa sana maishani mwako na kujikuta unaishi maisha yasiyo yako halisi.
Jambo la kufanya waone watumishi wa Mungu wakuombee


Sasa baada ya kukuonyesha mambo kadhaa yanayoweza kukufanya usiyaishi maisha yako halisi uliyopangiwa na Mungu uyaishi hapa duniani, nataka nikupe mambo ya msingi ya kuyajua kisha uyaingize kwenye maombi.
1. Ili Mungu aweze kukurudisha kwenye maisha yako halisi nilazima jambo LA kwanza ukubali KUOKOKA ili Bwana Yesu awe kiongozi na Mchungaji wako
Kwahiyo kama bado hujaokoka waone watumishi wa Mungu ili wakuongoze sala ya Toba, au unaweza wasiliana nami.

2. Jambo la pili baada ya kuokoka nilazima uishi maisha MATAKATIFU usiwe ni mtu wa kijichangaja, Mara uko kwa Yesu na kwenye dhambi.
3. Jambo la tatu hakikisha unafanya maombi ya kujitenga na ROHO ZA MIZIMU ya familia yenu na ukoo wenu upande wa baba yako na upande wa mama yako kwa kutumia Damu ya Yesu kristo.
Kumbuka kwamba roho za mizumu ya familia na ukoo na kabila lenu zinaweza kukufunga usiweze kuyaishi Yale maisha yako halisi uliyoandaliwa na Mungu uyaishi, ndio maana nikwa kueleza kwamba Fanya MAOMBI ya kujitenga na hizo roho za mizimu kwa kutumia DAMU YA YESU KRISTO na Jina la YESU KRISTO.

4. Vunja roho zote za asili ya kwenu zilizokamata maisha yako halisi
5. Vunja misingi yote ya vizazi ambayo imeyaficha maisha yako halisi uliyotakiwa na Mungu Baba uyaishi
6. Muombe Bwana Yesu kwa kupitia Damu yake ayakomboe na kuyafungua maisha yako halisi kisha akuingize kwenye maisha yako halisi ili uanze sasa kuyaishi.
7. Ukishamaliza kufanya hayo maombi anza sasa kila siku kumshukuru Mungu aliye Hai kwa kuyafungua maisha yako na kukurejesha kwenye maisha yako halisi aliyokuandalia hata kabla hujatungishwa mimba tumboni mwa mama yako.
Huo ndio muongozo mfupi wa wewe kufanya maombi ili uweze kurejea katika kuyaishi maisha yako halisi.
Kama endapo utashindwa kuyafanya hayo maombi unaweza kuwasiliana namimi ili niweze kukufanyia hayo maombi ya kuyafungua maisha yako halisi ambayo Mungu alikuandalia ili uyaishi


Unaweza kuwasiliana nami kwa mawasiliano haya;
Simu: +255 765 867574
Email: samwelikibiriti@gmail.com.com
Pia utanipata kwenye WhatssAp kwa namba hiyo.

Hapa ndio mwisho wa somo hili la kwanza jiandae kwa somo la pili.
NAKUTANGAZIA KUANZIA MUDA HUU MUNGU WANGU NINAYEMTUMIKIA KATIKA KRISTO YESU AYAFUNGUE MAISHA YAKO NA KUKUREJESHA KWENYE MAISHA YAKO HALISI ALIYOKUANDALIA ILI UYAISHI

Comments