JE! MALANGO YAKO YA KIROHO YANATUMIWA NA NANI NA KUPITISHA VITU GANI KUJA MAISHANI MWAKO?.

Na Mwl Samweli Kibiriti

Katika somo hili la pili tutapita kujifunza eneo hili la malango kiroho. Kila mwanadamu anayo malango yake kiroho na yanatumika kupitisha vitu kuja kwenye maisha yake aidha vizuri au vibaya.
Malango ni nini?
Kwa tafsiri lahisi nikwamba Malango ni eneo lililopo kwenye ulimwengu wa roho ambalo anaweza kulitumia MUNGU au shetani kuingiza vitu au kuingia mahali kwenye ulimwengu wa mwili".

Maana yake nikwamba ili vitu vilivyoko kwenye ulimwengu wa roho viingie kwenye ulimwengu wa mwili huwa vinapitia kwenye malango. Pia nataka ufahamu kwamba MUNGU na ufalme wake au shetani na ufalme wake mmoja wapo ndie mmiliki na mtawala wa malango yako na kuna vitu atavipitisha hapo kuja kwenye maisha yako aidha vizuri au vibaya.
Ukisoma ZABURI 24:7-10 Utaona Biblia inaweka wazi kwamba malango huwa yanasikia kabisa kiroho ndio maana hapa yanasemeshwa ili yainua vichwa juu kwa yameinama. Utajiuliza kwamba nikwa nini yameinama?
Jibu lake nihili yameinama kwasababu yalikuwa yanatumiwa na shetani ndio maana hapa yanasemeshwa yainue vichwa juu ili Yesu kristo kama mfalme aingie na kuyatumia haleluya.

Sasa nikuulize je wewe malango yako yakiroho yameinama au yameinuka? Na je ninani anayeyatumia ni Yesu kristo au ni shetani? Tuendelee kuwa pamoja utanielewa huku mbele ya somo hili.
Ukisoma kitabu cha NEHEMIA 12:30 Biblia inasema "Makuhani na Walawi wakajitakasa, nao wakawatakasa watu, na Malango na Ukuta". Nataka nikuulize swali nikwanini hawa makuhani walitakasa malango na kuta za Yerusalem?
Sasa hapa somo letu linahusu malango hebu tuache hili eneo la ukuta nitalifundisha siku nyingine. Sasa hawa Makuhani na Walawi kutakasa malango ya mji wa Yerusalemu maana yake nikwamba kiroho kuna vitu visivyofaa ambavyo vilikuwa vinapita kwenye hayo malango, kwahiyo waliyatakasa ili kuyatenga kwa ajili ya kusudi la MUNGU ili yeye ayatumie.

Ukisoma kitabu cha KUMBUKUMBU LA TORATI 28:52-55 utaona Biblia imeweka wazi kabisa kwamba Adui au shetani huwa anakamata malango ya MTU au eneo na kuyakaza kiroho. Sasa nataka ufahamu jambo hili kwamba Shetani akitaka kukutesa kwenye kila eneo la maisha yako huwa anayatafuta malango yako kiroho na akiyapata anayakaza nawewe kujikuta huku kwenye ulimwengu wa mwili unateseka na kupata shida, pia ataingiza vitu vyake visivyofaa kwenye malango yako ili azidi kukutesa.
Sikiliza nikwambie shetani akikamata malango yako ya uchumi atakutesa sana kwenye eneo lako LA uchumi na kujikuta husongi mbele, akikamata malango ya familia ataitesa sana hiyo familia kwenye kila eneo na wote waliomo ndani. Akikamata malango ya Afya yako atakutesa sana na magonjwa.
Shetani akikamata malango ya biashhara yako atahakikisha hiyo biashara haisongi mbele wala hupati wateja, akikamata malango ya Ndoa yako atahakikisha unaishi kwenye ndoa ya machungu na kutokupata watoto. Akikamata malango ya Elimu atahakikisha wanafunzi wanafeli na kushindwa kwenye masomo na mitihani, akikamata malango ya kanisa atahakikisha halisongi mbele na kuongezeka.
Nataka ufĂ hamu tu kwamba hauolewi na kuoa kwasababu shetani ameshikilia malango yako na uko hivyo ulivyo kwenye maisha ya matatizo kwasababu shetani kakamata malango yako kiroho.
Katika sehemu ya pili ya somo hili nitaanza kuingia ndani na kukuonyesha aina mbalimbali za malango ya vitu vinavyopita hapo.

Baada ya kukuletea utangulizi wa somo hili nataka tupige hatua twende mbele kidogo. Nilisema kwamba malango ya kiroho yanaweza kutumiwa na Mungu au shetani kuingiza vitu kutoka ulimwengu wa roho na kuja maishani mwako. Sikiliza Leo unaishi maisha ya shida na mateso nikwasababu shetani kayakamata malango yako na kuna vitu visivyofaa anaviingiza maishani mwako.

Leo wako mabinti wengi hawaolewi au uchumba unaharibika bila kuelewa tatizo ni nini pia wako vijana wa kiume hawaoi bila kuelewa sababu ni nini, ngoja nikuweke wazi rafiki yangu kama endapo shetani kakamata malango yako ya kuoa au kuolewa au uchumba nikwamba atahakikisha kwamba hupati huoi au kuolewa pia ukiwa kwenye uchumba atauvuruga na kuhakikisha hamfikii lengo LA kuingia kwenye ndoa.
Ndio maana unaweza kumkuta binti ni mzuri na yuko na sifa zote za kuolewa lakini haolewi nahuku umri ukizidi kwenda mbele mpaka anajikuta anakata tamaa ya kuolewa na kuamua kuzaa tu na mwanaume yoyote yule.

Ukisoma MITHALI 31:23 Inasema "Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee Wa nchi". Hapa unaona huyu mwanaume yuko malangoni, sasa fahamu jambo hili shetani akimzuia mume wako wa kukuoa kwenye malango utaomba sana wala hatokei na kujikuta unakata tamaa kumbe MUNGU amesha kujibu na kukupa mume wako ila kazuiwa kwenye malango yako ya kuolewa ndio maana humuoni, jambo LA kufanya wewe ni kushughulikia hayo malango ili yamuachie Mume wako au Mke wako.
Hebu tusome pia MHUBIRI 12:4 Inasema "Na milango kufungwa katika njia kuu......". Hapa kuna jambo nataka tujifunze unaona Biblia inasema kuna milango iliyopo njia kuu lakini imefungwa, nataka kusema hivi kwenye mji unaoishi na kufanyia kazi zako za mikono kuna malango yako kwenye hizo njia kuu za mji uliopo sasa shetani akifanikiwa kukamata malango yaliyopo kwenye hizo njia kuu kwenye huo mji atahakikisha watu wanaotumia hayo malango wanaishi maisha ya mateso.
Unaweza ukawa hujanielewa nihivi malango yaliyopo kwenye njia kuu za mji uliopo yanahusika kabisa na maisha yako. OK wewe unafikili nikwanini kuna miji ukiingia hao watu wote wenyeji na wageni ni kulalamika tu masaa yote kuhusu maisha? Ukishaona hivyo ujue kwamba kwenye ulimwengu wa roho kuna malango yao ambayo shetani ameyakaza ndio maana wanabakia kulalamika na kuteseka.
Wewe unafikili nikwanini wako watu wanaoanzisha biashara na hazidumu zinakufa au haziwapi faida? Nenda kacheki malango ya huo mji kwamba yanamilikiwa na nani ni MUNGU au shetani.

Kwa Leo tuishie hapo kwenye sehemu ijayo nitakuonyesha vitu vinavyopita malangoni. Usikose kuendelea kufuatilia somo hili.
Kama uko na maswali au unahitaji ushauri au maombezi kuhusiana na tatizo lolote ulilonalo usisite kuwasiliana nami kwa Mawasiliano haya
Simu ni +255 765 867574 na kwa Email ni: Samwelikibiriti@gmail.com.

MUNGU WA MBINGU NA NCHI AZIDI KUKUHUDUMIA

Comments