JE, TARAJIO LAKO NI UZIMA WA MILELE?



Na Mtumishi Peter M Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kila mtu ana hitaji lake kubwa ambalo anataka atendewe muujiza na MUNGU wa mbinguni.

Ni kweli kabisa hitaji hilo ndilo ambayo linamuumiza sana ndugu huyu.

Kuna Mwanamke  hitaji lake kubwa siku zote anaomba apate Mume.

Kuna kijana hitaji lake kubwa anaomba apate kazi.
Kuna ndugu hitaji lake kubwa ni ndoa, kuna mwingine hitaji lake kubwa ni uchumi, kuna ndugu mwingine hitaji lake kubwa ni kupata mtoto N.k
Ni kweli hitaji hilo ndilo kubwa kwake na linamuliza kila siku,  lakini naomba niseme kwamba hakuna hitaji kubwa kama kuingia uzima wa milele.
1 Yohana 5:11-13 ''Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba MUNGU alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa MUNGU hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa MUNGU.'' 
Chanzo cha uzima wa milele ni kumpokea Mwana wa MUNGU YESU KRISTO.
Kama kuna hitaji la muhimu zaidi mwanadamu analotakiwa kuliombea au kulihitaji basi ni uzima wa milele.
Uzima wa milele hauko nje na YESU KRISTO.
Uzima wa milele ni muhimu sana.
Uzima wa milele hutafutwa.
''Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.-Mathato 6:33 '' 
Hakika ufalme wa MUNGU ni muhimu sana na hutafutwa lakini cha ajabu wanadamu walio wengi hutafuta baraka zao tu huku wakiwa hawauhitaji uzima wa milele.
MUNGU anasema tuutafute kwanza ufalme wake maana ufalme wa MUNGU ndio muhimu zaidi kwetu kuliko baraka zingine zote.
ukihubiri neno la baraka utapata marafiki wengi sana na hakika huduma yako itachanua sana lakini ukihubiri watu kuacha dhambi na kutubu utapata wakukusapoti wachache sana.
Dunia inapenda baraka za muda tu badala ya kupenda uzima wa milele ambao ni wa milele.
Kumpokea YESU na kumtumikia ni faida kubwa sana kwako.
Kumtumikia YESU kutakupa kibali na utampendeza MUNGU.

Warumi 14:18 '' Kwa kuwa yeye amtumikiaye KRISTO katika mambo hayo humpendeza MUNGU, tena hukubaliwa na wanadamu.'' 
 
Kama kuna hitaji ambalo linatakiwa tuliombee sana basi ni hitaji la kupata uzima wa milele.
Ya dunia yatapita yote.
Ndoa itapita, mali zitapia lakini uzima wa milele hautapita.
Ndugu hata kama unaombea hitaji lako nakuomba kumbuka pia kulia kwa ajili ya ndugu zako ambao wanatenda dhambi na majina yao hayomo katika kitabu cha  uzima wa milele.
Lia kwa ajili ya ndugu zako ambao hawataki kuokoka japokuwa wanajua kabisa kumkataa YESU ni kuukataa uzima wa milele.
Mathayo 25:46 '' Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.'' 
Watenda dhambi wataingia katika adhabu ya milele bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Mambo hayo mawili ndio yako mbele ya kila mwanadamu yaani mbele yako kuna jehanamu au uzima wa milele.
Ni heri kuchagua uzima wa milele kwa kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kuna umuhimu mkubwa sana kwa kila mtu kuhitaji uzima wa milele,  na ili kuupata uzima wa milele ni kuokoka na kisha kuanza kuishi maisha matakatifu.  huko ndiko kuwa mwenye haki hata ukapata uzima wa milele.
Mtu akikuambia kwamba kati ya furaha ya miaka 60 na furaha ya miaka zaidi ya Bilioni kumi utachagua nini?
Naamini utachagua miaka zaidi ya Bilioni kumi.
Huo ni mfano kati furaha ya muda mfupi ukiishi duniani na furaha ya milele naamini utachagua furaha ya milele.
Uzima wa milele ni jambo la kwanza la muhimu sana kwa kila mwanadamu.
Watu wengi wamekataa kubadili mfumo wao wa maisha ili tu wasipate uzima wa milele.
Lakini Biblia inasema neno hili katika siku ya mwisho 
''Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.-Danieli 12:2''

Kila mwanadamu anayeokoka anatakiwa kwanza awaze uzima wa milele na sio kuwaza mengine.
Lia kwa ajili ya watoto wako ili wapate neema ya kumpokea YESU
Lia kwa ajili ya ndugu  zako ili wapate neema ya kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu.
BWANA YESU ndiye pekee wa uzima wa milele.
ukimpata YESU umepata uzima na baraka za ki-MUNGU.
Ukimpata YESU umepata uzima na baraka za ulinzi wa MUNGU.
BWANA yu karibu kuja ili kumlipa kila mtu sawasawa na matendo yake.
Ndugu lia kwanza kwa ajili ya ufalme wa MUNGU kwamba usikupite.
usikupite.
 '' Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.-Mathayo 6:33 ''
-Ufalme wa MUNGU ndio muhimu zaidi kwa kila mwanadamu kabla ya maombi mengine yote.  

Mtu akitamani uzima wa milele ni lazima achukue hatua ya kuufuata uliko, na uzima huo hauko kwingine ila ni kwa YESU KRISTO, hivyo anayeutaka uzima wa milele mwambieni ajisalimishe kwa YESU ili aandikwe jina lake kwenye orodha ya waenda uzima wa milele. baada ya kuandikwa jina lake kwenye kitabu cha uzima anatakiwa pia akumbuke kwamba kama ataendelea na maovu jina hilo litaondolewa kwenye orodha ya waenda uzima wa milele.
Warumi 6:23 '' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA  wetu.'' 

Kumbe ni muhimu kujua kwamba Ingawa ni kweli kabisa MBINGU MPYA inawasubiri watakatifu lakini pia ni muhimu kukumbuka kwamba ZIWA LA MOTO linawasubiri watenda dhambi.
Wakati wa kuishi duniani ndio wakati wa kuamua sehemu ya kwenda baada ya kuondoka duniani.
BWANA YESU anakusubiri kwenye MBINGU MPYA kama tu utakubali kumpokea na kuliishi Neno lake.
Hakikisha unautafuta kwanza ufalme wa MUNGU kwa wewe kuokoka na kuacha dhambi.

Licha ya hayo yote tuliyojifunza lakini pia Jitahidi sana jina lako lisiwe kwenye chupa za soda tu bali Liandikwe kwenye kitabu cha uzima wa Milele .
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments