KAFARA YA UTAWALA


 
 
Ufufuo na uzima Morogoro

Na:     STEVEN NAMPUNJU (RP)
& DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi: Kabla ya kufahamu undani wa kafara ya utawala, je kafara ni kitu gani? Kafara ni kitu kinachotolewa kwa Mungu au kwa mizimu kama sadaka, kwa ajili ya kuepukana na balaa fulani. Baadhi ya watu wasiomjua Mungu, mara nyingi  huenda kwa wazee wao vijijini ili  kutoa kafara ili  kupata jambo fulani. Kafara huambatana na KUMWAGA DAMU. Kafara haihusiani na kutoa sadaka ya ndizi, matunda au chochote kile  kisichokuwa na damu. Makundi  makubwa ya Damu zinapomwagwa: (1) Damu hunena mema au (2) Damu hunena mabaya.

Vipo vitu kama vitatu hivi vya kujifunza kuhusiana na damu:
1.      Damu inao uwezo wa kutoa sauti: Damu iliyomwagika mahali popoteinaweza kupaza sauti na wengine wakaitafsiri sauti hiyo.
2.      Damu inaweza kuomboleza: Kupitia damu yamtu au mnyama, damu  yaweza kutoa sauti ya kuomboleza kwa uchungu wa kumwagika kwake.
3.      Mungu  ana uwezo wakuisikia sauti  inayopazwa na Damu na kuweza kutoa tafsiri yake: Mfano: MWANZO 4:9-10….[Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.]… Kaini alijua yale mauaji aliyofmfanyia ndugu yake ni siri. Mungu lakini aliweza kuisikia sauti ya damu ya Habili na kutoa tafsiri yake. Tafsiri hii  inaweza kuleta madhara kwa mtu  fulani anayeishi.
Imeandikwa katika 2KORINTHO 4:4….[ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.]… Wapo watu wanaweza kumwaga damu kwa malengo yao hapa duniani. Ni  kwa sababu mungu  wa dunia hii amepofusha fikra zao. Kumbe mungu  wa dunia hii anaweza kupofusha fikra za wasiaoamini,  na hivyo kuficha ile nuru ya injili ili isiwazukie.  
Imeandikwa katika WALAWI 17:14…[Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.]… Kumbe basi ndani  ya damu ndipo uhai ulipo.  Kafara inapotolewa ni sawa na kuutoa uhai wa kile kilichotolewa.
MADHARA YA UMWAGAJI DAMU YA MWANADAMU

·        Amwagae damu ya mwanadamu, damu yake nayo  itamwagwa: Imeandikwa katika MWANZO 9:6…[Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.].
·        Hatima ya mtu inaweza kubadilishwa kwa kmwaga  damu   ya mwanadamu: Maana yake,  damu ya mtu mmoja ikimwagwa, hata hatima ya mtu huyo au  taifa lake inaweza kubatilishwa.

Imeandikwa katika MWANZO4:1-12….[Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. 2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. 8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]*. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.]… Jina la Kaini lilikuwa na tafsiri  ya “mtoto atokaye kwa Bwana”. Hatima ya Kaini ilibadilishwa kwa sababu hii ya kumuua ndugu yake, badala ya kuwa mtu wa kutulia ikambidi awe  mtoro na mtu asiye  na makazi. Unapomuona mtu leo hii,  ni mtoro katika maisha yake, ujue kuna sadaka ya damu  ilimwagwa kwa ajili yake wakati fulani akiwa anajua au bila yeye kujua. Utoro  waweza kuwa kwenye biashara, kwamba kila akifanya biashara yake mji  huu anaacha na kuanza kitu  kingine kipya,  na au kuhamia mji mwingine kuanzisha kitu kingine kipya bila mafanikio yapatiakanayo kwa kukaa mahali pamoja na kutulia.

MIFANO YA WATAWALA WALIOAWAHI KUTOA KAFARA
1.      HIELI MBETHELI

Hieli Mbetheli aliwatoa kafara  wanae wawili  kwa nyakati tofauti ili mambo ya ufalme/utawala wake yaende vizuri. Imeandikwa katika YOSHUA 6:26…[Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.]…

1WAFALME 16:34….[Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.]…Inawezekana mfalme aliambiwa kuhusu katazo la Yoshua, lakini kwa kutaka nguvu ya uongozi wake, akaona aendele tu kutoa kafara za wanae wawili  ili kudumisha utawala wake.

Imeandikwa katika 2WAFALME 3:4-10…[Basi Mesha, mfalme wa Moabu, alikuwa mfuga kondoo; naye alikuwa akimlipa mfalme wa Israeli sufu ya wanakondoo elfu mia, na ya kondoo waume elfu mia. 5 Lakini ikawa, Ahabu alipokufa, mfalme wa Moabu akamwasi mfalme wa Israeli. 6 Akatoka wakati ule ule mfalme Yoramu katika Samaria, akawahesabu Israeli wote. 7 Akaenda akatuma kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akasema, Mfalme wa Moabu ameniasi; je! Utakwenda pamoja nami tupigane na Moabu? Akasema, Nitakwenda; mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi zangu ni kama farasi zako. 8 Akauliza, Njia ipi tuiendee? Akajibu, Njia ya jangwa la Edomu. 9 Basi mfalme wa Israeli akaenda, na mfalme wa Yuda, na mfalme wa Edomu; wakazunguka mwendo wa siku saba; wala hapakuwa na maji kwa jeshi, wala kwa wanyama waliowafuata. 10 Mfalme wa Israeli akasema, Ole wetu! Kwani Bwana amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.]…Kule jangwani wanajeshi walikuwa hawana maji ya kunywa.

Imeandikwa katika 2WAFALME 3:4-11-17…[Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hapana hapa nabii wa Bwana, ili tumwulize Bwana kwa yeye? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya. 12 Yehoshafati akasema, Neno la Bwana analo huyu. Basi mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, na mfalme wa Edomu, wakamshukia. 13 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa Bwana amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu. 14 Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. 15 Ila sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga, mkono wa Bwana ukamjia juu yake. 16 Akasema, Bwana asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki. 17 Kwa kuwa Bwana asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji;    nanyi mtakunywa, ninyi, na ng'ombe zenu, na wanyama wenu. 18 Na jambo hili ni jepesi machoni pa Bwana; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu. 19 Nanyi mtapiga kila mji wenye boma, na kila mji ulio mzuri, na kila mti mwema mtaukata,   na chemchemi zote za maji mtaziziba, na kila mahali palipo pema mtapaharibu kwa mawe. 20 Ikawa asubuhi, wakati wa kutoa sadaka ya unga, tazama, maji yakaja kwa njia ya Edomu, hata nchi ikajaa maji..]… Unapokuwa na changamoto za maisha usiwaendee waganga wa kienyeji, bali umfuate mtumishi wa Bwana. Elisha aliwajibu waandae mahandaki ili watu wakae ndani yake na wakitoka tu mle washambulie adui zao. Ili ushinde unapaswa uandae mahandaki (siyo moja) na ambayo ni kama vile wanamaombi, vikundi na ministries mbalimbali kanisani. Hata hivyo, maji ya mafuriko haya yatakuja kutoka chini kuelekea juu kinyume na kanuni  za dunia hii. Walio kwenye handaki wanakuwa na nia moja ya ushindi.
2.      MFALME WA MOABU
Huyu mfalme waMoabu pia aliwahi kutoa kafara ya watawala ili aendelee kudumu madarakani. Imeandikwa katika 2WAFALME 3:21-27…[Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi, wakasimama mpakani. 22 Wakaamka asubuhi na mapema, na hilo jua likametameta juu ya maji, na Wamoabi wakayaona yale maji yaliyowaelekea kuwa ni mekundu kama damu. 23 Wakasema, Ndiyo damu hii; bila shaka hao wafalme wameharibika, wamepigana kila mtu na mwenziwe; basi sasa, enyi Wamoabi, nyara hizo! 24 Hata walipokuja matuoni kwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapigapiga Wamoabi hata kwao. 25 Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri; mpaka katika Kirharesethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo wakauzunguka wakaupiga. 26 Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27 Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.]…Ilikuweppo hasira kuu juu ya Israeli baada ya mwana wa kwanza wa mfalme wa Moabu kutolewakafara ukutani. Mashetani yalipandwa na hasira baada ya kupokea damu hii. 
 
MADHARA YA  KAFARA ZITOLEWAZO
1.      Mungu kutozisikia sauti za watu wanapoomba.
Imeandikwa katika MIKA 3:1-4…[Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu? 2 Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. 3 Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani.4 Ndipo watakapomwomba Bwana, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao.]… Watawala wanapoomba, Mungu hazisikii  sauti  zao. Endapo haki haitendeki, Mungu atauficha uso wake  kwako. Kafara zinazotolewa kwa mungu asiye Mungu muumba mbingu na nchi,
2.      Kiongozi anayekuwakilisha wewe ana uhusiano  mkubwa na hatima yako  na kila kitu ulicho nacho. Mkumbuke Ayubu jinsi ambavyo watoto na familia  yake, mali zake, na mifugo  yake vilivyolindwa na Bwana. Maana yake ni  kuwa, hatima ya vyote itategemeana na mahusiano yaliyopo kati ya kiongozi wako  na Mungu.
3.      Kiongozi anayetoa kafara kwa mashetani, anawaunganisha watu na mashetani.
Imeandikwa katika 1KORINTHO 10:20-21…[Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.]…. Mungu  tunayemtumikia hapokei kafara za wanyama au za wanadamu. Kwenye familia au taifa, jambo likitokea na ukamuona mmojawapo wa watu anachukua wanyama kuchinja ujue mtu huyo anataka kuwaunganisha ninyi na madhabahu za kuzimu.
Imeandikwa katika WAEBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.]… Yesu ni mjumbe wa Agano Jipya. Damu ya Yesu inanena mema, lakini pia zipo damu  zinazonena mabaya. Leo tutaomba kwa ajili ya taifa letu, ili kama zipo damu zilizomwagwa kwa ajili ya kuharibu maisha ya watanzania, tuzikatae kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Kuanzia leo, na kuanzia sasa, ewe kuhani, ewe mtawala uliyemwaga damu mahali popote ili unitawale, leo nakukataa kwa Jina la Yesu. Kila nguvu ya utawala wako ulizowekeza ili kunitawala leo najitoa kwenye utawala wako, naitoa na familia yangu na taifa langu kwenye kafara zako kwa Damu ya Yesu. Amen.

Kumbuka damu zinapomwagwa hupindisha hatima za watu. Yamkini ni damu za watu au wanyama zilizomwagwa ili kukuvuta nyuma usisonge mbele. Leo tuikate mikono  yote ya mashetani inayokuvuta urudi  nyuma kwa Damu ya Mwanakondoo Yesu Kristo.
Kama ilivyokuwa kwa Zakaria, baba wa Yohana Mbatizaji aliyebisha sana kuhusu kuzaliwa kwa Yohana na kisha badala yake akaupata ububu, vivyo hivyo kiongozi au mtu  yeyote Tanzania anayetaka kutoa  matamko ya kuhatarisha amani na uchaguzi mkuu mwaka huu, kuanzia wiki hii kinywa chake kitiwe ububu kama kile kinywa cha Zakaria kwa Jina la  Yesu. Amen. Wapo wanadamu pia wanaotamka maneno mabaya juu ya maisha yako.  Wiki  hii  ni wiki ya kufunga midomo.
Ikiwa upo katikati yetu na hujamwamini Yesu, haya yote tunayoenda kuyaomba siku hii kingyume na kafara za watawala hayatakusaidia. Yesu akija kwako anakupa uzima tena wa milele.

Comments