KESHO ILIYOPIGA KONA

NA ASKOFU MKUU Dr JOSEPHAT GWAJIMA, UFUFUO NA UZIMA.
Mungu alipokuumba ameiweka kesho yako kabla hujazaliwa, ameona mkeo mumeo kabla huja zaliwa ameona kazi yako kabla hujaiona. Kila alichokiumba Mungu ni kikamilifu ndiomaana anaitwa wa kwanza na wa mwisho ambapo maana yake ni mianzo yote ilimkuta na miisho yote itamuacha. Kwa kawaida kuna namna fulani inaweza ikatokea na kesho yako ambayo Mungu amekupa ikapiga kona, kwa mfano unaweza ukawa umepewa kesho yako uwe rubani wa ndege na mbinguni wanakuona na kujua kuwa wewe ni rubani lakini ikatokea namna fulani ukaja ukaishia kuwa mwendesha bodaboda. Inawezekana unajishangaa ndoto yako ilikuwa uwe Mkurugenzi fulani au Mbunge au Waziri lakini leo hii upo ni mfanyakazi wa ndani au ni mama lishe au ni muuza magazeti na hata hujui utatokaje hapo ulipo ili uifikie ndoto yako. Hiyo ndio maana ya kesho iliyopiga kona.
Maisha ni kile ambacho Mungu amekipanga uje uwe na haijalishi watu wanasemaje au wanafanyaje kuhusu wewe.
“Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?”
Matendo ya Mitume 13:6

Wachawi wamejaa hila ni wajanja sana, hujifanyia ndugu ili wawatende mabaya na hula nyama za watu na kunywa damu zao ili wajiimarishe, ni waovu kwenye kila eneo la Maisha ya watu, ni wana wa ibilisi ni waongo kama baba yao, ni adui wa haki yote na hawaachi kuipotoa ndoa ya mtu iliyo nyooka, wachawi hawaachi kuipotoa biashara ya mtu iliyo nyooka, hawaachi kuzipindisha njia za maisha ya mtu zilizo nyooka, pia hawaachi kulipindisha Taifa lililonyooka. Wachawi ndio wakala wa shetani wa kupindisha maisha ya mtu yaliyonyooka.
“Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.”
1Yohana 3:10

“Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.”
Yohana 8:44

“Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano”
Luka 22:31

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wawe waangalifu sababu shetani atawapepeta kama ngano. Wachawi huona kile ambacho utakifanya miaka ijayo na wakakipindisha lakini Mungu anao uwezo wa kukirudisha hata kama inaonekana kibinadamu ikashindikana.
“Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
“Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
Wachawi wanaweza kumtupa mtu gerezani. Kwa mfano unaweza kumwoma mtu anaimba lakini yupo gerezani au mtu anaweza akawa anafanya kazi fulani lakini yupo gerezani. Maana yake wachawi wanakuwa wamemtengenezea mtu aishi kwenye mfumo fulani wa Maisha kwamba:- aamke asubuhi, anywe chai aende kazini na jioni arudi na daladala nyumbani aje alale kila siku kazi ni ileile, mshahara ni uleule, hakuna mabadiliko kwenye maisha mtu kama huyu anakuwa yupo gerezani na lazima gereza hilo livunjike kwa jina la Yesu.
Kwenye ulimwengu wa Roho yapo magereza ambayo yamefunga familia mfano wasisome mpaka chuo kikuu, wasisafiri, wasipate maisha bora bali wakae vilevile kama walivyo.
Kuna watu wengine hawataki kabisa kuolewa. Hii hutokana na.
1. Aliwahi kuolewa ,na mume wake akamtendea mambo ya ajabu, hivyo ndani ya akili yake ikampelekea kuwachukia wanaume wote.
2. Wazazi wake walikuwa wana mgogoro hivyo alipofikia umri wa kuolewa haoni ndoa kama ni jambo zuri.
3. Inawezekana kwenye familia yao kuna mashetani ya kuwazuia kuolewa. mashetani haya ni ya kiume na yanakuwa yameshafunga naye ndoa katika ulimwengu wa roho pasipo yeye kujua. Kama sheria ya ndoa inavyosema kwamba mwanamke akiolewa hawezi kuwa na mume mwingine,mapepo haya yanakuwa yanamwingilia kimwili wakati wa usiku,kwa sababu hiyo anakuwa hapendi kuolewa. na hata kama anafanya biashara yanakuwa hayamwachii kusafiri kibiashara sababu anaweza kwenda na kukutana na mwanaume akawa mumewe. Jini huyu anakaa ndani yake na usiku hutoka nje na kumuingilia kimwili.
4. Mtu huyu huwa ana matatizo ya kuzaa sababu anakuwa amekwisha zaa sana rohoni watoto wa kichawi. Lengo lao ni kuwa na uzao wa kushetani duniani.

Ukiri: “ninakataa kuzaa watoto wa kichawi kwa jina la Yesu mume wa kiroho au mke wa kiroho ninamteketeza kwa jina la Yesu”
Mtu ambaye ana mume wa kiroho ukifika wakati wa siku zake huumia sana au hazioni kwa sababu chakula chao hawa ni damu, hufanya haya yote ili kuipindisha kesho yake lakini Bwana Yesu ametupa njia ya kutokea na kurudisha kesho iliyopiga kona na misiba yote Imekwisha kwa jina la Yesu.
Kuna majini ya kike ambayo huipindisha kesho ya mtu, asili yao ni ya kiarabu na hufanya mahusihano ya kimwili na wanaume sababu ya kuwa na watoto wa kijini.
Ukiri.
“Kwa jina la Yesu kuanzia sasa Mke/Mume wa ndotoni nakupa talaka kwa jina la Yesu, muda mrefu nimekuwa vile ambavyo Mungu hajataka niwe na leo ninakataa kubaki hivi hivi kwa jina la Yesu”
Mungu si mwanadamu hata aseme uongo, Maisha yako yapo pale pale, Mungu ni Mungu wa huruma hata kama ukienda chini ya bahari ataunyoosha mkono wake na kukuokoa kama alivyomuokoa Yona”
Maombi:
Baba Mungu katika jina la Yesu kristo, kwa damu ya Mwana kondoo, ninainyoosha kesho yangu iliyopiga kona kwa jina la Yesu, nanyoosha kesho yangu kwenye Biashara kwa jina la Yesu, nanyoosha kesho yangu iliyopiga kona kwenye ndoa kwa Jina la Yesu, nanyoosha kesho yangu kwa damu ya Yesu Amen. (endelea kushindana kwa damu ya Yesu)
Kukata tamaa sio kutatua tatizo, mfano mzuri Musa alizuiliwa lakini baadaye alipenya, Yusufu alizuiliwa ndoto yake isitimie lakini baadaye alipenya, Yesu alizuiliwa lakini baadaye alipenya.
Ukiri:
“Kwa jina la Yesu shetani yeyote aliye nje yangu au ndani yangu ambaye amejipanga kunizuia ninaamuru kuanzia sasa achia kesho yangu kwa jina la Yesu.”
Kuna wakati shetani anakaa kwenye macho yako anakudanganya kwamba matatizo uliyo nayo ni ya kawaida kumbe ni yeye ndiye anayesababisha, pia hukaa kwenye mawazo yako ya akili na kila unachokiwaza kinatokana na yeye, shetani huwatumia wale watu wanaokuzunguka ili wakukwamishe mahitaji yako ili usikende kwenye kesho yako.
“Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.”
1wathesalonike2:18

“Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.” Zakaria 3:1
Ukiri:
“Katika jina la Yesu shetani yeyote anayefuata Ndoa, Bishara, Elimu, kazi yangu kutokana na maagano yaliyofanywa kijijini ninavunjilia mbali maagano yote kwa jina la Yesu. Navunja mazindiko na maagano ya familia yangu kwa jina la Yesu, maagano ya kifo, laana yaliyofanywa na wazazi wangu na babu zangu ninayavunja kwa jina la Yesu.”
Jina la Yesu halina mbinu mpya au za zamani bali jina la Yesu linaweza kutenda kazi hata wakati wa mawimbi.
Chochote kinachoanzia mwilini ni cha muda mfupi sana bali kila kinachoanzia Rohoni ni cha kudumu na hata kama mtu akikunyang’anya hautachukua muda lazima utakipata.
Mungu ana njia zake kumpa mtu kitu japo mwanadamu anawaza kwa akili zake mwenyewe atapata kitu kwa njia zake mfano ukiitwa kwenye usahili wa nafasi fulani ya kazi na ukakuta watu ni wengi na nafasi iliyotangazwa ni moja tu,kama ni saa yako lazima utaipata,hata kama wengine wana sifa kubwa kuliko wewe. Hii ni kutokana na maombi uliyoyofanya na kukufanya uipate kazi hiyo kuanzia Rohoni. .

Comments