KIAPO CHA KICHAWI



NA ASKOFU MKUU Dr JOSEPHAT GWAJIMA, UFUFUO NA UZIMA.



Mambo ya Walawi 5:4-
“Au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo”

Kuapa kunaweza kuwa kuapa kwa kutenda uovu au kutenda jambo jema. Biblia inaongozwa kwa kiapo cha Mungu kwa wanadamu kuna mambo mengine Mungu anawafanyia watu kwasababu aliwaapia watu hivyo hawezi kuacha kutokuyafanya.
Kwenye nguvu ya kiapo mtu unaweza kuapa jambo zuri ili ulifanye. Wana wa Israeli walipokuwa wanaodoka Misri walifika katika mto Yordan

Yoshua 9:1-
“Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo; ndipo walipojikutanisha pamoja wenyewe kwa wenyewe, ili kupigana na Yoshua, na hao Israeli, kwa nia moja. Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai, wao wakatenda kwa hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyoraruka-raruka, na kutiwa viraka; na viatu vilivyotoboka na kushonwa-shonwa katika miguu yao, na mavao makuukuu waliyokuwa wanavaa; tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa umekauka na kuingia koga. Nao wakamwendea Yoshua hata maragoni huko Gilgali, nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi. Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mwakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi? Nao wakamwambia Yoshua, Sisi tu watumishi wako. Yoshua akawauliza, Ninyi ni nani? Nanyi mwatoka wapi? Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la Bwana, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri, na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi. Kisha wazee wetu, na wenyeji wote wa nchi yetu, walinena nasi na kutuambia, Chukueni vyakula mkononi mwenu kwa ajili ya safari, mwende mkawalaki watu hao, na kuwaambia, Sisi tu watumishi wenu; basi sasa fanyeni agano nasi. Huu mkate wetu tuliutwaa ukali moto katika nyumba zetu, siku hiyo tuliyotoka kuja kwenu, uwe chakula chetu; lakini sasa, tazama, umekauka, na kuingia koga; na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa ni vipya; sasa, tazama, vimeraruka-raruka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana. Basi hao watu wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa Bwana. Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia. Kisha ikawa, mwisho wa siku ya tatu baada ya kufanya hilo agano nao, walisikia habari ya kuwa watu hao ni jirani zao, na ya kwamba waliketi kati yao. Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikilia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu. Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu. Lakini wakuu wote waliwaambia mkutano wote, Sisi tumewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli; basi sasa hatuwezi kuwagusa watu hawa. Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho kiapo tulichowaapia. Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia. Basi Yoshua akawaita, akanena nao, na kuwaambia, Mbona ninyi mmetudanganya, huku mkisema, Sisi tu mbali sana na ninyi; nanyi kumbe! Mwakaa kati yetu? Basi sasa mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu. Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo Bwana, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili. Basi sasa, tazama, sisi tu mkononi mwako; basi kama uonavyo kuwa ni vyema na haki kwako wewe kututenda, tutende vivyo. Naye akawafanyia hivyo, na kuwaokoa na mkono wa wana wa Israeli, ili wasiwaue. Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.”

Wana wa Israeli wametoka katika nchi ya Misri kwenda katika nchi ya ahadi na walipovuka mto Yordani walijiliwa na watu waliovaa magunia na viatu vilivyo tobokatoboka vya zamani sana wakawaambia wana wa Israeli kwamba walivyoanza kuondoka mkate wao ulikuwa wamoto na viatu vyao na nguo zao zilikuwa mpya sana lakini ilikuwa si kweli walijifanya wanamjua Mungu wa Israeli amewatuma wana wa Israeli kuwauwa watu wote watakaokutana nao ili wamiliki mahali pao. Wale watu waliwaendea wana wa Israeli ili wapate kiapo kutoka kwao ili wasiuwawe. Mkutano wa Israeli ulikutana na wale watu mbele ya safari yao na kushindwa kuwauwa kwasababu walikwisha waapia hivyo Yoshua akawafanya kuwa wapasua kuni, wabeba maji na kufanya kazi za ndani kwa wana wa Israeli na Mungu wao.
Kuna wakati wana wa Israeli waliingia vitani wakaapa kwamba hatakula mtu wala kunywa mpaka washinde vita. Walipoingia porini wakakuta masega ya asali yanamwaga Asali lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejaribu kunyoosha mkono wake kushukua hiyo asali kwasababu ya nguvu ya ile asali. Mtoto wa mfalme alikuwa hayupo wakati wa kiapo kile lakini yeye alikula. Kiapo kinaweza kumfunga mtu akiona jambo zuri lakini asiliguse. Mtoto wa Mfalme Yonathan alihukumiwa kuuwawa japo hakuwepo wakati kiapo kilivyokuwa kikitolewa.

1Samweli 14:26-
“Na hapo watu walipokwisha kuingia mwituni, tazama, hiyo asali ilikuwa ikidondoka; walakini hakuna mtu hata mmoja aliyetia mkono wake kinywani; kwa sababu hao watu walikuwa wakikiogopa kile kiapo. Ila Yonathani hakusikia, hapo babaye alipowaagiza watu kwa kiapo; basi yeye akainyosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake, na kuichovya katika sega la asali, kisha akatia mkono wake kinywani; na macho yake yakatiwa nuru.”

Mathayo 5:33-
“Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako”

Yakobo 5:12
“Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.”

Kwenye agano la kale watu walikuwa wanaapa na kuangukia katika matatizo.
Yeremia 11:1-
“Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Yasikieni maneno ya maagano haya; ukaseme na watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; ukawaambie, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya, niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu; ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi ijaayo maziwa na asali, kama ilivyo leo hivi. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee Bwana.”

Moja wapo ya Sababu ambayo Mungu aliwapa nchi ya ahadi wana wa Israeli ni kwasababu aliwaapia baba zao japo walikuwa wakimuudhi njiani lakini aliwaongoza mpaka wakaifikia.
Ezekieli 16:59
“Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitakutenda vile vile kama ulivyotenda, uliyekidharau kiapo kwa kulivunja agano."

Kuna wakati Mungu alimwambia Musa ajitenge na wana wa Israeli ili awauwe wote lakini Musa alimkumbusha kiapo alichowaapia Baba zao na kuna wakati watu walikuwa wakitenda maovu lakini aliwavumilia mpaka akawafikisha kwenye Nchi ya ahadi.
Isaya 45:23
“Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa”

Mwanzo 22:16
“Akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee”

Zaburi 119:109
“Nimeapa nami nitaifikiliza, Kuzishika hukumu za haki yako.”

Isaya 54:9
“Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.”

Yeremia 44:16
“Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema, Neno lile ulilotuambia kwa jina la Bwana, sisi hatutakusikiliza. Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.”

Shetani naye ni mungu wa dunia hii na yeye ana majeshi yake ambayo ni mapepo majini, miungu n.k.
Matendo ya mitume 23:12-14
“Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo. Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu arobaini. Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo.”

Hakuna uharibifu unaompata mtu bila kikao cha uharibifu iwe ni kwenye kazi, ndoa, safari, biashara.
Biblia inasema makuhani walikaa kikao ili wamuuwe Paulo. Watu Zaidi ya arobaini wameapa kwaajili ya kumwangamiza mtu mmoja.
Shetani hajaumba kitu chochote hutumia kile alichokiumba Mungu na kukitumia kwa maslahi yake binafsi. Wachawi wamejifunga kwa kiapo ili mtu fulani asishinde, asiolewe, asisafiri, asifanikiwe kwenye jambo Fulani japo dalili zote zinaonyesha mtu Fulani anakaribia kushinda lakini kuna watu wamekaa na kuwaendea wazee kuwaambia wamekaa na hawata kula wala kunywa mpaka ashindwe, biashara yake iharibike, asiolewe.
Bwana naye ameapa na kusema hatakuacha wala hatakupungukia kabisa, Mungu ameapa na kusema kwa kupiga kwake sisi tumeponywa na Mabaya hayatatupata sisi wala tauni haitakaribia hemani mwetu.

Watu wengi wanaapa ili Fulani asijenge, asizae, asioe au asiolewe na viapo hivi hufanywa wakati wa usiku au mchana na wengine huapa kwa maneno raihisi tu kwamba “tuone kama utafanikiwa” wengine wanaapa bila kula au kunywa mpaka viapo vyao vitokee, wengine wameapa kule kijijini kwamba kwenye nyumba yenu hakuna atakayefanikiwa lakini sisi tunaye Mungu wa Yakobo ambaye ametoa ahadi zake kwetu kwa kiapo na zitatimia kwa jina la Yesu.
Matatizo yako hayapo mjini au kwenye wizara fulani bali ipo kule kijijini kule wale wazee wa kule wamewahi kuapa kwaajili ya ukoo wenu kwamba kwenye familia yenu asitoke mbunge au waziri au mtu atakaye safari nje ya nchi au mtu atakayefika chuo kikuu, waliapa kwenye njia panda au kwenye visima visivyokauka na ile tarehe yao roho mtakatifu aliiona tunaifua na kukivunja kile kiapo kwa jina Yesu.
Vita sio vyetu vita ni vya Bwana na Mungu wa mbinguni ameapa kwa nafsi yake hatamdanganya Yakobo atamwambia yaliyo kweli. Unapokuwa na Yesu hauzuiliki
Tumeona Yonathan alikula asali japo hakuwepo wakati wa kiapo.
“Katika jina la Yesu leo kwa jina la Bwana wa majeshi ninavunja kiapo cha ukoo familia ndoa kazi biashara walicho hapa kwamba mimi sitafanikiwa ninavunja kiapo kwa jina la Yesu ninasafiri kwenda kwenye kijiji nilipozaliwa ilipo familia yangu ninavunja kiapo cha kila aliyeapa kwamba mimi sitafanikiwa ninakivunja kiapo hicho kwa jina la Yesu’

“Kwa jina la Yesu ninakataa kuharibikiwa sawasawa na kikao chao kwa jina la Yesu, kiapo cha wazee wa kijiji, kiapo cha wazazi, kiapo cha wachawi ninakivunja kwa jina la Yesu”
Mungu ametuonyesha mambo mengi yanaendelea kwasababu ya viapo. Kuna mtu alimwendea Yesu ili amponye mgonjwa wake lakini Yesu alimwambia nenda nitakuja lakini mtu yule alimwomba Yesu aseme neno tu mgonjwa wake apone ndipo Yesu akamwambia apone sawasawa na Imani yake, yule mtu aliporudi alimkuta ameshapona na alipouliza amepona muda gani wakamwambia muda ambao Yesu alikuwa na naye.
Maana yake Neno moja linaweza kumponya mtu na akafunguka kabisa kutoka kwenye kiapo chake.

Kuna baadhi ya familia nyumba zina na watoto wenye mama tofauti yaani Baba anakuwa anawake wengi na inatokea kwenye nyumba moja watoto wa nyumba ile wanafanikiwa sana kuliko wengine. Kinachokuw kimetokea ni kwamba wanakuwa wamewafunga wenzao kwa viapo mfano asipatikane mtu wa kuwaoa au kuolewa nao, asipatikane mtu wa kusoma mpaka chuo kikuu au kusafiri. Viapo hivyo vyote vinaondoka kwa Damu ya mwakondoo Yesu kristo.
Mungu alimpa Ibrahimu ahadi alipokuwa ana umri wa miaka sabini na mitano na ahadi yake ikatimia Sara akiwa na miaka 90. Usiwe na wasiwasi kwamba ndoto yako haitatimia bali unatakiwa ujue kazi ndio kwanza imeanza na ndoto yako itafanikiwa kwa jina ya Yesu.
Mungu alikuwa ameshaapa atawatoa wana wa Israeli na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi, Yesu aliapa msalabani kwamba Imekwisha,
Ufufuo na uzima

Comments