KUNG’OA MIPAKA ULIYOWEKEWA NA WACHAWI



Na Mchungaji Kiongozi Paul Joshua, Ufufuo na uzima Kigoma.
YOSHUA 1:1-4 “Ikawa baada ya kufa kwake Musa mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni mtumishi wa Musa akasema Musa mtumishi wangu amekufa haya basi ondoka vuka mto huu wa Yodani wewe na watu hawa wote mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. Kila mahali zitakapokanyaga nyayo za miguu yenu nimewapa ninyi kama nilivyomwapia Musa. Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni mpaka mto ule mkubwa mto wa Frati nchi yote ya wahiti tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua hapo ndipo patakuwa mpaka wenu”.
Tunamuona Mungu anawaambia wana wa Israeli habari ya mipaka katika maeneo, kumbe kuna mipaka ambayo mtu anaweza akawekewa. Mungu anaweza kumuwekea mtu mpaka wa namna Fulani wa mafanikio yake lakini na shetani naye anaweza kumuwekea mtu mpaka katika maisha yake ili asifanikiwe kuzifika Baraka zake ambazo Mungu amempangia. Yoshua alipoambiwa avuke na wana wa Israeli mbele yake kulikuwa na mpaka wa kuwazuia wasivuke akangalia mbele haononi pa kupitia maana kulikuwa kuna kizuizi cha bahari ya shamu, Bahari ya shamu ilikuwa ni mpaka ambao ungewazuia wana wa Israeli kuvuka lakini Bwana akawapigania Yoshua akavuka na watu wote katika bahari ya Shamu.
Mipaka ni eneo lako la kumiliki na kila mtu ana kitu ambacho Mungu amemwekea mpaka wake wa kumiliki, na kazi ya shetani ni kupunguza eneo lako la kumiliki yaani kiwango chako cha kumiliki mafanikio kinapungua ni kweli unapata lakini unachokipata sio kiwango chako ambacho Mungu amekupangia.
Wachawi wanaweza kumzuia mtu asiende au wanaweza kuzuia kanisa lisisonge mbele maana wanaweka vikwazo vya rohoni ambavyo vinamfanya mtu asisonge mbele
ISAYA 57:14 “Naye atasema tutieni tutieni itengenezeni njia kiondoeni kila kikwazacho katika njia ya watu wangu”.
BWANA anasema kipitia kinywa cha nabii isaya kwamba tukiondoe kila kitu ambacho kinakwaza na sisi leo tunakwenda kuviondoe vikwazo vyote ambavyo shetani ametuwekea. Kila tukio lolote ambalo linatokea kwako liwe zuri au baya linaanzia rohoni ndipo linakuja kwenye ulimwengu wa mwili, maana wachawi wanao uwezo wa kutengeneza tukio lolote na kumuwekea mtu
1WATHESOLONIKE 2:18 “Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam mimi Paulo mara ya kwanza, na mara ya pili na shetani akanizuia”.
Kumbe shetani anaweza kuwazuia watu wasipite, wachawi wanaweza kumzuia mtu asiende mbele yawezekana umehangaika sana katika shida yako au umetumia fedha nyingi ili uvuke katika shida yako lakini imeshindikana maana kuna watu ambao wanazuia. Kuna uwezekano wa roho hata masomo yako yakadhuiliwa au mshahara wako ukadhuiliwa, tumezoea kusema ni mpango wa Mungu wala si mpango wa Mungu ni mpango wa shetani. Familia ya mtu inaweza ikafungwa isifikie kiwango Fulani cha mafanikio, kila mafanikio ya mtu au kila hatua ya mtu kuna vita na raiti ingekuwa hakuna wachawi wala waganga wa kienyeji wewe usinge kuwa na maisha kama hayo uliyonayo. Unashangaa unasoma lakini ukifika form four unafeli hata kama una akili, kwenye hatu ngumu kwa mtu ni kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine ndio maana unaweza ukakuta wengine wanazeekea kwenye hatua moja na mchana wa leo tunakwenda kubomoa magereza yote ambayo watu wamefungiwa ili wasisonge mbele.
Familia mnaweza mkawekewa mpaka wa miaka wa kuishi yawezekana ikawa katika familia hatakiwi mtu kuvuka miaka hamsini unashanga mtu akifikisha miaka thelasini tu anakufa. Ni hatari sana kwenye familia kuwa kuna mchawi ama mganga wa kienyeji kwa sababu maisha unayoishi wewe na familia yako siyo ndo maisha ambayo Mungu alikupangia
HESABU 34:1 “Kisha BWANA akanena na Musa na kumwambia waagize wana wa Israeli uwaambie mtakapoingia nchi ya kanaani (hii ndiyo nchi itakayowaangukia kuwa urithi maana hiyo nchi ya kaanani kama mipaka yake ilivyo)
Shetani anaweza kukupunguzia ukubwa wa eneo ambalo Mungu amekupangia kumiliki ni kweli utasoma lakini sio kwa kiwango ambacho Mungu alikupangia ndio maana ni wachache ambao wamefanikiwa, ndio maana unatakiwa kukataa hatua uliyonayo usilidhike kwa kile unachokipata maana unatakiwa kupata zaidi ya hicho kwakuwa kuna kitu kinaweza kikawa ndani ya mwili wako au nje ya mwili wako hata adui anaweza akawa ndani ya mwili wako au nje ya mwili wako na ni hatari sana kama adui yako yupo ndani yako. Unaweza ukawa una mapepo ambayo ndio adui wako wanakuwa hawataki ufanikiwe katika maisha yako ama wanakuwa hawataki upate mtoto.
Furaha yako ya mwilini isikudanye maana una vita katika ulimwengu wa roho kuna uchawi ulifanywa kwa muda mrefu kwamba wewe mama kila mtoto utakayemzaa asikusaidie kuna sehemu ambayo kuna sehemu ambayo kumewekwa ukuta ili mtu asifanikiwe kuna walinzi hawataki uvuke unakuwa ni mpaka umewekwa katika maisha ya mtu.
Kila mtu kuna boksi lake la maisha ambalo Mungu alimkabidhi na wengine hawana leo yawezekana wamenyang’anya na wengine wana nusu na wengine wameshafanikiwa. Ukishindwa kumiliki duniani ndo imepita usidhani utakwenda kumiliki mbinguni maana mbinguni hakuna gari wala bajaji cha kufanya ni kupambana hapa hapa duniani kuvitoa vitu rohoni na kuvileta katika ulimwengu wa mwili kumtoa mchumba wako rohoni na kumleta katika ulimwengu wa mwili.
Wachawi wanaweza kuona maisha ya mtu tangu akiwa tumboni kwa mama yako bado hajazaliwa na wakajua huyu mtu baadae atakujakuwa nabii au mchungaji ndio maana hujaanza kulogwa leo vita yako ilianzia tumboni mwako ukiwa bado hujazaliwa. Kuna watu wamekatizwa miaka yao ya kuishi mtu anakuwa amepangiwa kuishi miaka mia lakini anaishi miaka arobaini maana amewekewa ukuta wa mauti na wachawi ili asiishi miaka mingi.
Piga picha katika familia yenu ni kwanini maisha yenu yanafanana hakuna hata mmoja aliyefanikiwa, lazima utambue kuna kitu ambacho kimewekwa ili msivuke katika maisha kila unapotaka kuvuka shida zinaanza magonjwa unaanza.
Kila jaribu unalopitia katika maisha yako lina mlango wake wa kutokea lakini itategemeana na kiwango cha mtu cha kumtafuta Mungu ndio maana ukifika hatua unaona umekwama mwambie Mungu akuonyeshe njia utoke kwenye shida uliyonayo Mungu anategemea kuona kiwango chako cha kumtii.
Kama mtu umelogwa ama umefugwa hata kama ukiwa na kazi nzuri huwezi kuvuka ni lazima uanze kuivunja mipaka yote ya kishetani.
KUTOKA 14:10-12 “Hata Farao alipokaribia wana wa Israeli wakainua macho yao na tazama wamisri wanakuja nyuma yao wakaogopa sana wana Israeli wakamlilia BWANA. Wakasema Musa je ni kwa sababu hapakuwa na makaburi katika misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya kututoa katika nchi ya misri? Neno hilo silo tulilokuambia huko misri tukisema tuache tuwatumikie wamisri maana ni afadhali kuwatumikia wamisri kuliko kufa jangwani”.
Ukiona unafika sehemu unapitia sana magumu elewa kwamba unakaribia kwenye mafanikio yako, jaribu kuangalia umepitia mambo mangapi katika maisha yako ambayo ni magumu lakini Mungu amekusaidia na angalia jaribu lako ambalo liko mbele yako haijalishi watu wengine wanasema nini juu yako.
Kile ambacho hukiwezi Mungu anakiweza pale ambapo umewaza unaona umekosa jibu umepambana na umeshindwa unaona umeaibika mbele za watu hapo ndipo Mungu anainuka kukusaidia. Kwanini Mungu anasubilia umeshidwa ndipo anakuja kukusaidia anasubiri hadi watu waanze kukusema umeshidwa Mungu anasubiri adui zako waanze kusema wameshamaliza huwezikufanikiwa tena pale ambapo wanasema tuone kama atavuka ndipo Mungu anakuja tunajifunza hata kwa Daniel, Meshack, na Abedinego walipokamatwa hadi wanatupwa kwanye tanuru la moto na Mungu akaenda kuwaokoa kwenye moto je ni kwanini hakwenda kuwaokoa mwanzoni Mungu anasubiri watu waanze kusema hawezi tena.
Pale ambapo unaona umekosa jibu Mungu yuko pamoja na wewe usiangalie kuna shida gani imekuzunguka mwangalie Yesu usiangalie wanadamu wanasema nini juu ya maisha yako mwangalie Mungu anakwenda kukupigania. Leo uangalie msaraba mtazame BWANA Yesu umewaangalia wanadamu vyakutosha leo inua macho yako mtazame Yesu utapona. Unapoamua kupambana katika masha yako simama mwenyewe jifunze kusimama kama wewe hata katika wokovu simama kama wewe usisubilie wenzio wakupitie kwenda kanisani usikae unasema mbona Fulani haombagi ama huwa hafungi.
Ungejenga wokovu wako kwa kumuangalia mtu utaanguka chini, ukijenga wokovu wako kwa kikundi Fulani utaanguka chini ukiwategemea watu wakutie moyo siku moja utakakuja kushangaa. Jifunze kumsikiliza Mungu kuhusu maisha yako usiwasikilize sana wanadamu amua kusonga mbele ukimtegemea Mungu. Kuna shehemu umeshindwa kuvuka yawezekana umeomba sana lakini shida yako haijaondoka, ukuta na mipaka ambayo imewekwa juu ya maisha yako bado inakuzuia wewe mwenyewe unafahamu ni eneo gani ambalo umeshindwa kuvuka yawezekana wanao wanashidwa kusoma shule huo ni mpaka ambao umewekwa.

Kwenye familia kuna namna mbili za mzaliwa wa kwanza, wa kwanza kuzaliwa katika familia huwa anakuwa ni lango la familia anakuwa lango la wengine kufanikiwa na anakuwa ni rahisi sana kupokea mambo mabaya katika familia au mambo mazuri. Pia kuna mzaliwa wa kwanza wa rohoni unakuwa ni lango unaweza ukasababisha familia Yesu wote wakaokoka haijalishi ni wapili au watatu wewe unakuwa ndiye mzaliwa wa kwanza katika wokovu.

Comments