KWA SABABU YA ELIMU YAKE NDOGO NATAKA KUMWACHA.


 BWANA YESU asifiwe.
Nilimshauri rafiki yangu mmoja jambo hili ambalo nataka na wewe ujifunze kitu.

Rafiki yangu aliniandikia hivi akiomba ushauri.
 
Bwana Yesu asifiwe!
Nimesoma ujumbe wako wa :MAMBO KUMI YANAYO WEZA KUCHELEWESHA WACHUMBA KUFUNGA NDOA, asante mtu wa MUNGU kwa ujumbe mzuri, Mungu akubariki sana... Ila nilikuwa na maswali yanayo endana na ujumbe wako kwa sehemu.

1.mimi ni mwanafunzi wa degree chuo kikuu, Nina mchumba wangu ambaye tumekuwa naye kwenye uchumba sio kwa muda mrefu, ni kama miezi Kazaa hivi, binti huyo ameokoka na anamsimamo mzuri wa wokovu pia ana nipenda na mimi na mpenda pia, Changamoto ipo hapa yeye kiwango chake cha elimu ni form four pia alifeli hata cheti hana cha hiyo form four, kwa kadri siku zinavyo kwenda nahisi uzito kuendelea naye katika uchumba na mpaka nimesha fikiria binafsi kuvunja uchumba lakini bado sijamwambia, nikifikilia kwa maisha ya sasa na mipango niliyonayo nahisi kama sitaweza kuifikia nikiwa nae, hivyo nimefikili kuwa na mchumba ambaye tunaendana katika level ya elimu....
Nahitaji ushauri wako katika hili,
NB:sijawahi kufanya nae suala lolote la zinaa, napia kwa sasa sina msichana yeyote ambaye nawaza awe mbadara wake...



Majibu yangu Peter Mabula yalikuwa ni haya;

Ubarikiwe ndugu yangu .
Biblia inasema mke mwema hutolewa na MUNGU.
Inaposema kwamba mke mwema hutoka kwa MUNGU hiyo humaanishwa kwamba sifa za kiroho na kimwili hupangwa na MUNGU.
Naona elimu ndio kikwazo cha uchumba wenu lakini kikwazo hicho sio cha kiMungu ila ni cha kibinadamu.
Huyo binti wakati mwingine anaweza kukufaa kuliko wenye PhD 7 kama tu ni MUNGU amekupa.
Elimu ni suala dogo kwa MUNGU.
Mnaweza mkafunga ndoa na akajiendeleza hata kufikia elimu uitakayo wewe ndugu yangu.
Sababu za kiroho ndizo muhimu sana kuliko sababu za kimwili.
Kuna watu walilikataa kusudi LA MUNGU na kuwasema vibaya waliowaacha lakini walijuta baadae.
Unaweza kumwacha ambaye hatakusaliti maisha yake yote lakini ukampata msomi ambaye ndani ya miaka 10 akaleta ukimwi kwenye ndoa.
Siyaombei kwako ila huo ni mfano tu na nimewahi kuona.

Kuna wakati matatizo huja lakini wakati huo tofauti ya mke kutoka kwa MUNGU na mke kutoka kwenye nafsi huonekana.
Mama mmoja baada ya miaka 4 kwenye ndoa mmewe alipata tatizo na kuondoka nguvu za kiume. Leo ni mwaka wa 23 kwenye ndoa na hajawahi kumsaliti mume wake. Huyo ndie mke mwema.
Binti mmoja baada ya mwaka mmoja ndani ya ndoa mmewe akapata tatizo LA nguvu za kiume lakini amemsaliti zaidi ya Mara 50. Huyo ndie mke wa vigezo vya kimwili na sio kiroho.
Ndugu yangu. Una Uhuru wa kuchagua umpendae lakini mtafute kwa sifa za rohoni na sio za kimwili. Elimu ni sifa za kimwili.

Naamini kuna kitu umejifunza.

Ubarikiwe na waweza ku-share popote maana utakuwa umehubiri Injili.

Comments