Kwanini uulinde moyo?



Na Mtumishi Charles Francis
Bwana YESU asifiwe..
Ujumbe wangu kwako siku ya leo hakikisha unalinda sana Moyo wako kuliko vyote!


Kwanini ulinde moyo?

1. Moyo wako ni benki ya Amani yako, amani ikiondoka huwezi kuwa na ibada kamili na ya kweli na MUNGU. Namaanisha hata maombi utafanya kwa kuigiza au kwa malalamiko! Ndiyo maana Mathayo 5;8 akasema "heri wenye moyo safi maana hao watamwona MUNGU", kwanini anasema watamwona MUNGU? kwa sababu wataomba katika kweli na YEYE atajibu...... oooooohhhhh haleluya!

2. Moyo wako ndiyo injini ya mwili wako, ukiruhusu kuumizwa moyo unaruhusu magonjwa mwilini. Hapa ndiyo unasikia mara presha, mara mawazo, mara mtu anapata stroke!

3. Moyoni mwako anatakiwa akae MUNGU na utatu Mtakatifu, sasa chuki, wivu wa kijinga, roho mbaya na matendo mabaya hayatakiwi moyoni mwako maana hayo ni matunda ya shetani.

4. Moyo ukiumizwa huwa na maamuzi mabaya siku zote.

5. Moyo ukiumizwa husababisha akili kufanya kazi "kinyume nyume" utashangaa mtu anakuwa na maauzi ya hasira, ya haraka, ya uharibifu, anawaza uchafu.. wewe ukiona hayo fahamu hapo Moyo umeumizwa!

6. Moyo ukiwa na furaha utamsifu MUNGU vizuri katika utakatifu wake. Yakobo 5:13. Pia Moyo ni "kipokeleo" (receiver) cha kile ufahamu wako unawaza, sasa kama unawaza vibaya moyo wako utajiandaa kupokea na kuruhusu mabaya.

7. Ni kupitia Moyo na kinywa tu, mtu hupata kuamini na kuokoka, moyo ukiumizwa wokovu huondoka na wokovu ukiondoka ibilisi anakumaliza, Warumi 10:9.

NB: Moyo ni injini ya mwili, hivyo MUNGU ameweka mafuta huko ndani ili injini itembeze mwili vizuri kufikia kusudi la safari, sasa kila unapokubali kuumizwa unafanya safari yako iwe na vituo vingi na mafuta yanatumika mengi kuliko kawaida na unachelewa kufika au unaweza usifike ulikotakiwa kufika. Ngoja utanielewa tu, kwa mfano nikuulize: Umeanza wokovu pamoja na watu wangapi na katika hao unalingana nao au wamekuzidi?
 Ukipata jibu TAFAKARI SANA na CHUKUA HATUA.
Bwana YESU akupe kuutunza na kuulinda MOYO WAKO, AMEN.

Mtumishi Charles Francis, 0752 20 20 52.

Comments