Mapenzi Ya Mungu Hayazuiliki.

Na Askofu Mkuu Dr. Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.”
1 YOHANA 5:14 – 15

“Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.” Mwanzo 37: 5-8
Yakobo aliyekuwa na wake wawili. Mke mkubwa aliitwa Lea ambaye alizaa naye watoto kumi na Mke mdogo aliyezaa naye watoto wawili. Yusufu alikuwa mtoto wa pili kutoka mwishoni aliota ndoto na kuamua kuwashirikisha ndugu zake.
“Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.” Mwanzo 31:24
Katika nyakati hizo Mungu alikuwa anawajia watu katika ndoto na kuzungumza nao. Yusufu aliambiwa na ndugu zake ameota ndoto anataka aje awashirikishe hivyo walifurahia sana kwasababu walijua Mungu ameongea naye kupitia ndoto. Wale ndugu zake waliamua kumsikiliza mdogo wao na walipomsikiliza wakafahamu maana halisi ya ndoto yake kuwa atakuja kuwatawala na hawakuamua kumwita Mchungaji au Nabii kuja kuwatafsiria maana ya ndoto ile hivyo wakaamua kumshughulikia ili ndoto yake isitimie.
“Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke.” Matendo 21:14
Cha kushangaza ndugu zake Yusufu wapoanza kumchukia Yusufu akaota ndoto nyingine.
Ndoto ya pili aliyoiota aliona na Baba yao mzazi na Mama yao mzazi na ndugu zake wanamwinamia yaani maana yake Jua mwezi na nyota kumi na mbili zinamwinamia ndoto ambayo ilifanya mpaka Baba yake akamkemea sababu ya ndoto hiyo aliyoiota. Ndugu zake wakamchukia lakini Baba yake akaiweka moyoni ile ndoto.
Juhudi za kuizima ndoto ya Yusufu isitimie zikaanza pale ndugu zake walipoenda kuchunga kondoo porini Baba yake akamtuma aende kuwapelekea ndugu zake chakula. Zamani watu walikuwa wakichunga mifugo mbali na makazi na kipindi malisho hayatoshi maeneo ya nyumbani vijana walikuwa wakienda mbali kuchunga kondoo muda mrefu bila kurudi nyumbani hivyo Yusufu aliwafuata ndugu zake huko “Dothan” kama alivyotumwa na Baba yake na wale ndugu zake wakamwona kwa mbali na kabla hajafika walishauriana wamuuwe ili ndoto yake isitimie. Wakapanga kumuuwa na kumtupa shimoni ili wakaseme mnyama mkali kamla.
“ndoto ya mtu haiwezi kuzuiliwa na shimoni au kitu chochote kile”
21. “Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Reubeni akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue.”

katikati ya uongo na uovu mulemule akawepo rubeni aliye mhurumia Yusufu ili asiuwawe. Ruben ni mmoja kati ya wale waliotaka kumuuwa Yusufu lakini alitoa ushauri kwa wenzake wasimuuwe bali wamtupe kwenye shimo.
Yusufu alitoka nyumbani kwake na ndoto yake akafika kwa ndugu zake wakamvua nguo zake na kumtupa kwenye shimo ambalo halina maji. Rubeni aliamua baadaye wamuuze ili aende mbali na wao wasije wakamuinamia na kumtukuza kama kiongozi wao.
23 “Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji.”

Walipomtupa shimoni waliamua kula chakula na kusheherekea. Yuda naye aliamua kutoa ushauri wasimuuwe ndugu wa damu yao bali wamuuze apotelee mbali ili ndoto yake isitimie.
Wamidiani walipita maeneo waliokuwa wakichungia kondoo na ndugu zake Yusufu waliamua kumuuza kwao mpaka Misri.
Yusufu aliingizwa shimoni na kuuzwa hadi Misri akaenda kule akiwa na ndoto yake. Alipofika kule alinunuliwa nyumbani kwa Waziri mkuu wa Misri aitwaye Potifa. Huku Israeli wale ndugu zake waliichukua ile nguo ya Yusufu na kuichana na kuipaka damu ya mnyama ili kumdanganya mzee Yakobo kwamba ndiyo matokeo halisi yaliyotokea kwa mtoto wake.

Yusufu aliponunuliwa kwa waziri mkuu akawa mchapakazi mwaminifu akakutana na tatizo la kusingiziwa kutaka kumbaka mke wa waziri mkuu aliyekuwa akimtumikia, Yusufu akapatwa na huzuni nyingine akiwa ndani ya nchi ambayo siyo yake na kuhukumiwa gerezani kifungo cha maisha jela huku akiwa bado ana ndoto yake.
Akiwa kule ndani ya gereza alikutana na watu waliohukumiwa kwa kesi za kuharibu chakula cha Mfalme na kuharibu kinywaji cha mfalme.
Yusufu akiwa ndani ya gereza alikaa miaka ya kutosha na wakati anaota ndoto ya kuja kuwa waziri mkuu alikuwa bado mdogo na ndoto yake ilitimia akiwa na miaka arobaini.
“Miaka haimzuii Mungu kutimiza ahadi yake, Mungu huwa anawaokoa watu dakika za mwisho”
Yusufu alitoa ufafanuzi wa ndoto kwa mnweshaji wa Mfalme kwamba atatoka na kupona kunyongwa lakini amkumbuke pale yatakapo tokea lakini Yule mnweshaji hakumkumbuka Yusufu baada ya ndoto yake kutimia. Mungu alimpa mfalme Farao ndoto ya masuke saba ya njaa na yalio shiba na kupitia ndoto hiyo Yule mnyweshaji alimwambia Mfalme kwamba kuna mtu gerezani ambaye alimfafanulia ndoto yake na ikatokea vilevile kama alivyomweleza na Mfalme akaamuru Yusufu aitwe kutoka gerezani hadi Ikulu kutafsiri ndoto ya Mfalme.
“Mwota ndoto, ndoto yake inaweza kumpeleka hadi Ikulu kutoa ushauri”
Mfalme alimwomba ushauri kijana aliyetoka gerezani ili atatue tatizo la nchi litakalokuja kutokea na kumfanya kuwa Waziri mkuu wanchi.
“Bwana huwainua wenye haki kutoka kwenye shimo na kuwafanya kuwa wakuu ili kuwaaibisha wenye nguvu”
Mungu huwaweka wale maaduia zako hai ili waje washuhudie muujiza wako baadaye wakiwa bado wako hai, kuna wakati mwingine tunawaombea mabaya maadui zetu ama wafe au wapatwe na mabaya lakini Mungu huwaweka hai ili baadaye waje washuhudie mafanikio yako na kuuona utukufu wa Mungu ndani yako.
Yusufu alikuwa hajazaa bado na alizaa mtoto wa kwanza akamwita Manase maana yake Mungu amenisahaulisha taabu zangu na akamzaa mtoto wa pili akamwita Efrahimu Mungu alipombariki katika nchi ya ugenini.
Yusufu alianza kukusanya chakula cha kutosha kwenye nchi ya Misri kwa kipindi cha miaka saba ya shibe. Ilipoanza miaka saba ya njaa, Israeli ilikumbwa na njaa ile.
Baba yake aliamua kuwatuma ndugu zake kwenda Misri sababu ilikuwa ndio sehemu pekee ya kupata chakula. Yusufu alipowaona aliingia ndani na kulia ndipo akarudi nje na kuwaauliza wapo wangapi wakamwambia wapo kumi na mbili lakini mdogo wao mdogo hayupo aliliwa na mnyama mkali, Yusufu aliingia ndani na kulia tena sababu bado walikuwa wakiendeleza uongo wao kisha akarudi nje na kuwahoji Baba yao anaitwa nani na Yule mdogo wao aliyeliwa na mnyama anaitwa nani wakamjibu na ndipo akawaambia atawapa nafaka. Yusufu aliweka kikombe cha waziri mkuu ndani ya gunia la mmoja wao mkubwa kisha akatuma majeshi kuwafuatilia na kuwakamata kwa kosa la kuiba kikombe cha waziri mkuu. Ndugu zake walikataa sababu walijua hawawezi kuiba na kusema atakayepatikana na kikombe na auwawe, askari waliwakagua na kukiona kikombe na ndipo wakamchukua mtu mmoja ndugu wa Yusufu abaki misri ili waende na kumleta Benjamini anayependwa sana na Baba yao Yakobo. Yusufu alipomuona akawaambia ndugu zake “mimi ndiye Yusufu aliyeliwa na mnyama mkali” Baada ya hayo yote kutokea Yusufu aliwageuka na kuwafunga mpaka Baba yao atakapofika. Baba yao alifika huko Misri na kuonana na mwanaye Yusufu ambapo walifurahi na kuanzia hapo wana wa Israeli wakatengewa mji ulioitwa Gosheni. Hivi ndivyo wana wa Israeli walivyoingia Misri na kukua huko kwasababu ya chakula.
“Ishi na watu vizuri kwasababu utawahitaji kesho”
“Katika jina la Yesu ninaamuru kila anaye aliyechelewesha ndoto yangu aishi ilia je kushuhudia na kuaibika” Amen.

Comments