MASWALI YA VIASHIRIA KWAMBA WEWE UNAKABILIWA NA HALI YA KUKINAI AU KUCHOKA KAZI (JOB BURNOUT)

Na Mchungaji Peter Mitimingi wa ya VHM.
Ujumbe huu ni kutoka katika Darasa la COUNSELING TRAINING!
1. Je unajiona kama una hali ya wasiwasi au kujiuliza uliza maswali ya kina mara kwa mara juu ya kazi au huduma unayoifanya?
2. Je unajihisi kama unajiburuza tu mwenyewe kwenda kazini au kwenye huduma na unapofika kazini unajisikia ugumu kuanza kazi mara moja? Yaani unajivutavuta sana ndio unaanza kazi?
3. Je huwa unajikuta unapatwa hasira na kukosa uvumilivu kwa wafanyakazi wenzako, washirika wako, watendakazi pamoja nawe au wateja wako?
4. Je huwa unajihisi kukosa nguvu mara kwa mara ya kufanya kazi kwa kiwango na uzalishaji bora?
5. Je unajihisi hali ya kutoridhishwa na mafanikio ya kazi yako?
6. Je unajihisi hali ya kuvunjika moyo kuhusu kazi yako?
7. Je, unatumia chakula, madawa ya kulevya au pombe kujisikia vizuri au kwa kifupi kuhisi?
8. Je unajisikia hali ya usingizi mara kwa mara unaona hali ya hamu ya kula inabadilika badilika mara kwa mara?
9. Je,unasumbuliwa na kuumwa kichwa mara kwa mara kusikoelezeka, maumivu ya mgongo au malalamiko ya maumivu mengine ya kimwili?

Kama wewe umejibu ndiyokwa maswali yoyote kati ya haya, unaweza kuwa unakabiliwa na kuchoka kazi (burnout). Kuwa na uhakika wakushauriana na daktari wako au mshauri wako. Hata hivyo, Baadhi ya dalili hizi pia zinaonyesha hali fulani ya tatizo la kiafya, kama vile tatizo la tezi (thyroid disorder) au tatizo la sonono (depression).


KUKINAI AU KUCHOKA KUFANYA KAZI FULANI
OCCUPATIONAL BURNOUT OR JOB BURNOUT
Marko 6:31- 32
31 Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. 32 Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu.

Kuchoka kufanya kazi (job burnout) ni aina ya matatizo ya kisaikolojia ambayo huwakuta watu katika kupoteza hamu na shauku ya kuendelea kufanya kazi au huduma kwa nguvu ile ya mwanzo.
Kuchoka kufanya kazi yaani (Occupational burnout or job burnout) ni hali ya mtu kujihisi uchovu unao anzia ndani ya moyo kuja nje ya mwili wake kuhusu hiyo kazi anayoifanya. Baadhi ya dalili za mtu ambaye amechoka kufanya kazi fulani yaani (job burnout) ni pamoja na:
• Ukosefu wa shauku ya kuendelea kufanya kazi (lack of enthusiasm)
• Kukosa motisha ya kuendelea na kazi, (lack of motivation)
• Kuwa na hisia za kutokufaa au kutofanya kazi vizuri (feelings of ineffectiveness)
• Pia wanaweza kuwa na mwelekeo wakuchanganyikiwa (dimension of frustration)
• Wasiwasi (cynicism).

Comments