MUNGU HATAKI TUWE UTAKATIFU WA SIKU MOJA BALI UTAKATIFU WA SIKU ZOTE.

Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
2 Tiomotheo 2:19 ''Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu.''
-Kila alitajaye jina la BWANA YESU na auche uovu.
-Kila alitajaye jina la JEHOVAH MUNGU wetu na auache uovu.
 Kila mkristo hulitaja jina la BWANA  lakini mpango wa MUNGU ni katika utakatifu.
MUNGU anataka utakatifu wa siku zote.
MUNGU Hataki Utakatifu Wa Siku Moja Tu Kwa Wiki. 
BWANA Hataki Tuwe Watakatifu Siku Tu Za Ibada.
 MUNGU Anataka Tuwe Watakatifu Siku Zote.

1 Petro 1:15-17 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.''

 Ndugu Yangu, Usikubali Kuwa Na Utakatifu Siku Za Weekend tu, Usiwe Na Utakatifu Wa Jumamosi Na Jumapili tu Maana Siku Hizo Utakuwa Kanisa. 
 Unyenyekevu Unaouonesha Kwenye Ibada Jumapili Hakikisha Unyenyekevu Huo Huo Unauonyesha Nyumbani Na Kazini katika siku za kawaida.

Warumi 6:22-23 ''Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA  wetu.'' 

Usikubali Kumtii BWANA YESU Kanisani tu kisha  Ukitoka Kanisani Utakatifu Wote Unauacha Kwenye Viti Kanisani na unaondoka ukiwa na mipango yako ya dhambi.
Ni muhimu sana kumtii BWANA YESU siku zote haijalishi uko kanisani, kazini, shuleni au njiani.
Kwanini ukiwa  kanisani unakuwa mtakatifu sana na kila mtu anakusifia na kutamani  kuishi maisha kama yako?  kumbe Ukiondoka ibadani unakuwa mpagani maana utakatifu wako ni wa ibadani tu, Je Itakusaidia Nini Kujifanya Mnyekevu Ndani Tu Ya Jengo La Kanisa? 
Na Ukitoka Nje Ya Kanisa Ni Mdhambi Mkubwa?
Itakusaidia Nini Watu Wakakusifu Kila Siku Kwamba Hakuna Aliyeokoka Zaidi yako Lakini Kumbe Neno Sahihi Ni Kwamba Hakuna Mtenda Dhambi Kama Wewe. 
Ndugu Kuna Hukumu Mbeleni Na Siku Ya BWANA I Karibu.

Obadia 1:15 ''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.'' 

Siku ya BWANA i karibu sana.
Hakuna haja ya kupotesa muda wako kwenye dhambi.
Hakuna haja ya kujifanya mtakatifu kanisani tu.
Hakuna haja ya kujifanya mtenda mema mbele za watu tu wakati ukiwa nyumbani kila siku unampiga mkeo na umemgeuza kama ngoma.
dhambi itakusaidia nini?
Siku ya BWANA kuja kuhukumu iko karibu sana.
Siku hiyo wasanii wa utakatifu watajulikana, je kuna haja gani ya kufanya usanii wa kuigiza utakatifu?
Kuna wengine kazi yao ni kuizoelea tu ibada.
Anafundishwa Neno lakini anachukulia kawaida tu maana anajua na siku nyingine ya ibada atafundishwa. hiyo ni mbaya.
 Ukweli  ni kwamba Kuizoelea ibada kunaweza kumfanya mwamini kudumaa kiroho.

1 Yohana 3:8 ''atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.''

Kushikilia dhambi zako ni kujifanya kuwa mtoto wa shetani lakini BWANA YESU alikuja kuvunja kazi za shetani hivyo tukitaka kuwa wazima kiroho ni lazima tusiizoelee ibada bali tujifunze na kutii kile tunachojifunza.
BWANA YESU yuko katika neno lake ili atuweke huru.
Kama tunalizoea na kuliona la kawaida neno la MUNGU hakika tunapoteza mengi.
Kuna watu ni viongozi kanisani lakini wamekubali kuwa wasaliti katika ndoa zao kwa kutoka nje ya ndoa zao.
Kuna watu ni waimbaji kanisani lakini uasherati na uzinzi unawahusu. ndugu utapata faida gani katika uonvu huo?

Uzinzi ni mwanandoa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Uasherati ni watu wasio ingia kwenye ndoa kufanya mapenzi.
Kama mwanandoa atafanya mapenzi na MTU asiyeingia kwenye ndoa hapo mmoja atakuwa anafanya uzinzi ni mwingine atakuwa anafanya uasherati na tukio lunalofanywa na wazinzi na waasherati linaitwa uzinifu na ni machukizo makubwa sana yanayowapeleka maelfu ya watu jehanamu.
Wewe kama ni mtu wa kanisani unafanya dhambi hiyo naomba utambue kwamba hakuna mbinguni ya wazinzi wala waasherati hivyo ni muhimu kutubu na kurejee kwa BWANA na kuanza kuishi maisha mataktifu ayatakayo MUNGU wa mbinguni.

Matendo 3:19 ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;''

Ushauri wangu kwako ni muhimu na ni huu.
=usikubali kwenda kwenye dhambi.
=Usikubali kwenda kwenye mwaliko wa kufanya uovu.
=Usikubali kwenda kwenye kumbi za starehe.
=Usikubali kwenda kumtukuza shetani.
=Usikubali kumpa shetani utukufu wote  kwa kumtii katika matendo yako.
=Usikubali kuwa na utakatifu wa sikukuu tu bali uwe mtakatifu siku zote za maisha yako.
=Usikubali kufanya machukizo ili tu kuwafurahisha wanadamu.
=Usiende disko wala kokote kwenye tamasha la nyimbo za kidunia.
=Kataa ahadi ya kwenda kufanya dhambi ambayo mliahidiana na yeyote.
=Usikubali kujinajisi kwa sababu tu ya siku ya sikukuu na mapumziko.

Mtii BWANA YESU katika maisha yako yote.
 Isaya 1:16 ''Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; ''

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments