NITAWEZAJE KUKUA KIROHO ? ~03

Mch. Madumla.
Na mchungaji Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
04.HAKIKISHA UNASHIRIKI VIZURI KATIKA MATOLEO.
Kuna aina mbili za matoleo yanayoweza kukufanya ukue kiroho. Aina mbili hizi za matoleo,hutumiwa sana na waamini wenye kiu na shauku ya kufanya kazi ya BWANA na ya kuona ukuaji wa roho zao ukiongezeka siku baada ya siku. Nazo ni;
(A) Kujitoa nafsi yako kwa BWANA kama dhabihu.
(B)Kutoa matoleo ya sadaka za kawaida kulingana na taratibu zilizowekwa.
(A)Kujitoa kwa BWANA.
Sadaka ya kwanza kwa BWANA ni wewe mwenyewe kwa kujiachilia mbele za Bwana kwamba maisha yako yawe sadaka. Neno sadaka ni dhabihu inayotolewa madhabahuni pasipo kuhakiki matumizi yake. Kwa tafsiri hii ni kwamba unatakiwa uyatoe maisha yako kwa BWANA pasipo kujihakiki matumizi yako.
Mfano ; wapo wakristo wenye kuhitaji kukua kiroho lakini wanajihurumia sana kujitoa kwa dhati katika kazi ya Bwana,utakuta mchungaji katangaza watu wote wafike kanisani kushiriki maombi na mifungo,lakini mwingine akishaona kuna kufunga alafu kuna maombi ya mda mlefu basi haji kabisaa!,na hapo hapo anahitaji akue kiroho. Sasa utakuaje kiroho ikiwa ujahamua kijitoa kama sadaka?
Ikumbukwe ya kwamba unahitajika kuutoa mwili  wako uwe dhabihu kama ilivyoandikwa“ Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1
Ukuaji wa kiroho hutegemea pia mkao wako wa kiimani.
Wapo watu wengine mikao yao ni mibaya,yaani hawajakaa vizuri katika matumizi ya miili yao. Utakuta huku anampenda MUNGU na huku anaipenda dunia,yaani hajaamua kwa dhati kuutoa mwili wake kwa kazi ya Bwana. Maamuzi ya kufanya kazi ya Mungu nusu nusu yanakuchelewesha ukuaji wako wa kiroho.
 Hakuna hukuaji wowote ule katika roho yako ikiwa bado unaipenda dunia na mambo yake. Mfano,kijana aliyeokoka na anatamani akue kiroho,lakini bado ni mzinzi au mwesharati wa kawaida tu,tena akijidanyanya nafsi yake afanye dhambi hiyo kwa siri ili washirika wenzake wasimuone,papo hapo amesahau kuwa MUNGU anamuona kila kitu. Au mfano mtu ameokoka lakini bado ni mwizi fulani hivi,kwamba anaweza akamuhibia hata  mumewe pesa,au akawa ni mdokozi dokozi.
Ukihitaji kukua kiroho,ukubali kulipa gharama kwa kuyaacha yote ya dunia na kumuelekea Mungu.
~Kuacha mambo yasiyofaa ya kidunia inawezekana kabisa kwa msaada wa Roho mtakatifu ikiwa kama utamuhitaji,Yeye yupo kwa ajili yako. Kama wengine wameweza,wewe kwa nini usiweze?
Biblia inaposema “, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ” Ina maana pia,kutoichezea miili yetu kwanza hii miili si yetu ni mali ya BWANA bali sisi tumepewa kama dhamana tu ( 1Wakorintho 6:19-20).
Neno limeweka mkazo wa kuitunza miili ambayo ni hekalu la Roho mtakatifu. Ni pamoja na kushughulikia uvaaji mzuri wa miili hii tuliyopewa kama dhamana.
Ukihitaji kukua kiroho jiangalie unavaaje kwanza? Kama ni binti;~nguvo zako zikoje,je hazichochei matamanio kumfanya mwanaume anayekutazama ahisi vibaya hata kutamani kukutongoza? Au ikiwa ni mwanaume~Je unavaaje?Je nguo zako zimekustili kwa heshima kiasi kaamba hakuna uwazi wowote wenye kumfanya binti akuhisi vibaya? Mfano;Wapo vijana wa kiume wenye kuvaa shati kisha wanaacha wazi kidogo sehemu ya kifua ili nywele za kifuani(garden )zionekane,maana anajua kwamba atafanikiwa kuwanasa mabinti wenye kuchanganyikiwa na hilo garden lake.Acha mara moja mitego hii ya kishetani,na uanze kujistili vizuri kama watakatifu wanavyojistili kwa heshima.
Amua kujidhabihu kwa BWANA,uwe sadaka kama dhabihu ili muda wote upatikane uweponi mwa MUNGU. Kanisa liwe rafiki kwako,na hapo utaona ukianza kukua kiroho.
(B)Kutoa matoleo ya kawaida,sadaka zilizoamriwa.
~Mfano wa matoleo haya ni kama vile sadaka mbali mbali (sadaka za kawaida,sadaka za uinjilisti,sadaka za shukrani,sadaka za ujenzi N.K kulingana na utaratibu wa kanisa lako),Fungu la kumi,malimbuko,N.K
Sasa,ikiwa kama utashiriki vizuri katika eneo hili la matoleo pale unapoabudu,basi ni dhahili kabisa matoleo yatakunyanyua kiroho pasipo hata kujijua.
Mfano,matoleo kama fungu la kumi yatalinda kipato chako,na kukuwekea ulinzi wa kazi yako uifanyayo kwa mkono wako. Hivi unajua ikiwa kama uchumi wako ukizidi kudorola ndivyo hata uhuru wa kuabudu hupungua? Maana hutashindwa hata kumtolea BWANA dhabihu,au fungu la kumi. Mfano waweza ukawa unaomba vizuri kabisa,lakini unafikiria ukimaliza kuomba watoto hawajala,au unahitajika kwenda kanisani lakini nauli hauna N.K
Ila kumbuka kwamba,hata kama huna kitu lakini unapaswa kuabudu katika roho na kweli pasipo kufungwa na pesa wala mali,cha msingi uwe mwaminifu tu. Kwani pesa ni kitu gani mbele za Bwana?. Ila kama utajitahidi kushiriki kwa uaminifu wote katika matoleo mimi ninakuhakikishia hutakuwa hivyo ulivyo leo bali utakua na kuongezeka kiroho,kiasi kwamba MUNGU atafungua hata fahamu zako ili neno,maharifa yake ikakae kwa wingi.
Sasa,wapo watu ambao si waaminifu katika kulipa fungu la kumi au kutoa sadaka nzuri mbele za BWANA lakini papo hapo wanatazamia kukua kiroho. Mimi nakushauri bure,usiwe mmoja wao,bali wewe hakikisha unalipa zaka,unakuwa mwaminifu katika matoleo mengine maana kwa njia hiyo utakuwa kiroho…
ITAENDELEA…
~Ikiwa kama unahitaji maombi na kuongea nami moja kwa moja,basi usisite kunipigia kwa namba yangu hii +255 655 11 11 49.
Mchungaji Gasper Madumla.
Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)
UBARIKIWE.

Comments