![]() |
Na:
STEVEN NAMPUNJU (AP),UFUFUO NA UZIMA MOROGORO.
Utangulizi:
Ipo
tofauti kati ya kunyamaza na kutulia. Mtu anapokuwa amenyamaza, anakuwa kimya,
hatoi majibu wala maamuzi yoyote. Lakini Utulivu ni ile hali ya kuwa kimya. Katika Biblia haipo mahali
pengine popote ambapo Mungu ametoa ahadi kubwa kama hii ya kutonyamaza wala
kutulia, kama ilivyoandikwa katika ISAYA
62:1…[1 Kwa ajili ya
Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake
itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.]...Yerusalem
ni makao matakatifu wanapokaa watu wa Mungu. Vivyo hivyo, hata katika taifa
lako, Mungu hawezi kutulia wala kunyamaza unapomuita. Mungu wetu ni kweli, na anaposema kweli, kila uwongo hujitenga.
Sayuni yako kwa leo ni Tanzania, ambayo kupitia hiyo, Mungu anataka akutoe sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Sayuni ilikuwa “ngome ya Wayebusi”, na ikiwa sehemu
moja na mji wa Yerusalemu. Imeandikwa katika ISAYA 65:1-7…[ Watu wasionitaka wanauliza habari zangu; nimeonekana na hao
wasionitafuta; naliliambia taifa lisiloitwa kwa jina langu, 2 Nitazameni,
nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao
katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe; 3 watu wanikasirishao
mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza
uvumba juu ya matofali; 4 waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao
pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika
vyombo vyao; 5 watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana
mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao
mchana kutwa. 6 Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini
nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao; 7 maovu yenu na maovu
ya baba zenu pamoja, asema Bwana, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na
kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao
vifuani mwao.]… Mungu anasema hawezi kunyamaza kwa
ajili ya mtu anayetengwa na jamii yake.
Mungu anaweza kunyamaza kwa habari ya adui zangu, lakini kwa upande wetu
Mungu hawezi kunyamaza kamwe‼!.
Tunajifunza kuwa Samsoni alikuwa mnadhiri wa Mungu
tokea akiwa tumboni. Kwa hali hiyo,
Mungu hawezi kumuacha mtu kama huyu, kwa
kunyamaza tu pale anapomlilia. Yapo mengi
yanayoweza kumfanya Mungu anyamaze unapomuita.
Mji unaweza
kufungwa, na hata viongozi wake kufungwa kwa malengo fulani. Imeandikwa katika YOSHUA 6:1-27 ..[ Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa
kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia.
2 Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme
wake, na mashujaa wake. 3 Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita,
mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita.4 Na makuhani saba watachukua
tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba
mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. 5 Kisha itakuwa
watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya
tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka
chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili. 6 Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita
makuhani, akawaambia, Lichukueni sanduku la agano, tena makuhani saba na
wachukue tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana.7
Naye akawaambia watu, Piteni mbele, mkauzunguke mji, na hao watu wenye silaha
na watangulie mbele ya sanduku la Bwana. 8 Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema
na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo
waume mbele za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la
agano la Bwana likawafuata. 9 Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao
makuhani waliozipiga tarumbeta, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo
sanduku; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. 10 Yoshua
akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno
lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele,
ndipo mtakapopiga kelele. 11 Basi akalipeleka sanduku la Bwana liuzunguke huo
mji, likauzunguka mara moja, kisha wakaenda kambini wakakaa kambini.
12 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema,
nao makuhani wakalichukua sanduku la Bwana. 13 Na wale makuhani saba
wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana,
wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao
waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakizipiga tarumbeta
walipokuwa wakienda. 14 Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea
kambini; ndivyo walivyofanya siku sita. 15 Ikawa siku ya saba wakaondoka
asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara
saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba. 16 Hata mara ya saba
makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa
maana Bwana amewapeni mji huu. 17 Na mji huu utakuwa wakfu kwa Bwana, mji
wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye
na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi
tuliowatuma. 18 Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije
mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo
mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha. 19 Lakini fedha
yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa Bwana;
vitaletwa katika hazina ya Bwana. 20 Basi watu wakapiga kelele, na makuhani
wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao
watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi
kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea
kukabili mbele; wakautwaa huo mji. 21 Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote
vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, na
kondoo, na punda, kwa makali ya upanga. 22 Naye Yoshua akawaambia wale wanaume
wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo
mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia. 23 Basi wale
vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na
ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia;
wakawaweka nje ya matuo ya Israeli. 24 Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na
vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba,
na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya Bwana.25 Lakini Yoshua
akamhifadhi Rahabu, yule kahaba, na watu wa nyumba ya baba yake, na vitu vyote
alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa sababu aliwaficha
wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko. 26 Naye Yoshua
akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule
atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa
kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa
kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo. 27 Basi Bwana alikuwa pamoja na
Yoshua; sifa zake zikaenea katika nchi ile yote.]….Kuna
mahali wana wa Israeli walipaswa kwenda, lakini Yeriko ikajengwa haraka ili kuwazuia.
Kuna mahali ulipaswa uwe au ufike, lakini adui zako wakaufunga mlango ili
usipenye kabisa.
Swali: Kwa nini Yeriko ifungwe kwa wajli ya wana wa Israeli? Hata wewe, kuna
waliojenga ukuta kukuzuia usifanikiwe au kufikia kule ambapo Mungu
alikusudia.Siri ya kufanikiwa kwa wana wa Israeli ilikuwa kupiga kelele‼! Ndani
ya ule mji waliteka nyara, wakatwaa
utajiri,kila kilichokuwa chema ndani ya huu mji. Unapozuia taifa la Mungu,
wakiingia kwako wanaondoka na vile vyako. Ndicho kulichotokea kwa wana wa Israeli.
UKIRI
Leo sitanyamaza, katika Jina la Yesu. Chochote
kilichowekwa mbele yangu ili ninyamaze, leo sitanyamaza kwa Damu ya Yesu.
Amen.
|
Unapkutana na vikwazo pande zote, ujue kuwa umebeba
muujiza ndani mwako. Katika hali yoyote unayoipiita, usimwache Bwana. Kuna
nyakati ambapo, baraka na mafanikio
yanakuwa yamefichwa ndani ya taabu zako. Kwenye Goliath kulitukana taifa la
Israeli, ufalme wa Daudi ulikuwepo. Unapompiga Goliath, ufalme unakuja kwako. Wapo watu ambao hawawezi kuupata ushindi kamili, kwa sababu
ya kuvunjwa moyo au kukumbana na vikwazo mbalimbali. Unapaswa kukataa
kunyamazishwa, ung’ngane kwa namna yoyote ile hadi ukombozi wako uwe dhahiri
kwa kuonekana katka Jina la Yesu.
Sayuni ni tafsiri ya mji ulioimarika. Ahadi za
Mungu kwa ajili ya Sayuni zimeandikwa pia
katika ZABURI 87:2…[Bwana ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.]… Shetani hawezi kutawala popote
au kumtumikisha mtu yeytoe kama hana
faida. Baada ya Daudi kuiteka Sayuni, ulipewa jina la Mji wa Daudi. Imeandikwa
katika 2SAMWELI 5:1-10…[ 1
Ndipo kabila zote za Israeli
wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa
wako na nyama yako. 2 Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu,
wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli watoke nje, na kuingia ndani. Naye Bwana
akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya
Israeli. 3 Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye
mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za Bwana; wakamtia Daudi mafuta
awe mfalme juu ya Israeli. 4 Daudi alikuwa amepata miaka thelathini alipoanza
kutawala, akatawala miaka arobaini. 5 Huko Hebroni alitawala miaka saba na
miezi sita; na katika Yerusalemu alitawala miaka thelathini na tatu juu ya
Israeli wote na Yuda. 6 Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili
kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi,
wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania
ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo. 7 Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu
ndio mji wa Daudi. 8 Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi,
na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho
yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete
hawawezi kuingia nyumbani. 9 Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji
wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani. 10 Naye Daudi
akazidi kuwa mkuu; kwa maana Bwana, Mungu wa majeshi, alikuwa pamoja naye.]…
Sayuni ilikuwa ngome, ambayo baada ya kupigwa na Daudi, ilibadilishwa jina. Wapo Wayebusi waliokaa
katika hatima yako.
Wayebusi waliokaa ndani ya Sayuni, walikaa pamoja na
Israeli. Yoshua alishindwa kuwondoa Wayebusi kwa sababu walikuwa watu hodari.
Hata hivyo, Daudi alikuja kuuteka huu mji na ngome yao na kubadilisha Jina la
Mji huu kuitwa Mji wa Daudi.
1
WAFALME 8:1…[Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa
kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani
huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa
Daudi, yaani, Sayuni.]… Huu ni udhihirisho wa Mji wa Sayuni, uliotekwa
na Daudi na kuitwa Mji wa Daudi.
2NYAKATI
5:2…[Ndipo Sulemani alipowakusanya
wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa
Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji
wa Daudi, yaani, Sayuni.]…Kupitia Sayuni, ukoo wa Yesu ulitokea
hapo.
UKIRI
Ngome yoyote iliyopewa jina ili kunizuia nisipate
vyangu niachie kwa Jina la Yesu. Achia leo kwa Jina la Yesu. Yeyote unayekuja
ili uninyamazishe, leo uniachie kwa damu ya Yesu. Kuanzia leo, na kuanzi sasa
roho yoyote iliyotumwa kwangu ili kuninyamazisha leo naikataa kwa Damu ya
Yesu. Kuanzia leo sitanyamaza kwa Jina la Yesu. Achia maisha yangu, leo
nakataa kunyamaza katika Jina la Yesu. Amen
|
Mungu
anaposema kwa ajili ya Sayuni
hatanyamza ni kwa sababu Sayuni ni mji wake na israeli ni Taifa lake. Kwenye
maisha yetu, Mungu hawezi kunyamaza pia. Shetani anaweza kuona miisho ya jambo kabla ya hilio
jambo kutokea.
Vita inapotokea kwako ni ili unyamaze. Magonjwa
yanapokuja kwako ni ili unyamaze. Shetani alitaka kumnyamazisha Ayubu lakini
Ayubu akakataa kunyamazishwa. Shetani akatumiambinu zote,ikiwemoyakumtumia mke
wa Ayubu,lakini Ayubu akakataa kunyamazishwa. Ukikataa kunyamaza Mungu
ataingilia kati na utashinda.
Paulo na Sila walikatazwa wasihubiri kwa habari za
Yesu Kristo, na walipokataa kunyamazishwa wakawekwa gerezani. Wakiwa ndani ya
gereza, waliendelea kupiga kelele za shangwe na kumwimbia Bwana Mungu. Usiku
ule ule, malaika wa Bwana alikuja na
kuondoka na wale waliokuwa wakimwimbia Bwana na wafungwa wengine wakabaki mle ndani wakishangaa. Kataa kunyamazishwa kwa
Jina la Yesu hadi ushindi wako utokee.
Kama sina watoto sitanyamaza‼ Kama sijapata afya
sitanyamaza‼. Raheli alikataa aina zote za faraja za wanadamu, akiulizia wapo
wapi watoto wake? Wakiweza kukunyamazisha,
maana yake wamefanikiwa kumiliki hatima yako. Bartimayo wakati akitaka
kuupata muujiza wake, walitokea watu wa kumnyamazisha. Hata hivyo, Bartimayo
hakukubali kunyamazishwa na aliendelea kupaza sauti yake, hata alipopata uponyaji wake. Ngome yoyote mbele yako ipo kwa ajili
ya kuzuia mafanikio yako. Anayekunyamazisha ni yule anayetaka ukae katika hali ulioyo nayo.
Endapo yupo mtu ambaye haujaokoka, na upo katikati
yetu, ni vyema leo kufanya maamuzi ya kuja kwa Yesu na kuokoka.
Comments