USIUFUATE MWILI BALI OKOKA.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU apewe sifa ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo nazungumzia Mwili.
Ndugu Usiufuate Mwili Bali Mtii MUNGU. 

Wagalatia 5:16-17 ''Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.''

= Mwili Ni Adui.
=Mwili Una Mawazo Machafu Ambayo Ndio Chanzo Cha Anguko
Kuufuata mwili ni kufuata mambo ya dunia ambayo Biblia inakataza.

2 Kor 10:3-5 '' Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;  (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;''

 Mawazo Na Fikra Ndio Injini Ya Mwili.
 Dhambi Huanzia Akilini Na Kutekemkia Moyoni. 
Alivyo Mtu Moyoni Ndivyo Alivyo

Mithali 23:7a ''Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo''

=  Ndugu Sulubisha Mwili Wako, Omba.
Kuna watu miili yao imewasababishia wakawa mbali na Wokovu wa MUNGU ambao uko pekee katika BWANA YESU.
Kuna watu hufanya matendo mabaya wakidhani ni sawa tu, huenda kanisani na kudhani ni sawa tu. ni mbaya sana.
Wengine  hudhani wana MUNGU lakini huku wakiendeleza mambo ya mwili. Ni mbaya sana.
Japokua watu wengi wanateswa na miili yao lakini jawabu lipo.
jawabu ni YESU KRISTO.
Mimi ngoja nifafanue jinsi ya kuokoka.
Kumpokea YESU KRISTO ni:
   1. Kujua wewe ni mwenye dhambi na kumgeukia MUNGU na kutubu.
   2. Kumtegemea MUNGU akusamehe.
    3.Kumkaribisha YESU KRISTO atawale maisha yako kwa imani ili uwe kama anavyopenda.


Baada ya hayo jina lako litakuwa limeandikwa mbinguni kwenye kitabu cha uzima na pia utakuwa na kinga yaani damu ya YESU KRISTO dhidi ya majini, mapepo na wachawi maana ukiliitia jina la BWANA muda wowote utapona.

 Warumi 10:9-10 '' Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.''

 Biblia pia iko wazi ikizungumza kwamba nje na KRISTO hakuna uzima wa milele, hivyo kwa yeyote anayeutaka uzima wa milele ni muhimu sana kumpokea YESU.

 ''Yohana 14:6 ''YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi.''

Ni faida kuu kumpata YESU KRISTO maishani mwako.

  Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. '' 

 BWANA YESU mwenyewe anasema juu wanaouhitaji uzima wake wa milele kwamba 
 '' Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.   - Mathayo 11:28'' 

Kuna faida kubwa kuokoka na kuanza kuishi maisha mataktifu.
Kumpokea YESU na kumtii ni uzima kabisa.
Hakuna uhakika wa uzima popote ila kwa BWANA YESU .

 Warumi 8:1''Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU.'' 

Je umempokea YESU?
Kama umempokea YESU unatakiwa uanze kuishi kwa kuongozwa na ROHO wa MUNGU.
Kama umeokoka hakikisha haufuati mwili bali neno la MUNGU.
Wale wanaufuata Neno La MUNGU Biblia inasema hivi juu yao.
 Ni heri kuokoka  na kuishi maisha matakatifu ili uwe na uhakika wa uzima wa milele.

2 korintho 5:17  '' Mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya tazama ya kale yamepita , na tazama yamekuwa mapya''

Ndugu, Usiufuate Mwili bali okoka na anza kuishi maisha matakatifu. 

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments