AINA YA KWANZA YA WATU(SPONJI)

Na Mtume Peter Nyaga.
Somo la Leo. .....
Utangulizi
• Katika kila watu 10 kuna vichaa 2
• Kuna watu wanakwaza mpaka hautamani kuishi nao
• Hao vichaa 2 wamewekwa maalumu ili kukushughurikia usije ukaota kiburi.


Katika jamii tunayoishi sasa kuna aina na makundi mbalimbali ya watu. Kunawengine ni waungwana sana, wengine wakorofi sana, wenye tabia nzuri na wenye tabia mbaya pia.


AINA YA KWANZA
SPONJI


1. Kazi kumbwa ya mtu wa aina hii ya sponji kama unavyojua sponji kazi yake ni kufyonza tu mara inapowekwa kwenya maji huachukua maji kutoka kwenye bakuli na kuyahamishia kwake.


2. Mtu huyu wakati wote ana uhitaji, lakini kamwe hatoi kitu kwako. Anasema chako ni changu na changu ni changu.

3. Ni mtu anayetumia vitu na mali za watu wengine kwa manufaa yake binafsi na kamwe hawezi kuwaza wala kupenda kutoa vyake kwa wengine.

4. Anataka yeye tu, ndiye wapewe. Asipopewa anakuwa mkali na lawama nyingi na wakati mwingine kususia jambo fulani. Lakini yeye asipotoa anataka aeleweke na ichukuliwe kuwa ni bahati mbaya hajatoa na ni kawaida tu. (mambo madogo)

5. Huwa hatoi sadaka wala mafungu ya kumi kanisani wala michango yeyote ya harusi au jumuiya fulani. Neno SINA kwake ndio kama wimbo wa taifa anauimba kila iitwapo leo.

6. Yeye anapokuwa na jambo linalo mhusu, huwa wakwanza kuchangisha na kudai michango hata kama ni kwa nguvu atataka achangiwe au asaidiwe tena kwa haraka bila ya kucheleweshwa.

7. Wakati mwingine hudai michango kana kwamba niyeye aliye kukopesha kumbe ni msaada au mchango anadai kwa nguvu na vibaya mpaka inakuwa kero kwa yule anayetaka kumchangia au kumsaidia.

8. Sponji hujihalalishia kwamba yeye ni maskini hivyo anakibali maalum na sababu nzuri za kutokutoa. (Excuses)

9. Sponji Haina Uwezo wa Kutunza Maji Iliyoyanyonya Chomboni
Mara nyingi sponji inaponyona maji kutoka kwenye chombo, ukiitoa nje ya chombo huwa haina uwezo wa kuyatunza yale maji iliyoyanyonya kutoka kwenye chombo na kuyahifadhi, badala yake yale maji hudondoka na kupotea kabisa.

Ndivyo alivyo mtu huyu aina ya Sponji hata kama atapata pesa na mali kwa kunyonya kwa wengine mara nyingi ni watu wasio na maendeleo kabisa kwani huwa hawana uwezo wa kutunza na kumiliki vile walivyoweza kunyonya kutoka kwa wengine.

10. Sponji ni mtu maarufu sana kwa kukopa na kamwe halipi deni. Ukikomalia kumdai urafiki wenu unaishia hapo napi hata kulipa kabisa.


Soma Neno la Bwana....
Methali 18:1 Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe;Hushindana na kila shauri jema.
.......
1:yohana 2:11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
.........
1Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
..........
1Yohana 4:20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
........
Yakobo 3:16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
..........
Mwanzo 4:8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
9 BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
......
Methali 18:1 Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe;Hushindana na kila shauri jema
..........
1:yohana 2:11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
.......
1Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake....



1. Bega ndicho kiungo chenye uwezo mkubwa wa kubeba mzigo mzito kabisa kuliko kiungo kingine chochote katika mwili.

2. Gunia zito la kilo zaidi ya 100 hubebwa sio kichwani wala kwingine bali ni Mabegani.


3. Bega Baridi ni aina ya mtu mvivu asiyetaka kufanya kazi kwa bidii.

4. Bega baridi ni mtu anayejilegeza na kukwepa majukumu yake muhimu.

5. Bega baridi anapenda sana kula tena kula vinono, lakini hataki kufanya kazi kwa mikono yake.

6. Bega baridi hutumia nguvu na jasho la wengine kujishibisha na kunufaika.

7. Mwanaume ambaye ni bega baridi humwachia mkewe jukumu la kutafuta pesa za chakula na mahitaji ya familia, ada za watoto mavazi nk na yeye huachelewa kuamka na kupitiliza mezani kunywa breakfast na kwenda kupiga “misele” au kushinda akiangalia TV huku mkewe akihangaika na vibiashara huko na huko.

8. Bega baridi amejawa na roho ya uvivu na uzembe, bila ya kuhimizwa na kufuatiliwa huwezi kufanya kazi wala hawezi kumaliza kazi aliyopewa..
Mithali 14:23
“Katika kila kazi mna faida, bali maneno ya midomo huleta hasara tu.”
2Thes 3:10
“Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu, tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi asile chakula.”
Mithali 19:15
Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.


9. Mtu huyu hujitenga na kukwepa kuchangamana na watu.
Mithali 13:4
Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.


10. Bega baridi ni mtu anaye wahi kulala na kuwa wa mwisho kuamka.
Mithali 12:27
Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.


11. Bega baridi Hapendi kubeba jukumu lolote. Kila jukumu atakalopewa atatoa sababu au udhuru.
Mithali 20:4
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.


12. Yeye hupenda kupewa uhuru wa kujifanyia kile anachotaka yeye, na anapowewa huo uhuru huwa anashindwa kuutumia vizuri.
Mithali 21:25
Matakwa yake mtu mvivu humfisha, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.


13. Bega Baridi Hapendi mambo ya kusimamiwa, na anapoachwa pekeyake hawezi kujidhibiti.
MUNGU akubariki sana.
By Apostle Peter Nyaga 


Comments