AINA ZA SADAKA(2)

Na Mwalimu Nickson Mabena


KWA NINI TUNATOA SADAKA!?.
Kwenye sehemu iliyopita, nilikupa Sababu mbili, za Kwa nini tunatoa Sadaka,
Sababu hizo, ni
1.AGIZO LA MUNGU
2.UPENDO

Niliishia kuelezea kidogo hiyo sababu ya pili, ya Upendo!.
Nataka nizungumze kitu kimoja Muhimu, kwenye hii sababu ya Pili.
Kumbuka hivi, tunatoa Sadaka kwa Moyo, na Moyoni ni makao ya Imani, Biblia inasema "Kwa maana kwa MOYO Mtu huamini.....". RUMI 10:10
Kwa hiyo ninaweza kusema, Sadaka, tunatoa kwa IMANI.
Na Imani, Chanzo chake ni Kusikia neno la Mungu (Rumi 10:17),
Na Imani, ni Kuwa na HAKIKA na Mambo yatarajiwayo (EBR 11:1).

Kwa hiyo, tunatoa Sadaka huku ndani yako ukiwa na Uhakika wa kupokea Jambo fulani toka kwa Mungu!.
Nikupe Mfano, Mmoja nahisi utanielewa vizuri, SOMA MWANZO 22:1-14)
Mungu alimpa Ibrahim Mtoto uzeeni, kisha Mungu akamjaribu Ibrahimu, amtoe mwanae Isaka kama Sadaka!.
Kujaribu maana yake Kupima, Mungu alikua anapima nini kwa Ibrahimu!?.
Mungu alikua anaupima Upendo wa Ibrahimu, kwa Mungu.

Ndio maana baada ya kukubali kumtoa, Mungu akamwambia SASA NAJUA KAMA WANIPENDA..
Kwa kiswahili kingine naweza kusema, alimwambia, nilikua sijui unanipenda kwa kiasi gani, sasa ndio nimejua...
Ibrahimu, Kwa IMANI, alikubali kwenda kumtoa Isaka, kwa sababu ya UPENDO wake kwa Mungu!.
Kama Ibrahimu, angempenda Isaka kuliko Mungu, basi asingemtoa Isaka. Lakini Ibrahimu alimtoa Isaka, kwa sababu alimpenda Mungu kuliko Mtoto wake wa Pekee!.
Ukitaka Kujua kiwango cha Upendo wako kwa Mungu, usiangalie kitu kingine.
Angalia KUTOA KWAKO.
A)Kutoa fedha zako kwa Ajili ya Mungu
B)Kutoa Muda wako kwa ajili ya Mungu!.
(Rumi 12:1-2)


THAMANI YA SADAKA!.
Kwenye Utoaji, Mtu unaweza ukatoa Fedha, Vitu, Mda, au Mwili wako vikawa SADAKA!.
Unapoenda Kanisani, Ukatoa Gauni, kama hukutoa kwa Imani, hiyo sio sadaka bali Msaada, lakini Ukitoa kwa Imani, ndio Inakua Sadaka!.
Ok, turudi kwenye lengo letu,
Lengo la kipengele hiki, ni kukufundisha UBORA wa sadaka, ili sadaka yako iwe na Thamani Mbele za Mungu, vigezo gani vinaangaliwa!?.
Je! Ni kweli hadi nitoe hela nyingi sana, ndio sadaka yangu ikubalike Mbele za Mungu!?.
Nikitoa hela kidogo, inamaanisha Sadaka yangu haina thamani kwa Mungu!?.
Nakufundisha hili kwa sababu, Unapotoa Sadaka, lazima Utarajie kitu flani toka kwa Mungu, ndio maana wanasemaga, sadaka yako itamkie Maneno, unataka nini kupitia hiyo sadaka!.
Kama utakua unatarajia kitu toka kwa Mungu, maana yake Utatoa Sadaka yenye thamani, na Usipotoa sadaka yenye thamani, maana yake utatoa Kimazoea!.
Bwana Yesu atusaidie Sana!.
Hapa, nitaongea sana, hata Kugusia Michezo michafu inayofanywa Na Viongozi wa Baadhi ya Makanisa!!.
Tusome kwanza Maandiko!.
"Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku, Majiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, amin, nawaambia, Huyu mjane maskini, ametia zaidi kuliko wote wanaotoa katika sanduku la hazina; maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umasikini wake ametia vyote alivyokua navyo, ndiyo riziki yake yote pia." MARKO 12:41-44
Hayo maneno sio mepesi sana, lakini ndiyo kweli!.
Yesu anasema Mwanamke sadaka yake INA THAMANI ZAIDI, ya wale matajiri, japokua sadaka yake ilikua ni ndogo kuliko wale Matajiri!.
Angalia, kama ungemtafuta Mtu, ukamtaka akwambie Sadaka ipi ni Kubwa kati ya hizo, Angesema ni zile za Matajiri!.
Lakini, Mungu haangalii kama wanadamu waangaliavyo, Wanadamu wanaitazama Sura ya Nje, bali Bwana anaangalia Moyo (1SAM 16:7).
Mwanamke, alitoa kama Ibrahimu alivyotoa, alitoa kwa Moyo, Alitoa kile Roho Mtakatifu alichomwambia, na Sadaka yake, ikapata Kibali Mbele za Mungu!.
Kwa hiyo, ninaweza nikasema hivi, UBORA, au UTHAMANI wa SADAKA yako, hautegemei, wingi wa Fedha unayotoa, unaweza Ukatoa Vingi, lakini Sadaka yako Ikakataliwa!!. 

 kuna Maswali nimewahi kuulizwa, kupitia kipengele hiki, majibu yatapatikana!.
Maandiko katika Biblia, yanasema hivi
"Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume, Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?. MDO 5:1-3

Ukiweza soma habari yote hadi Mstari wa 11,
Anania na Safira walipouza Kiwanja, Roho Mtakatifu aliwapa Maelekezo ndani yao, ya kiasi cha kupeleka Miguuni kwa Mitume, maelekezo hayo, ndio yalikua yanaonyesha THAMANI Halisi ya Sadaka yao kwa Mungu, Maana yake, kama watapunguza, kama walivyofanya, watakua wanapunguza THAMANI YA SADAKA YAO!.

Roho Mtakatifu, ndiye anakupa Msukumo wa kutoa kiwango fulani cha fedha!, ingawa wakati mwingine, inakua ngumu kutii, kutokana na Mazingira uliyonayo,
Kwenye baadhi ya Makanisa, hufanya huwapangia watoaji wa Sadaka viwango vya kutoa sadaka, kwa lengo la kukusanya Mapato Mengi, lakini sio kwa lengo la kuwasaidia watoaji kubarikiwa na Mungu!.
Ukifika, kanisani Usitoe Sadaka, chini ya Kiasi kadhaa, huo ni Uhuni!.
Wengine wanasema toa kiasi kadhaa ili nikuombee, huu ni uhuni pia!.
Nimewahi kusikia mtu amempeleka ndugu yake akaombewe kwenye kanisa flani, Akaambiwa mgonjwa wako hatumuombei hadi utoe Laki moja!,
Hao ni matapeli tu kama wale Vibaka wa Ubungo!!.
Kiasi cha Kutoa, kinawekwa Moyoni mwako na Roho Mtakatifu!.
Anania, na Mkewe, waliona kiwango walichoambiwa na Roho Mtakatifu kutoa ni kikubwa sana,
Sasa Sijui, pengine walidhani Mitume watafaidi, kama wanavyosema watu wa sasa kwamba WACHUNGAJI WANAFAIDI,

Wao walipunguza kwa siri, walizani hawaonekani, kilichotokea ni Kifo cha wote wawili, kwa Sababu wamemwambia Uongo Roho Mtakatifu!.
WAKATI MWINGINE, MAZINGIRA ULIYONAYO YANAWEZA KUKUFANYA USITOE SADAKA KWA KIWANGO KILE MUNGU ALICHOKUSUDIA UTOE, LAKINI KUMBUKA, MUNGU HANA MPANGO WA KUTUFILISI, BALI ANA MPANGO WA KUTUBARIKI,
ANAPOKWAMBIA UTOE KITU FLANI, AU KIASI KADHAA CHA FEDHA, HATA KAMA KWA MACHO YA KIBINADAMU UNAONA KUPUNGUKIWA, LAKINI MUNGU, NDIO ATAKUBARIKI ZAIDI!.
Mara nyingi sana, watu wengi, hupingana na Roho Mtakatifu,
Anaweza akapata Msukumo wa Kutoa fedha kwa Mtu, akimuangalia pengine ana uwezo mKubwa kuliko yeye, alafu kiasi cha fedha anachoambiwa kutoa ni kidogo sana, anaanza kukidharau, na kufikiri kwamba atakuonaje!.
Au, Unaambiwa kutoa kiasi cha fedha, ambacho ni hela yako ya mwisho, unaanza kumpinga Roho Mtakatifu, unawaza kwamba utabakiwa na nini!.
MUNGU ANAKUA ANATAKA KUKUBARIKI KUPITIA HICHO KIDOGO ANACHOKWAMBIA UTOE!!.
Mungu akubariki kwa kuwa pamoja na Mimi, ahsanteni kwa kunisikiliza!.
Somo litaendelea!
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments