Ajali ya Basi yapoteza Maisha ya wachungaji wawili na wake zao wakitokea kwenye Kongamano


Ajali ya basi iliyotokea mkoani singida jumatatu usiku baada ya basi kugongana na Lori imefahamika kwamba ndani ya basi hilo walikuwemo wachungaji wawili na wake zao ambapo kwa pamoja walikua wakitoka jijini Dar es Salaam kwenye Kongamano la Wachungaji wa P A G ambalo lilifanyika katika kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church.

Kutoka kwenye Ukurasa wa facebook wa kanisa hiloo wameandika kama ifuatavyo na kuweka picha za wachungaji hao
DPC inasikitika kutangaza kifo cha wachungaji wawili waliopoteza maisha yao jana kwa ajali ya basi wakiwa safarini kuelekea Geita, Wachungaji hao ni kati ya wale waliotembelea kanisa la DPC na tuliabudu nao siku ya jumapili kuanzia ibada za asubuhi na Ibada ya kusifu na kuabudu. Askofu Lema Geita amefariki kwenye ajali hiyo. Habari kuhusu Mkewe bado tunaendelea kufuatilia, Tafadhali chukua wakati kuombea watoto wao waliowaacha na pia ombea makanisa waliokua wakiyaongoza, Mungu awe ndiye Nguzo ya kila kitu, Amina.

Comments