BWANA WA MAJESHI NI MUNGU MWENYE NGUVU.

Na mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Zaburi 24:10 '' Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.''

''BWANA Wa Majeshi'' Ni Jina La MUNGU, Limetajwa Zaidi Ya Mara 200 Kwenye Biblia. 
Kwa Waisraeli, MUNGU Alikuwa Ni "MUNGU Wa Majeshi" Au "BWANA Wa Majeshi". 
Jina Hilo Linamuonyesha MUNGU Akiwa Na Mamlaka, Uwezo Na Nguvu Zote. 
Ukweli Ni Kwamba Hakuna Adui Anayeweza Kumzidi MUNGU Katika Nguvu, Mamlaka Na Uwezo. 

 Zakaria 1:17 ''Piga kelele tena, na kusema, BWANA wa majeshi asema hivi, Miji yangu kwa kufanikiwa itaenezwa huko na huko tena; naye BWANA ataufariji Sayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena. ''

BWANA wa majeshi kwa kiebrania jina jilo lilitamkwa JEHOVAH SABAOTH.
Kwa hiyo JEHOVAH SABAOTH maana yake MUNGU wa majeshi au BWANA wa majeshi.
Hiyo unaweza kuiona katika Biblia ya Kiebrania mfano katika 

1 Samwel 1:3 '' Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.   ''

Manabii Zamani Walipokuwa Wakipewa Ujumbe Na MUNGU, Ni lazima  Ujumbe Huo Utimie Maana Umetoka Kwa MUNGU Na Kwa Kukazia Walisema "Asema BWANA Wa Majeshi". 

 Isaya 1:24-25 '' Kwa hiyo, asema BWANA, BWANA wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitatwaa kisasi kwa adui zangu; nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote; ''

BWANA wa majeshi Ni Jina La Sifa Kuu Ya MUNGU. 
Kumbuka Pia Kwamba Majeshi Ya Israeli Yalikuwa Majeshi Ya MUNGU Yaani Majeshi Ya YAHWEH

1 Samweli 17:45-47 ''Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, MUNGU wa majeshi ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko MUNGU katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.'' 

 MUNGU Anaitwa Hivyo Hata Leo Kwa Sababu Ana Majeshi Ya Malaika Wasiohesabika Ambao Siku Zote Wako Tayari Kutekeleza Maagizo Yake

Zaburi 148:2 ''Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.''

 Malaika ni jeshi la MUNGU kwa ajili ya kutekeleza agizo la MUNGU. 
Lakini pia MUNGU mwenyewe pekeyake  ni zaidi ya jeshi maana yeye ni muumbaji na anajua yote.
Ni lazima tunyenyekee kwa BWANA wa  Majeshi  aliye na uzima wetu.

 1 Wafalme 22:19 ''Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto.''

 Mamlaka Ya BWANA MUNGU Haina Kikomo, Hata Leo Tukiomba Kupitia YESU KRISTO, MUNGU Atatushindia Kudhihirisha Kwamba Yeye Ni BWANA Wa Majeshi. 

Yohana 14:13-14 '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.'' 

BWANA wa  MAJESHI ni MUNGU mtakatifu hivyo lazima tuishi maisha matakatifu siku zote. 
Ona hapa MUNGU wa majeshi akisema. 

 '' Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, Bwana wa majeshi.- Yer 2:19   ''

Hata katika agano jipya bado MUNGU ni MUNGU wa majeshi.
MUNGU ni BWANA wa majeshi na atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake.

Yakobo 5:4 '' Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa BWANA wa majeshi.   ''

 Sisi Ni Silaha Za Vita Vyake.
Na sisi tukiomba BWANA wa majeshi anatujibu na kutushindia.
BWANA haji kutusaidia bali kutushinda.

Mithali 18:10 ''Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama. '' 

Tuende kwa nani wakati BWANA wa majeshi anao uzima wetu?
Tumtegemee nani wakati hakuna mwenye nguvu kama BWANA wa majeshi?
Hakika hatuna wa kumtegemea ila BWANA wa majeshi aliye MUNGU mwenye nguvu sana.

Zaburi 27:1-6 '' BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake. Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba. Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.''
-Kukaa ndani ya KRISTO ndio kukaa ndani ya BWANA wa majeshi.
-Kumtii ROHO MTAKATIFU ni kukaa katika ulinzi wa BWANA wa majeshi.
Hakuna aliye kama BWANA wa majeshi.

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments