HABARI JUU YA MIFUPA MIKAVU.

Na: STEVEN NAMPUNJU. (RP) &
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP), UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi wa Somo: Imeandikwa katika EZEKIELI 37:-1-10…[Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; 2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. 3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. 4 Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. 5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. 6 Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 7 Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. 8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. 9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. 10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.]…Mungu alimuuliza Ezekiel je mifupa hii yaweza kuishi?  Mungu akamwambia Ezekiel aitabirie, aiambie isikie sauti ya Bwana.
Tunajifunza kwamba kumbe kilicho kikavu kinawweza kusikia  sauti ya Bwana. Alipotoa utabiri  mtikisiko ukatokea na mtikisiko huo ukaanza kuunga mfupa . Nyama na ngozi  vikawa juu ya mifupa ile. Baadae upepo ukavuma na upepo huo ukaleta uhai  ndani ya watu.  Ezekieli aliamuru upepo ukaleta uhai.
UPEPO UNA MAJINA:

 Tunasoma katika MATENDO YA MITUME 27:9-13..[Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya, 10 akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia. 11 Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo. 12 Na kwa sababu bandari ile ilikuwa haifai kukaa wakati wa baridi, wengi wao wakatoa shauri la kutweka kutoka huko ili wapate kufika Foinike, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi; nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazinimashariki na kusinimashariki. 13 Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.].. Upepo wa kusi ulileta matumaini kwenye safari yao. Baada ya upepo wa kusi  ukavuma upepo mwingine  ulo kuwa mbaya ambao uliondoa matumaini. 
MATUKIO YANAOWEZA KUTOKEA BAADA YA UPEPO KUVUMA.
  1. Upepo wa Kusi
Imeandikwa katika MITHALI 25:23 kwamba [Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.]. Upepo huu una matokeo mawili makubwa.

Ø  Upepo wa kusi huleta mvua.
Ø  Asinziae huleta uso wa ghadhabu.
  1. Upepo wa  Mashariki
Imeandikwa katika MWANZO 41:23…[Na tazama, masuke saba membamba, dhaifu, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.]… Upepo wa mashariki ukivuma unaweza kukausha na kufanya dhaifu na vyembamba.  Leo umwamini Mungu atuondeee upepo uliovuma katika maisha yako. Hivyo ulivyo leo sio vile ambavyo Mungu alivyokuumba  baada ya kuvuma kwa upepo wa mashariki. Mchawi anaweza kuuamua akutumie upepo gani ili akukamate. Upepo ukivuma unakuja na matokeo yake. Kwenye nnchi yetu upo upepo unavumishwa ili nchi yetu ibaki katika hali ililyo nayo.

Imeandikwa katika HOSEA 13:14-15…[Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu. 15 Ajapokuwa yeye ni mwenye kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya Bwana itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.]… Kukumbuka upepo wa mashariki una nguvu  na unavuma kwa nguvu na kwa bidii. Unaweza ukaa na Baraka zako lakini upepo wa mashariki ukavuma ukakausha kila kitu. Inawezekana wewe unaonekana kuwa ni mkame. Yaani huwezi kusaidika yaani huwezi kuanza chochote,  lakini leo utaisikia sauti ya Bwana.
Imeandikwa katika YONA 4:8 [Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.]… Upepo wa mashariki wenye hari nyingi ukampiga Yona mpaka yona akazimia.
Imeandikwa katika KUTOKA 10:12-15...[Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya Misri, waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe.13 Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige. 14 Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo. 15 Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; hapakusalia hata jani moja, mti wala mmea wa mashamba, katika nchi yote ya Misri.]… Farao alipozidi kuwazuia Mungu akawaletea upepo wa mashariki ambao ulileta nzige waile kila kitu kilichosazwa. Tunajifunza kuwa Upepo wa masharki unaweza kumtoa mtu kwenye nafasi yake.
Kama ilivyoandikwa katika AYUBU 27:21 [Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka;  Na kumkumba atoke mahali pake.].. Upepo huu  ni kana kwamba huu upepo una mikono. Ni kwamba unaweza kumchukua mtu kutoka kwenye nafasi yake aliyopo. Leo tunae Bwana mtenda miujiza atavumisha upepo mwingine wenye Baraka  nao utazirudisha Baraka zetu na kwenye nafasi zetu katika Jina la Yesu.
UKIRI
Ee upepo a masharki ulievumma ili unitoe mahala pangu, leo nakataa kwa jina la Yesu. Nakataa leo kuchukuliwa na upepo wa kila aina. Amen
 
Upepo wa Mashariki waweza kuwa jini, au pepo au mashetani au mchawi kwamba likija kwenye maisha yako na kukutoa kwenye nafasi yako.
UKIRI
Kuanzia leo ee upepo  na alie ndani ya upepo leo nakushinda kwa nguvu ya msalaba kwa jina la Yesu. Amen
 
Mungu ametazama watu leo na ameona kuwa tumekuwa wakame. Ziko familia ambazo hazina matumaini, mtu mmoja mmoja amepoteza matumaini kabisa, wapo watu ambao wamekaushwa, tumeona upepo wa mashariki unaweza kukaausha na kumeza na kubaki kilicho kinyonge. Lakini pia tabia zinaweza kukukausha.
Tunasoma katika ISAYA 43:6… [nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.]. Mungu  anataka watu waletwe toka mbali…kusini toa na kaskazini usizuie.
Magharibi naweza kuotoa upepo wa kutoa nzige, kama ilivyoandikwa katika KUTOKA 10:19 [Bwana akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.]

Comments