HAKIKISHA MANENO YAKO YANATHIBITISHWA NA MATENDO YAKO.

Na Mtumishi Peter Mabula
BWANA YESU atukuzwe sana.
Nakukaribisha tujifunze Neno la MUNGU.
Ni heri sana maneno yako yakathibitishwa na matendo yako.

Warumi 2:16A ''katika siku ile MUNGU atakapozihukumu siri za wanadamu''

Kuna siku ya MUNGU kuzihukumu siri za wanadamu.
Kuna wtu kwa maneno yao huonyesha ni watakatifu sana lakini wakati huo huo matendo yao yamejaa uovu.
Ni Heri Maneno yako yakathibitishwa na Matendo yako.
 
Kuna mtumishi mmoja alienda kuhubiri mkoa Fulani, alipofika huko alihubiri na kuwasema vibaya wachungaji Wa Kule kwamba walelala na hawafai. Jambo hilo liliwaumiza wachungaji wale lakini hawakujibu, waliendelea na jukumu lao na wajibu wao wa kuchunga na kulisha kondoo wa BWANA YESU. Hata mwezi mmoja haukupita yule mhubiri mwenye makeke akakamatwa akizini na mke wa mtu gesti.
Aibu kuu ilimkuta na kumbe akikuwa akiwapeleka watu mbinguni huku yeye hana mpango WA kwenda huko.
Ni hatari sana kuishi maisha bandia huku ukiwaaminisha watu kwamba wewe ni mtakatifu.
Ni heri sana kila mtu maneno yake yathibitishwe na matendo yake.

 Sawasawa na matendo yake kila mmoja atalipwa, sio sawasawa na maneno yake bali matendo maana wengi sana maneno yao mbele za watu ni maneno mazuri lakini matendo yao hayafanani na matendo yao.
Ni muhimu kukumbuka pia kwamba 
'' Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa BABA yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.- Mathato 16:27''



 Kuna watu hujionyesha mbele za watu kwamba wao ni watakatifu.
Ndugu, kama unataka kujionyesha kwamba wewe ni mtakatifu jitenge kwanza na shetani pamoja na mawakala wake.


Yakobo 4:7-10 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza. ''

-Habari za kujionyesha mbele za watu kwamba wewe ni mtakatifu wakati kila siku unashinda kwa waganga WA kienyeji ni kujidannya. mwenyewe.
-Habari za kusema wewe ni mtakatifu wakati unafuga majini na huwa unayatuma kwa watu huko ni kujidanganya.
SAA yaja ambayo kila lililofichwa litakuwa wazi.
Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.


Marko 4:22 ''Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi. Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.''

 Huwezi kumpenda MUNGU kama Neno la MUNGU halimo ndani yako.
-Kama kuna mtu anasema anampenda MUNGU huku neno la MUNGU halimo ndani yake basi huyo anampenda MUNGU kwa midomo tu na sio roho.
Kila mtu leo ukimuuliza ''unampenda MUNGU'' atakuambia nampenda sana lakini mbona anafanya mabaya na kumhuzunisha MUNGU kila siku?
Huyo hampendi MUNGU maana kumpenda MUNGU ni kuchukia uovu.
Kama huchukii dhambi na unazitenda kila siku kisha unasema kwamba wewe unampenda MUNGU napenda tu kukuambia ukweli kwamba wewe ni muongo.

 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.

1 Yohana 2:6 ''Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake(YESU), imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye(YESU) alivyoenenda. ''


Kuna watu pia huenda kanisani na kwa nje huonekana kama ni watakatifu lakini kumbe ndani wana chuki na hasira dhidi ya wengine.
Hayo ni makosa tena ni machukizo.
-Matokeo ya chuki na hasira yanaitwa hasara.
-Chuki yako ukiijumlisha na hasira yako ni lazima tu itakuletea Hasara yako.
Kwa wateule haitakiwi kuwepo chuki hata moja.
 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.

Warumi 12:9-11 '' Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA;''

 Kuna baadhi ya wana kanisa huonekana ni watakatifu mbele za watu lakini ndani ya mioyo yao huongea maneno yasiyo na maana.
- Maneno yasiyo na maana hufyonza nguvu ya MUNGU ndani ya mtu.
Ni mhimu sana kujitenga na maneno mabaya tena ni muhimu sana kujitenga na maneno yasiyo na maana.
usikubali kukaa katika baraza la mwenye misaha na tena ikatae njia ya wakosaji.

 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.

Zaburi 1:1-3 ''Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.''

 Kipimo sahihi cha kupima kama unampendeza MUNGU au unamchukiza ni kusoma neno la MUNGU, maana neno la MUNGU li hai na linayajua makusudi ya moyo, pia neno la MUNGU lina pumzi ya MUNGU, na hatuwezi kujificha mbele ya  neno la MUNGU. 
 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake
Hivyo kwa kusoma BIBLIA utajua kabisa uovu wako mfano utasoma kwamba uasherati, uchawi,ibada ya sanamu na ufisadi ni dhambi.
 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.

Wagalatia 5:19-21 ''Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU. '' 
 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.
Utatakiwa kuacha uovu maana watendao matendo hayo wasipotubu hawataurithi ufalme wa MUNGU. 
 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.
Hivyo kwa kusoma BIBLIA utatambua uovu wako na ukiachana na uovu huo utakua umefanya jambo jema sana.
 Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.
Nasema tena  Ni heri maneno ya Mtu yakathibitishwa na maisha yake.
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments