HAKUNA KATIKATI AU KUCHAGUA YOTE!

Na Frank P. Seth

"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako" (Kumbukumbu la Torati 30:19)
Kuna jambo moja KUBWA mwanadamu atafanya siku ZOTE za maisha yake, nalo litapelekea MAFANIKIO au ANGUKO lake bila shaka. Jambo hili sio jingine ila ni KUCHAGUA.

Sasa angalia, huwezi kumchagua Mungu na Shetani kwa wakati mmoja, mambo ya ulimwengu na uzima wa milele kwa pamoja, utajiri na umasikini kwa pamoja, uzima na mauti kwa pamoja, nk.
Shida kubwa tuliyonayo sasa katika maisha ya watu wengi ni KUDHANI kwamba mtu atafanikiwa kuishi KOTEKOTE na akashida tu bila shida. Kwa mfano, ndoa nyingi zimeshindikana kwa sababu mtu anataka aishi kama SINGLE wakati ni MARRIED! Anataka aishi na VIMADA wakati aliapa kuishi na MMOJA tu! Mwishowake anakemea shetani wakati kwa kweli ALICHAGUA huku akijifariji kwamba mambo yataenda tu! Haiwezekani, chagua moja! 

Angalia jambo hili, watu hudhani maisha yao ni Mungu amewachagulia kwahiyo hawafanyi chochote kwa sababu mwishoni ni Mungu "AMEAMUA" hivyo! Sawa, najua kuna nyakati na mipaka ya makazi kwa wanadamu wote, lakini nakwambia bado USIPOCHAGUA hutapata hata kilichochako kwa maana uliamua NATURE ikuchagulie! 

Mwingine atadhani natania, angalia hapa, hata kuwa masikini au tajiri ni kuchagua pia. Kanuni iko wazi, afanyaye kazi kwa bidii atafanikiwa, na mvivu atakuwa masikini...Je! Si kuchagua tu hapo? Angalia tena, Mungu anabariki kazi za mikono yako, inamaana lazima UCHANGUE kufanya kazi kwa mikono yako ili UBARIKIWE, kinyume na hapo, umasikini utakumaliza kwa kukosa maarifa.

Ni wakati wa kuchagua...acha kusingizia neema huku unatenda yasiyofaa (Neema inatufundisha kukataa uovu..) Kama umejikwaa ukaanguka, CHAGUA kuamka, tubu, usirudie tena hiyo dhambi au kosa, songa mbele..acha kumsingizia Ibilisi...hatma yako iko mikononi mwako mwenyewe.
Frank P. Seth

Comments