HOFU YA MUNGU IKO WAPI

Na Rachel Mashauri  Scharp

Hofu Ya Mungu/kumcha Mungu hutufanya kukaa Mbali na dhambi na hutufanya kufuata maagizo yake na kuishi sawa na mapenzi yake. Kuwa na na hofu Ya Mungu ndio kumcha Mungu. Somo Hili ni pana sana nazungumza kwa ufupi tu. Nitaendelea wakati mwingine.
Mith 1:7 kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa.
Kumcha Mungu ni kukaa mbali na uovu ( mith3:7. Mith 14:16), kwa hiyo kama uovu umekutawala wewe si Mcha Mungu na huna hofu Ya Mungu. Na huwezi kumshinda dhambi kama Uko Mbali na Mungu huombi husomi neno, huna muongozo wa Kiroho.
Kumcha Bwana ( kuwa na hofu ya Mungu)ni kukataa uovu ( mith 8:13, ayub 28:28, mith 16:6-7)

Kuna Baraka na Faida ukiwa na hofu Ya Mungu na kumcha Mungu
Zab 128:1-4Heri wamchao Bwana na wanaoishi kufuatana na amri ZAKE. Utapata Matunda Ya jasho lako.
-kama humwogopi Mungu kumbe hata Matunda Ya jasho lako hutakula

- utapata miaka mingi Ya kuishi ( mith 10:27, 22:4)
- Utarithi uzima wa Milele( math 5:5, Zab 33:12)
Kumb 28:1-14
( Faida za duniani zipo nyingi sana kubwa ni ufalme wa mbinguni)

Hasara ni nyingi sana za kutokumcha Mungu na kutokufuata maagizo yake
- utakosa uzima wa Milele
Na hapa dunia utalaaniwa kumb 28:15-68

Sasa jamani najiuliza hofu Ya Mungu iko Wapi siku hizi satu hawamwogopi Mungu kabisa wanatenda dhambi kirahisi kabisa hawamwogopi Mungu kabisa wengine wanamwogopa mwanadamu badala Ya Mungu. Watu wanatenda dhambi makusudi ili baadae watatubu. Mmefanya damu Ya Yesu kama sabuni Ya kuogea. Tunamsubisha Yesu msalabani mara nyingine?
Watu wanafanya mazoea kabisa mpaka dhambi imekuwa sugu wala hawaoni kama ni dhambi wanafika kipindi wanasema Mungu anajua sisi ni dhaifu jamani ni makusudi kabisa. Mungu ameweka neno lake na atahukumu sawa na neno lake.
Tumrudie Mungu watu wa Mungu tusizoee dhambi hofu Ya Mungu ituingie tuuone macho Ya Mungu yanatufuata wakati wote hata sirini.

Tubu Leo umrudie Mungu nafasi ingalipo kabla Neema haijafungwa.
Shalom

Comments