JE MALANGO YAKO YA KIROHO YANATUMIWA NA NANI NA KUPITISHA VITU GANI KUJA MAISHANI MWAKO?(2)

Na Mwlimu Samwel Kibiriti

SEHEMU YA TATU:
BAADHI YA MALANGO YA KIROHO NA VITU VINAVYOPITA HAPO LANGONI.
Nataka nikuonyeshe baadhi ya vitu vichache vinavyoweza kupita kwenye malango kiroho.

1. DHAMBI HUPITA LANGONI
Nataka utambue kwamba dhambi ni roho inaweza kumtawala mtu na kumtesa pia huwa inakaa langoni kwa mtu au familia au ukoo au mji n.k isipotubiwa.

Tusome MWANZO 4:6-7 Ona Mungu anamwambia Kaini kuwa "BWANA akamwambia Kaini, kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama uukitenda vyema, hutapata kibali? Na usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea MLANGONI, nayo inakutamani wewe, walakini yakupasa Uishinde".
Hapa tunamuona MUNGU akimueleza kaini kwamba dhambi imekaa kwenye mlango wake inamtamani lakini kaini akashindwa kuishinda dhambi nayo ikamshinda na kujikuta anamuua ndugu yake Habili.

Hii dhambi ya uuaji iliyokuwa kwenye malango ya familia a familia ya kaini haikuondoka hapo kwenye malango kwasababu kaini hakuitubia kwa MUNGU na tunaiona inakuja kumvamia kitukuu chake aitwaye Lameki ambaye ni kizazi cha tano kwenye familia ya kaini nayeye akaua MTU kama babu yake alivyomuua ndugu yake Habili.
Tusome MWANZO 4:17-24 Lameki anasema "Lameki akawaambia wake zake, sikieni sauti yangu, Ada na Sila; enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; maana nimemwua mtu kwa kumtia jeraha; kijana kwa kunichumbua; kama Kaini akilipiwa kisasi Mara saba, Hakika Lameki atalipiwa Mara Sabini na saba".
Lameki hapa ameweka wazi kwamba kamuua mtu kama kaini babu yake, unajua nikwasababu gani Lameki ameua? Jibu nikwamba babu yake alishindwa na roho ya dhambi ya uuaji iliyokuwa Langoni wala hakuitubia kwa MUNGU namatokeo yake ikakaa kwenye lango LA familia ya kaini.

Nataka nikuulize wewe Rafiki yangu je kwenye Malango ya familia yenu kuna roho ya aina gani imekaa hapo ambayo mababu na bibi zako waliifanya? Na je kuna mtu ameitubia hiyo dhambi kwa MUNGU ili awasamehe? Na kama haijatubiwa maana yake itawatesa kizazi baada ya kizazi mtakuwa kifungoni.
Ok unafikili nikwanini kwenye familia na Ukoo kuna matatizo sugu yanayotesa kizazi baada ya kizazi. Kwa mfano ziko familia na Koo zinateswa na roho ya wizi unakuta hiyo roho inatembea toka kizazi hadi kizazi na watu wanauwawa kwasababu ni wezi au kufungwa magerezani ukishaona hivyo ujue kwamba kwenye Malango ya Familia na Ukoo huo yanapitisha roho ya wizi.
Kwanini kwenye familia na ukoo wenu watu wanaolewa na kuachika? Au kuoa na kuacha wake? Kuanzia kwa mababu na mabibi mpaka kwenu Leo, ukiona hivyo ujue kwamba kwenye malango ya familia na ukoo wenu yanapitisha hiyo roho ya kuoa na kuacha au kuolewa na kuachika.
Familia nyingine na koo nyingine huteswa na roho ya kuoa wake zaidi ya mmoja au kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja nahata waliookoka wanateswa na hiyo roho, ukiona hivyo ujue kwamba malango ya familia na Ukoo wenu yanapitisha hiyo roho.

Kwanini kwenye familia NA ukoo wenu mnaishia kidato cha NNE hakuna anayevuka hapo? Ukiona hivyo ujue kwamba kwenye malango ya familia na ukoo wenu yanapitisha roho ya kuishia kidato hicho na huvuki hapo hata kama unataka kwenda mbele.
Familia na koo nyingine hao watu kila wanachoanzisha na kukifanya kinakufa hakiendelei nawewe unapata shida hiyohiyo unaanzisha biashara au mifugo na inakufa tu, ukiona hiyo ujue kwamba malango ya familia na ukoo wenu yanapitisha hiyo roho.

Familia na koo nyingine wanafanya biashara lakini hakuna anayevuka kuingiza faida kiasi Fulani pamoja na kujitahidi sana kufanya biashara. Au wengine wameajiliwa makazini lakini wako na kiwango kinachofanana cha mshahara.
Wengine wanateswa na roho ya kufukuzwa kazi pasipo sababu za msingi na wengine wanateswa na roho za ulevi au kuuana au kulogana au roho za magonjwà mbalimbali n.k

Je wewe kwenye malango yenu ya familia na Ukoo yanapitisha roho gani ambayo inakutesa na kukusumbua? Au kuwatesa ndugu zako?
Katika sehemu ya tano nitakueleza malango mengine NA roho zinazopita hapo.

Jambo la kufanya kwenye hayo malango ya familia na ukoo wenu niwewe kwenda mbele za MUNGU kwa maombi ya toba kutubia dhambi na uovu wa familia na ukoo kisha iachilie Damu ya Yesu kristo ipite kwenye hayo malango na funga hizo roho zinazowatesa kwa kutumia Jina la Yesu Kristo.


SHEHEMU YA NNE:

BAADHI YA MALANGO YA KIROHO NA VITU VINAVYOPITA HAPO LANGONI.
Baada ya kukueleza lango la kwanza kuwa dhambi inapita malangoni hebu tuendelee mbele.

2.( Lango linalopitisha roho ya Utasa ).
Kwenye familia ya Ibrahimu kulikuwa na Lango ambalo linapitisha roho ya utasa kwenye hiyo familia toka Ibrahimu na mtoto wake na mjukuu wake.
MWANZO11:27-32
Utaona Biblia ikiweka wazi kwamba Sarai MKE wa Ibrahimu alikuwa tasa.
MWANZO 25:21
Unamkuta mtoto wa Ibrahimu aitwaye Isacka naye MKE wake Rebeca alikuwa tasa.
MWANZO 29:31
Unamkuta Yakobo mjukuu wa Ibrahimu naye MKE wake Raheli alikuwa tasa.
Sasa hii roho ya utasa ilikuwa inapita kwenye malango ya familia ya Ibrahimu na walipomuomba MUNGU kuhusu utasa wa wake zao MUNGU aliwafungua matumbo nao wakazaa watoto.

Je wewe kwenye familia yenu au ukoo wenu kuna vitu gani huwafuatilia toka kizazi hadi kizazi? Wengine wameokoka ila bado wanafuatwa na vitu vya kurithi hii ikiwa na maana kwamba kuna malango kiroho yanayopitisha vitu hivyo au roho hizo.
3.( Kuna malango ya Mauti na malango ya Kuzimu ).
Hili nalo nilango ambalo limeua watu wengi sana kabla ya wakati wake. Wako watu ambao ni ndugu zetu hata wazazi wetu tumewazika makaburini lakini sio kwamba muda wao wa kufa umefika hapana wengine nikweli muda wao umefika, ila wengine ni malango ya mauti na kuzimu yamewaua kabla ya wakati wao.
Hebu tusome AYUBU 38:17 Inasema "Je umefunuliwa malango ya Mauti? Au umeyaona malango ya Kuzimu?. Haya malango hufanya kazi pamoja yaani kwamba lango la mauti likimuua mtu huwa lango la kuzimu linampokea.
ISAYA 28:15,18 Inasema "Kwasababu mmesema, Tumefanya Agano na Mauti, tumepatana na Kuzimu......Na Agano lenu mliloagana na Mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na Kuzimu hayatasimama...."
Hapa tunaona kwamba kuna watu huwa wanafanya agano na mauti ili mtu afe pia wanapatana na kuzimu.

Ngoja nikueleze Rafiki yangu viko vifo vingi sana ambavyo hutokea kwa watu mfano: ajali, mafuriko, kujinyonga, majanga ya moto, n.k hutokea kumbe ni malango ya mauti yanaua watu.
MATHAYO 16:18
Utaona Bwana Yesu akisema kuwa malango ya Kuzimu hayatalishinda kanisa.
Haya malango ya kuzimu na mauti yakifanya kazi ndani ya familia au ukoo utaona jinsi watu wanavyokufa bila sababu za msingi. Unaweza kumkuta Mtu alikuwa mzima ghafula anaumwa na mkimkimbiza hospitali wanasema hana maji au damu imepungua, au presha imepanda au kushuka n.k na baada ya muda anakufa,
Nyie mnafikiri kuwa huo ugonjwa ndio uliomuua kumbe ni malango ya mauti na kuzimu ndio yamemuua kwa siri kupitia huo ugonjwa.

Nataka niseme tu wazi kwamba Vifo Vingi sana vinavyotokea wala MUNGU Baba hahusiki ila watu wengi wanauawa na malango ya mauti na wakifa wanaenda kuzimu.Unaweza ukawa unatembea kumbe nyuma yako malango ya mauti na kuzimu yanakufuata kwa siri ili kukuua au kuua mtoto wako au mzazi wako.
ZABURI 102:20 Inasema "Ili akusikie kuugua kwake, aliyefungwa, na kuwafungua walioandikiwa kufa". Umeona hapa Biblia inasema kuna watu wamefungwa Na kuandikiwa kufa.
Wako watu wanatembea duniani lakini tayari wako na nembo ya mauti. Je wewe haujawekewa nembo ya kufa bila kujua?. Malango haya ya mauti yameua ndoa za watu wengi sana mpaka wameachana, yameua mahusiano ya uchumba wa vijana, yameoa mahusiano kati ya wazazi na watoto wao na kuwafanya waishi kwa ugomvi, yameua ndoto za maisha ya watu, kuua biashara na mitaji ya watu n.k

Nimalize kwa kusema hivi je kwenye familia na ukoo wenu hakuna malango ya mauti na kuzimu yanayotenda kazi? Je unapotembea na kuishi kwako malango ya mauti na kuzimu hayakufuati kwa siri ili yaweze kukuua? Je nimaeneo gani ya maisha yako au maisha yenu ambayo malango ya mauti yanatenda kazi?
Je hakuna watu ambao wamepatana na malango ya mauti na kuzimu kwa ajili yako au ndugu zako au watoto wako?
Je huyo ndugu yako anayeumwa sasa hivi sio kuwa ni malango ya mauti na kuzimu yamejificha nyuma ya ugonjwa huo ili yamuue na kumpeleka kuzimu? Nanyie mnakazana tu kumpeleka hospitali moja baada ya nyingine bila kuingia kwenye maombi ya ndani sana.

Nitaendelea kukueleza malango mengine katika sehemu inayofuata usikose pia mkaribishe na rafiki yako
Kwa ushauri na maombezi wasiliana nami kwa simu hii +255 765 867574
KUMBUKA MAISHA BILA YESU NI SAWA NA KUENDESHA GARI KWENYE GIZA TOTORO BILA TAA. KAMA HUJAOKOKA LEO HII OKOKA MKARIBISHE BWANA YESU MOYONI MWAKO
MUNGU BABA AKUBARIKI

Comments