JIFUNZE KUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA.


Mch.Madumla.
Na mchungaji Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Ifike wakati ujifunze kumpa BWANA MUNGU nafasi ya kwanza kwa kila hatua katika maisha yako. Kwa maana zipo faida nyingi mno za kumtanguliza Mungu katika yale yote uyafanyayo.Kumbuka ya kwamba;hakuna aliyemtanguliza Bwana Mungu katika mambo yake na akapata hasara.
Kuna mambo magumu unayoyapitia hivi sasa ni kwa sababu hukutaka kuenda na Mungu katika safari yako ya maisha. Laiti kama ungempa BWANA Mungu nafasi ya kwanza basi ni dhahiri yasingelikuwepo mapito hayo yote,la hata kama yatakuja lakini hayatakugalikisha (Zab.2:4).
 Kumbuka hili,mateso mengine huja kwa sababu umemuacha Mungu. Laiti Bwana angelikuwa upande wako,angelikupigania(Zab.118:5-7)
Mtangulize MUNGU kwanza kwa kila ulifanyalo. Mfano, unataka kuanzisha biashara basi anza na Bwana. Ikabidhi biashara yako kwa Bwana Mungu kabla ya kufanya chochote kile. Mfano tena;labda kijana wako anaanza shule,basi mkabizishe kwa Bwana Mungu. Labda unataka kujenga na umeanza na kuwa na wazo hilo,basi anza na Mungu akupe wepesi wa ujenzi lakini pia akulinde.
Ukiingia ofisini kwako,anza na BWANA mkabidhi ofisi hiyo na umwambie akuongoze namna ya kufanya kazi kwa usahihi. Hata ukiwa umeingiza hasara badala ya faida kabla ya kuangalia tatizo basi mtazame Mungu,anza na Bwana akupe njia ya utatuzi Yeye ni Mungu anaweza mambo yote.
Ukiwa umefiwa,anza na Bwana~sababu Yeye Mungu atakuongoza katika kipindi hicho,atakupa wepesi wa kumaliza msiba,atakufariji na kukulinda. Labda yawezekana unaumwa basi wewe katika ugonjwa huo huo kila hatua anza na Bwana.
Ukiwa shuleni,mpe Mungu nafasi ya kwanza~mkabizi masomo yako,mkabizi uelewa wako Yeye akusaidie. Na hakika ukiweza kumtengea muda wako kisha ukaomba,ukasoma neno lake hapo utafaulu katika viwango vya juu mno,kisha Bwana atakuwa upande wako.
Mimi ninamshangaa mtu yule afanyaye mambo yake yeye mwenyewe kana kwamba Mungu hayupo. Utakuta mtu kaamka,hajaomba! Alafu anaenda kazini,nako haombi? Akirudi anaendelea na mambo yake akimaliza huenda kwenye TV~anaangalia stesheni zote hata zile ambazo hazimuhusu,kisha anaenda kujitupa kitandani wala haombi ndivyo amalizavyo siku yake pasipo kuomba kabisaa!!!
Au utakuta mtu bado hakufanikiwa kupata kazi maalum,basi yeye kutwa ni kufanya mambo yake tuu pasipo hata kumtanguliza Mungu Yeye awezaye kumpea kazi nzuri.
Sasa ninakupa siri hii;Ukitaka wepesi wa kushinda yale yote uyapitiayo katika maisha yako,wewe mpe Mungu nafasi ya kwanza kisha utaona mambo yako yatakavyokuwa.
Mch.Madumla.
Gasper Madumla
Yawezekana hujui utaanzaje kumpa BWANA MUNGU nafasi ya kwanza katika yale uyanyayo. Au tena inawezekana ikawa umejaribu mara nyingi kumtanguliza Mungu katika mambo yako lakini inafika wakati unarudi nyuma na kukata tamaa. Ninaomba niombe na wewe leo; nipigie sasa kwa +255 655 11 11 49.
Mch.Gasper Madumla.
Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)
UBARIKIWE.

Comments