KUMTUPA NJE MKUU WA ULIMWENGU

 
Na:     STEVEN NAMPUNJU (RP)
& DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi: Dunia na vyote vilivyomo ndani yake vinaunda kitu kiitwacho ‘Ulimwengu’. Mkuu wa ulimwengu huu ni yule mwenye madaraka juu ya ulimwengu huu: upate nini; uishi vipi; ule nini‼!; n.k. Huyo  ndiye mwenye mamlaka ya kuamua usome wapi, ule nini, uishi vipi‼. Kumbuka Mungu anaheshimu mamlaka. Zipo mamlaka zimewekwa lakini zinasimamia matatizo ya watu. Kwenye YOHANA 12:31 imeandikwa…[Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.]…Na pia imeandikwa katika 2KORITNHO 4:4… [ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.]….Yupo ‘mungu’ wa dunia hii, anayeweza kupofusha fikra za watu. Huyu tena anayo mamlaka.
Kwenye LUKA 4:1-12 Yesu alikuwa anajaribiwa. Imeandikwa [Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. 4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. 5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. 9 Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.]…. Huyu mwenye mamlaka anamwambia Yesu mambo haya. Huyu anayetoa kwa wale anaopenda leo ni siku ya kumkamata na kufutilia mbali  kwa Jina la Yesu. Kutokana na  uhitaji  wa mtu, mkuu wa ulimwengu  huu anayo majina mengi. Mungu wetu anaitwa “Nipo ambaye nipo”. Kwamba ukiwa na kiu, yeye Mungu ni kisima cha maji ya uzima, ukiwa na njaa yeye ni chakula cha uzima
Majina ya mkuu wa ulimwengu huu nayo ni mengi pia; Mifano ya majina yake nikama vile:-

1.      NYOKA WA ZAMANI: kama  ilivyoandikwa katika UFUNUO 12:7..[Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;]… Yesu pia anafananishwa na nyoka wa shaba aliyeinuliwa  jangwani kipindi kile  cha Musa.
2.      BABA WA UWONGO:  Imeandikwa katika YOHANA 8:41-43...[Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. 42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. 43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu. 44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo;    wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.]…. Endapo yupo mtu asiyetaka kumsikiliza Yesu Krsito, maana yake siyo wa uzao wa Ibrahimu.
3.      MWIZI: Imeandikwakatika YOHANA 10:10…[Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.]… Mkuu  wa ulimwengu hapa anaitwa mwizi kutokana na kazi ya wizi anayoifanya.
4.      MUUAJI  TOKA MWANZO: Imeasndikwa 1YOHANA 3:8-12…[atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. 11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.]… Muasisi wa mauaji ni shetani ambaye ndiye mkuu wa ulimwengu huu.
5.      MSHTAKI WA NDUGU: Imeandikwa katika UFUNUO 12:10…[Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.]… Mkuu wa ulimwengu huu unamtambua kutokana na kazi zake. Ili uweze kuzishiinda hila za ibilisi nikuzijua hila zake. Imeandikwa katika MAOMBOLEZO  3:31-33…[Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.]…. Siyo kusudi la Bwana kumhuzunisha mtu yeyote. Uonapo huzuni au mateso  yameandama maisha yako, usimhusihse Mungu bali ujue huo ni mpango  wa Mkuu wa Ulimwengu huu (shetani).
UMUHIMU WA KUMTUPA NJE MKUU WA ULIMWENGU
·        AMESHIKA VIPAWA NA KUZUIA HATIMA YA MTU: Mfano wa kwanza: MARKO 5:1-10…[Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. 2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, a kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.]….  Mkuu wa ulimwengu huu hupaenda kuzuia watu wasivae nguo. Uonapo watu wanavaa nguo fupi sana, na pengine za nusu uchi, ujue mkuu wa ulimwengu huu yupo kazini. Kumbe uonapo mtu hakai  nyumbani, ni kazi za mkuu wa ulimwengu huu. Huyu  kijana alipaswa awe mhubiri  wa injili lakini mkuu wa ulimwengu huu akamzuia ili  asiione nuru ya injili maishani mwake. Aliyepaswa afanikiwe anarudi  nyuma.
UKIRI
Ewe mkuu wa ulimwengu uliyenizuia nisifanikiwe, leo kwa Jina la Yesu nakukataa,  ninakutupa nje, ewe mkuu wa ulimwengu huu, achia maisha yangu katika Jina la Yesu. Amen
·        ANAWEZA KUKUZUIA: 1 YOHANA 3:8… [atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.]… Yesu alikuja duniani ili kuvunja kazi za ibilisi. Wapo watu ambao wanayo mamlaka juu ya maisha yako.  Mwenye mamlaka huyu anaweza kuzuia uinuke kwa kiwango  gani,  au uwe mtu  wa aina gani‼
·        ANAWEZA KUTUMIA CHOCHOTE: Mkuu wa ulimwengu huu anaweza kutumia wanyama au vitu (mfano: paka, panya, nazi n.k.). Yesu pia aliwahi kutumia mamlaka yake kuwatuma Petro Baharini wakavue samaki, na ndani ya samaki yule wa kwanza akawaambia wataokota humo fedha itakayotosha kulipia kodi kwa Petro na Yesu.
UKIRI
Ninashinda kazi zako, na utawala wako kwa Damu ya Yesu, niachie katika Jina la Yesu. Amen
Yamkini  wewe unanga’ng’ania kuolewa au kupata kazi kumbe wakati hup huo hujamtoa nje mkuu wa ulimwengu huu anayekuzuia usivipate hivi vyote.
Imeandikwa katika YOHANA 14:30..[Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.]… Ewe Mkuu wa Ulimwengu huu,  huna kitu kwangu.  Leo  ninakunyang’anya vyote vinavyonihusu katika  Jina la Yesu.
Leo tuiambie bahari iliyokamata fedha zetu/ afya zetu/ndoa zetu/biashara zetu, iachie kwa Jina la Yesu. Leo tuilazimishe bahari iliyomeza samaki ambao ndani yao kuna fedha na vitu vyetu,  iachie kwa Jina la Yesu. 
Ili upate itategemea ukaribu wako na mwenye mamlaka. Ili ufanikiwe sana, inabidi  uunde ukaribu sana na mwenye mamlaka. Maana yake, ukaribu wako na mwenye mamlaka  utakufanya upate unachokitaka. Maana yake, ukiwa karibu sana na Mungu au ukijenga ukaribu wako na shetani ndivyo utakavyopata unavyotaka kutoka kwa mwenye  mamlaka husika. Wakati mwingine mchawi mmoja anaweza kumuumbua mchawi mwingine,na hii  ni kutokana na ukaribu alio nao  na yule mwenye mamlaka (kwa jinsi anavyotoa kafara kubwa n.k).  
Mkuu wa ulimwengu huu  lazima atupwe nje. Shetani  hahitaji  majadiliano kama ya wanasiasa, hapana! Shetani anapigwa tu‼ Mkuu wa Ulimwengu huu ana uwezo wakubadilisha tabia. Pengine ulikuwa na mume, leo hii humpendi tena.
UKIRI
Katika Jina la Yesu, Imeandikwa “nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kazi zote za  yule muovu wala hazitanidhuru”, wewe mkuu wa ulimwengu ninakutupa  nje kwa Jina la Yesu. Amen.

Haipaswi mtu kuwa vuguvugu. Siri kubwa ni kumgeukia Yesu Kristo, kwa kuwa mkuu wa ulimwengu huu  hana kitu kwetu. Leo wewe ambaye hujaokoka ni wakati mzuri ukafanya maamuzi ya kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako kwa kuokoka.

Comments