KUNA MWONGOZO WOWOTE KATIKA KUOMBA JINSI YA KUPATA KAZI? MAANA NATAFUTA KAZI.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze somo hili ambalo chanzo chake niliulizwa swali na ndugu mmoja.

Ndugu huyo anaanza kwa kusema.
Nina swali mtumishi Peter Mabula, hivi Kuna mwongozo wowote katika kuomba jinsi ya kupata kazi maana natafuta kazi ? Ubarikiwe

Majibu yangu kwa nfugu huyo yalikuwa kama ifuatavyo, hivyo nakuomba na wewe ujifunze kitu kupitia majibu haya.



 Ubarikiwe sana kwa swali lako na naamini utapata majibu yatakayokupa baraka hiyo ya kazi uitakayo.
Mwongozo wa maombi yanayojibiwa ni mmmoja tu.
=Mwongozo wa maombi ili kupata kazi ni kumpa YESU maisha yako ili upate kibali cha kupokea.

Mithali 18:10 '' Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama. '

=baada ya hapo tubu toba ya kweli 
Isaya 55:6-9 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.   ''

 =baada ya hapo omba kwa imani katika KRISTO.
 Waebrania 11:1,6 ''Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.''

 =Baada ya hapo ni omba bila kukoma yaani omba hadi upokee baraka yako. 
 1 Thesalonike 5:17 ''ombeni bila kukoma;''

=Jambo jingine la kutambua ni kwamba MENGINE HAYAWEZEKANI ILA KWA KUFUNGA NA KUOMBA.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga. ''

Hata hivyo yote hapo juu yaambatane na SHUKRANI kwa MUNGU 
Wakolosai 4:2 ''Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; ''

 =Pia tambua kwamba kumzalia BWANA matunda ni jambo la muhimu sana kwa anayehitaji kupokea kwa BWANA 

Yohana 15:16 ''Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni.''

 MUNGU akubariki sana ila tambua pia kwamba kuna kazi ambazo  zinaweza kuwa ni chanzo cha wewe kutenda dhambi na kumkosea MUNGU wako. au kazi yenyewe ikawa ni kazi ya dhambi. 
Hivyo ni ngumu MUNGU kukupa kazi hiyo maana haimuhusu hata kidogo.
Mfano unaomba kazi kampuni ya pombe, hata ukipata kazi hiyo ni kwa matakwa ya shetani na sio MUNGU.
MUNGU akubariki na hakika utapokea kazi nzuri kwa jina la YESU KRISTO omba kwa maelekezo hayo na mimi nitakuombea pia maana kwa BWANA YESU ni uhakika kupokea. 
 MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
 Warumi 8:26-27 ''Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo MUNGU.''
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments