MAOMBI YA MWINGIRA KWA KANISA LA EFATHA.

Na Mtume na Nabii Josephat Mwingira
Hii inatoka katika sehemu tu kidogo ya Mafundisho ya Mtume na Nabii Josephat Mwingira katika maombi kwa kanisa wakati wa kumaliza mwaka 2015 na kujiandaa kuinga mwaka 2016.

 "Maombi siyo kwamba yanafanya MUNGU Akusikilize, bali ni UELEWA WAKO ndio unaofanya MUNGU Akusikilize...........UNAELEWA Nini Wewe?"

1) Ngoa na haribu kabisa kila kinachozui Kanisa lising'ae na kuonyesha utukufu ule ambao BWANA ALIUKUSUDIA.

-Ondoa kila kinachozuia mng'ao wako, pingana nacho lazima ungae, mng'ao wako ndio mng'ao wa Kanisa. Acha watu wakikuona wamuone YESU.
-Ng'oa kila kinachoondoa na kuchafua mng'ao wako.


 2) Angamiza kwa nguvu zake aliye juu kila kilichosimama kati yako na watu ambao MUNGU amewakusudia kuja Efatha kupitia wewe.
-Wako watu ambao MUNGU ameruhusu wamjue yeye kupitia wewe, angamiza kila kilichosimama kati yako na hao watu, tumeamriwa kuzaa matunda.
-Sema BWANA YESU nimeangamiza na nitaendelea kuangamiza kila kinachosimama kati ya Efatha na wale waliokusudiwa kuja Efatha.


 3) Ondoa kila giza na utando unaolizunguka Kanisa na watu wake.
-Ondoa utando na giza kwako KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI, Ibrahimu alitaka kumchinja mwanae ISAKA lakini BWANA alipoondoa utando alimwona kondoo.

-BWANA waondolee watu wako giza na utando wakaone yale uliyo wakusudia. Sema BABA ondoa giza mbele yangu, ukiondoa giza na utando sitakuwa mtu wa kawaida.

 Naachilia nguvu ya kuondoa giza na utando ipite mbele yako iondoe kila giza na utando mbele yako. Lazima tung'ae, lazima tuwe bora, Efatha lazima ingae maana ni Kanisa lako linaloandaa watu kwa ajili ya unyakuo.
 Lazima uingie mwaka mpya huku unang'aa, maombi haya utayaomba mwezi mzima ukiwa njiani, nyumbani na popote utakapokuwa ng'ang'ana nayo, angamiza na haribu usimwache adui akakukanyaga, ni lazima ung'ae.

 Kuanzia leo nakuagiza ukang'ae na usipoteze mng'ao wako. Pokea mng'ao wako, ng'aa ofisini, barabarani, kariakoo na Mikoa yote ng'ara KWA JINA LA YESU.


Sema nina ng'ara, utang'ara asubuhi, utang'ara mchana, utang'ara jioni na ukilala utang'ara, wachawi, majini na dhambi wataona mwanga wako watakimbia. Utukufu utakujia na mema yatakujia. Kuanzia leo nakuoachia upako wa kungara.

Comments