MASAIDIANO

Na Frank P. Seth

"Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye. Visiwa vimeona, vikaogopa; ncha za dunia zilitetemeka; walikaribia, walikuja. Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu. Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike" (Isaya 41:4-7).
Duniani hakuna mmoja awezaye kusema, "sasa nina kila kitu wala sihitaji msaada wa mtu". Tajiri na masikini, wote tunahitajiana ili kufanikiwa katika mambo yetu. Kweli, hata ukamilifu wa dahari hatakuwepo mmoja asiyemhitaji mwingine ili kufanikisha mambo ya kimaisha. 

Tazama makundi haya, kuna tufauti ya kati ya "mtu tegemezi" na "mtu afanyaye kazi na wengine kwa masilahi ya wote au wengine". Kundi la kwanza, sifa yake kubwa ni LAWAMA. Yani mtu anaona AMESTAHILI kusaidiwa na MTU fulani, tena asipopata msaada ni ugomvi. Sawa, kuna wajibu wa mzazi kwa mtoto, mke na mume kila mmoja kwa mwenzake, ndugu na ndugu, nk. Tazama, ni nani unamtanguliza katika KUFANIKIWA kwako? Je! Tegemeo lako ni nani? Kama tegemeo lako ni MTU na sio MUNGU, shida yako ni mkubwa kwa maana kila mwanadamu akipungua wewe hutaacha kulaumu na kulalamika tu, yamkini hata kulaani; eti, hujasaidiwa jinsi unavyotaka!

Sasa angalia jambo hili, Je! Unauza ili upate faida mara dufu au zaidi? Je! wewe ni MLANGUZI? Je! Unatumia mizani isiyo sahihi kwa sababu uwauziao HAWAJUI? Je! Ni haki ufanyavyo (ukifanya hivyo nafisi mwako unasikia nini)? Kumbuka, siku zote, jambo la kwanza katika mambo yote ni KUSAIDIANA na wengine ili kama ukiweza, yamkini uwape UHERI katika maisha yao. Japo unauza, au unafanya wajibu wako, kwanini UUMIZE wengine?

Jambo jingine, kama huwezi kumsaidia mwingine kwa VITU au NGUVU zako, basi mpe neno la kumtia moyo ili asonge mbele asikate tamaa. Bila shaka neno la faraja na kutia moyo lina huisha kama kilkivyo chakula wakati wa njaa. Sema tu, tia moyo tu, ikiwezekana, toa tu, hutapungukiwa.
Frank P. Seth

Comments