
Na:
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
STEVEN
NAMPUNJU(RP), UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi
wa Somo: matukio ya Kichawi ni matukio yanayotokea kufuatana
na uchawi kuhusishwa. Duniani leo, zipo nguvu nyingi za giza zinazotumiwa na
wanadamu, na nguvu hizo ni UCHAWI.
Malengo ya wachawi au wanadamu kutumia
uchawi ni:
·
Kuwaumiza watu wengine kimazingara
·
Watu wengine hutumia uchawi ili
kujilinda
·
Wengine tu huutumia uchawi kwa ajili ya
kujifurahisha. Hawa ni wale ambao wakiwatesa watu wengine hufurahia kuona
mateso yale. Yesu alisema, “furaha yangu ni kuona mapeznzi ya Baba yangu yanatimia”.
Upande wa shetani wao hufurahi kuona mabaya yakitokea.
·
Wengine hutumia uchawi kwa ajili ya
kufanya miujiza /mazingaumbwe n.k.
Imeandikwa katika HESABU 23:23…[Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli.
Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda
Mungu!]…. Inamaanisha kuwa,
endapo uchawi haupo, basi mtu anaweza kufanya jambo nalo likafanikiwa.
Wachawi huwa na mawasiliano ya karibu na roho za
mashetani.
Katika Biblia wapo amaboa waliwahi kutengenezewa
matukio:
Mfano
1:
MATHAYO 9:32-34…[Hata hao walipokuwa wakitoka,
tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. 33 Na pepo alipotolewa, yule bubu
alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli
wakati wo wote. 34 Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa
pepo.]… Hapa Yesu anamsaidia mtu bubu ambaye madaktari na familia
yake walikuwa na taarifa tofauti ambayo Yesu aliibadilisha historia na taarifa
hizo kuwa uponyaji wa kudumu. Yamkini hata wewe kwenye ukoo wako yapo mambo
ambayo mnayazoea kama yahusuyo ukoo wenu. Ukimwamini Yesu atabadili historia
yako.
Mfano
2:
MARKO 9:14-18…[Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu
wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; 15 mara mkutano wote walipomwona
walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. 16 Akawauliza, Mnajadiliana nini
nao? 17 Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako,
ana pepo bubu; 18 na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga
meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.]…
Mzazi wa huyu kijana alipogundua matatizo ya mwanae, alijua kuwa ni pepo na kwamba
matukio haya ni ya kutengenenezwa. Kitendo
chake cha kumwaamini Yesu
kilimfanya amlete huyu mwanae kwa Yesu.
Matukio ya
huyu kijana (mfano wa 2) ni ya kubwagwa chini‼: Kwamba akiwa kitandani, mapepo yakimpanda
yanambwaga chini. Kwamba angekuwa yupo kwenye ndoa baadae anabwagwa chini
(kuachika). Tukio lingine ni kukonda. Unaweza kutumia virutubisho vyote
kwa mwanao lakini bado anaendelea kukonda tu.
Imeandikwa MARKO 9:19-21…[Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi
hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. 20 Wakamleta kwake;
hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini,
akagaagaa, akitokwa na povu. 21 Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini?
Akasema, Tangu utoto.]…Unaweza kuwa na matukio maishani unayoyaona kama ya kuzaliwa
nayo. Ukimwamini Yesu matukio kama haya
yanango’oka kwa Jina la Yesu. Hata kama taabu uliyo nayo ni ya miaka mingi,
itaondoka tu.
Imeandikwa MARKO
9:22-27…[Na mara nyingi
amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote,
utuhurumie, na kutusaidia. 23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake
aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie
kutokuamini kwangu. 25 Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio,
akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi
nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. 26 Akalia, akamtia kifafa sana,
akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. 27 Lakini Yesu
akamshika mkono akamwinua naye akasimama.]…Matukio yaliyofuatia
maombi ya Bwana Yesu ni: Kijana kutiwa kifafa sana, pepo akamtoka, akawa kama
amekufa.
Jamii yako
yaweza kuleta visa wanapokuona umeletwa kanisanai kuombewa. Wengine
watasema unaonekana kama umekufa. Hata biashara yako yaweza kuonekana kama
imekufa baada ya kuombewa. Wachawi wakitengeneza tukio baya la ubaya au mauti,
Mungu hulibadilisha na kuwa tukio jema la wokovu kwa Jina la Yesu.
Bwana ametutuma kutabiri uzima mahali pasipo na
uzima kwa Jina la Yesu. Ezekieli alioneshwa bonde lenye mifupa mikavu, na Bwana akamwambia aitabirie ile mifupa
ili iwe na uzima tena. Baada ya pale
ulitokea upepo ambao uliifanya ile mifupa kuingiwa na nyama na uzima tena kwa
ile mifupa.
HASARA
ZA MATUKIO YA KICHAWI KUWEPO:
1.
Matukio
haya juweza kuzuia kutajwa kwa habaari ya mtu fulani:-
Kivipi? Endapo ni ofisini, habari za mtu zinaweza kuzuiwa zisitajwe. Ni kama
mchujo vile unafanyika. HESABU 23:23….[Hakika hapana uchawi juu ya
Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli
zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!]…Matukio ya kichawi yakiondolewa, habari zako
zitasemwa. Sasa, habari zangu zitasemwa. Endapo uchawi na uganga vitaondolewa,
habari zako zitaanza kutangazwa na kusemwa.
2.
Matukio
ya kichawi huweza kumfanya mtu aache imani:- MATENDO 13:6-12.. [Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo,
wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu; 7 mtu
huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali
akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini
Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka
kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo,
akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na
uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana
zilizonyoka? 11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu,
usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na
kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. 12 Ndipo yule liwali, alipoyaona
yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.]…
Tukio la kichawi hushindana na hatimanzuri ya mtu. Wapo watu wameacha waume au
wake zao ichwai.
UKIRI
Achia
habari zangu kwa Jina la Yesu. Ewe silaha ya kuacha imani kwa nguvu za
kichawi, leo achia kwa Jina la Yesu. Aliyetengenezea
tukio kwa ajili ya misha yangu, nakataa kwa Jina la Yesu.
|
3.
Matukio
ya kichawihuweza kusbabisha magonjwa, hasasra na matatizo:
Utagundua kuwa matukio kama haya yakiwemokatikafamili,matatizo nayo huwa hayakosekani.
NJIA
IPI YA KUZISHINDA MATUKIO YA KICHAWI?
1.
Ili
uweze kushinda, njia nzuri ni
kumpokea Yesu Kristo maishani mwako. Imeandikwa katika YOHANA
1:12..[ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto
wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;]… kwa hiyo,unapokuwa
mwana wa Mungu, siyo rahisi kwa wachawi
na mawakala wao kukuletea matukio ya
magonjwa, au misiba au mikosi.
2.
Njia nyingine ni kuomba mwenyewe. Ni
vizuri uweze kuomba ukiwa mwenyewe, kwa sababu siyo mara zzote unaweza kuwa na wachungaji karibu na wewe kwa
ajiliya kukuombea unapopatwa na matukio ya kichawi.
Comments