MCHUNGAJI AISHI NA MALAIKA TANGU IJUMAA HADI JUMAPILI BILA KUMTAMBUA!

Wafanyakazi wa Huduma ya VHM

Ilikuwa siku ya Ijumaa mwezi fulani mwaka 2013, kijana mmoja smart alifika Nyumbani kwa Mchungaji mmoja mkoani Arusha. Huyo kijana alijitambulisha kuwa ameokoka, ni mwenyeji wa Dar es salaam ila amekuja Arusha kihuduma. Alimwomba Mchungaji nafasi ya kulala kwa siku atakazokuwepo Arusha, Mchungaji akakubali.
Katika maongezi, Mchungaji aliona kijana ana hekima sana na anajua sana Neno la Mungu. Siku ya Jumapili Mchungaji akamwomba afundishe somo kwenye kipindi cha Sunday school.
Kijana akiwa anafundisha, Kanisa lilitaharuki likiyastaajabia mafundisho yenye uzima toka kwa huyo Mwalimu/kijana. Mchungaji alikuwa amejiandaa kuhubiri, lakini kwa kile alichokiona kwenye Sunday school, akaghairi, akamwomba kijana asimame pia wakati wa Neno.
Wakati wa mahubiri pia alilishangaza Kanisa kwa jinsi Nguvu na Neema ya Mungu ilivyokuwa juu yake. Alipomaliza kuhubiri alimuuliza Mchungaji angetaka Mungu awafanyie nini. Mchungaji akasema wanahitaji jengo la kanisa kwa kuwa walilokuwa nalo lilikuwa duni. Kijana akasema, "Mwamini Mungu, mwezi ujao tarehe kama ya leo, mipango ya ujenzi itaanza." Baada ya ibada, kijana akaaga, akabeba begi lake akaondoka.
Kabla mwezi ule haujaisha, Watumishi wa huduma ya The Voice of Hope Ministry (VHM), inayoongozwa na Mchungaji Peter Mitimingi, walifika Arusha wakaweka kambi kwenye kanisa hilo. Hao watumishi huduma yao ni kuyafikia maeneo magumu kwa Injili, pia huwa wanakusanya sadaka kwa ajili ya kuwasaidia wanaookoka pamoja na Wachungaji vijijini.
Siku ile aliyoisema yule kijana ilipofika, Mchungaji Mitimingi alikwenda kuongea na Mchungaji mwenyeji kuhusu jengo la Kanisa. Mchungaji Mitimingi akamwambia kuwa VHM wameona vyema wawajengee jengo jipya na mipango ya ujenzi ianze siku hiyo!
Mchungaji mwenyeji aliuliza kama yule kijana aliyekuja mwezi uliopita iwapo alikuwa mwenzao. Mchungaji Mitimingi akasema hawakuwahi kutuma mtu kabla na yule kijana hawamjui!
Ndipo wakashangaa wote, wakatambua kumbe yule kijana alikuwa Malaika wa Mungu!

Comments