MSIJE MKACHUKIZWA

Na Mtumishi Lusajo Brown



Tusome pamoja....
Yohane 16
1 Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.

Karibu tujifunze juu ya unabii huu ambao Yesu aliwaambia wanafunzi wake.
Sababu kubwa ya unabii wowote ule ni kwamba unataarifiwa juu ya mambo hilo ili uanze kujiandaa ama kuchukua hatua kwa ajili ya jambo hilo.
Basi katika unabii huu Yesu anasema ametuambia ili tusijetukachukizwa, kama sivyo tuwaombee na kuendelea kuwahubiri injiri ya kweli.
Saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa amtolea Mungu ibada.
Nadhani jambo hili hakuna aliye mgeni nalo kwamba kuna watu katika dini yao wanapomuua mtu wa imani tofauti na yao anapapata thawabu kwa Mungu wao.
Jambo la kujiuliza ni Mungu yupi anayeelekeza kuua ili mtu abarikiwe?

MUNGU wetu wa mbinguni aliye mtakatifu yeye anaagiza ili mtu apate kufanikiwa katika njia zake anapaswa kuliweka Neno ama maagizo ya Mungu moyoni mwake asiende kulia wala kushoto.
Kumbe sasa wayafanyayo hayo ni wazi kwamba hawakumjua Baba wala Yesu Kristo hivyo ni wana wa uasi yaani Mpinga Kristo.
Jambo hili lilianza miaka ya 300 BK baada ya wale mitume na wanafunzi wa kwanza kuwa wameuawa baada ya kazi kubwa ya kuhuburi injiri na mhusika mkubwa akiwa ni himaya ya Rumi kwa nyakati hizo na baadae sasa kuibukia Babeli ambaye ni mama wa uasi kutoka nyakati za nyuma huko ukiangali historia ya mfalme Nebukadneza. Huko ndiko chimbuko ya dini zote za kuabudu sanamu kama wahindu budha na uislamu wenyewe. Kwa hiyo ulifanyika ukatili wa ajabu sana juu ya wakristo kwa kuwalizimisha kuikana imani la sivyo wangeuawa, kwa hiyo waliuawa watu wengi sana nyakati hizo, kitu ambacho kiliiwezesha dini hii kuenea kwa kasi katika maeneo ambayo tayari yalikuwa na ukristo lakini chimbuko lake ikiwa ni Babeli ambayo ni Iraq kwa sasa,
Kwa hiyo kwa wale wasomaji wa Biblia kama wanaijua historia ya Babeli. Watakuwa wanaelewa hiki ninachokisema.
Kwa hiyo Hao ni wapinga Kristo maana Babeli haikumjua Mungu na sasa hawamjui Yesu na wala hawataki kusikia habari zake. Kanda hiyo ya mashariki ya kati ni kanda ambayo iko kinyume kabisa na ukristo kiasi cha mtu akionekana ameokoka. anawekwa hadharani na kuuwawa.

Cha msingi wapendwa ni kuwaombea tu na kuzidi kuwahubiria injiri ya kweli wapate kuokoka.
Anangalia maneno haya ya Yesu.
Yohane 10
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Hitaji la Mungu kwa mwanadamu awe na uzima wa milele tena awe nao tele.
Tuwaombee hao.
Mungu akubariki.

Comments