Na Mtumishi Peter Mabula. |
Ndugu huyu alianiandikia hivi;
Hallo Peter Mabula mtumishi wa MUNGU.
kwanza namshukuru MUNGU kwa kuyapitia mafundisho yako, kwani kwa muda mrefu nimekuwa nikifikiria njia ya
kuacha uzinzi kwani sioni FAIDA yake lakini kila nikijitahidi kuacha najikuta nimetumbukia tena na moyo unaniuma sana kwani nilikuwa
NIMEOKOKA na kwa kweli nilikuwa na matamanio mkubwa ya kumtumikia
Mungu na sasa hayapo kabisa na kwa kweli uvivu katika kumtafuta Mungu mara kwa mara umenifanya nirudi nyuma na kila nkijitahidi kusimama najikuta narudi nyuma kweli inaniumiza
Imefika mahali nimekata tamaa kabisa hata ya kwenda kanisani na hata nikitamani kwenda kanisani nakuta moyo unanirudisha ;
Na isitoshe kila nikifikiria maovu niliyomtenda Mungu naona kabisa kama sina nafasi kwake, kwa mtu niliyemjua na kuanza kutenda maovu mabaya ingawa natamani sana nirudi kwake
Na mbaya zaidi kweli wakati mwingine nimekuwa nikiomba maombi kwa watumishi wa MUNGU kuomba sala ya toba lakini najikuta narudi tena kulekule hivyo naona kama namtania Mungu na kuingia kanisani nkiwa mwenye dhambi naona kama kumfanyia masihara muumba naomba ushuri wako.
Baada ya mimi Peter Kuusoma ujumbe wa ndugu huyo hapo juu nilimjibu na kuahidi kuanza kumuombea. Majibu yangu hayo nataka yakusaidie na wewe ili umpokee BWANA YESU na kusimama imara katika wokovu wa BWANA.
Majibu yangu ni haya;
ubarikiwe kwa kunieleza siri yako inayokutesa kwa muda mrefu.
Naomba nikushauri kama ifuatavyo;
Kuacha dhambi kwa mtu yeyote huja baada ya mtu huyo kuamua kuipenda mbingu badala ya jehanamu.Naomba nikushauri kama ifuatavyo;
''Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.-Ufunuo 20:15''
Nakuomba kama hilo kanisa ambalo uliokokea mwanzo liko karibu basi muone mchungaji na mweleze kisha atakuongoza sala ya toba na utaanza upya na BWANA YESU.
''Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.-Yakobo 5:16 ''
''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.-Warumi 10:9-11''
Yohana 3:18-21 '' Amwaminiye yeye(YESU) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.''
dhambi ni mbaya kuliko sumu maana dhambi inaweza kuzaa jehanamu hivyo kama tunaiogopa sumu kwenye chakula basi tuogope na dhambi kwa namna hiyo hiyo maana dhambi ina madhara makubwa sana zaidi ya sumu.
8. Sahau mambo ya nyuma na yafute kabisa kwenye akili yako ili yasikufanye ukose ujasiri wa kuendelea mbele.
9. Hakikisha unakuwa kielelezo cha matendo mema.
10. Liishi Neno la MUNGU siku zote.
Mathayo 13:41-43 '' Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa BABA yao. Mwenye masikio, na asikie.
''Ndio maana Biblia siku zote inatushauri kwamba
''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;-Matendo 3:19''
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.
Comments