PETER MABULA :USHUHUDA WANGU WA INJILI MWAKA HUU.



BWANA YESU atukuzwe.
Zaburi 9:1-2 '' Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu.''


Namshukuru MUNGU Mwenyezi kwa uzima alionipa.
Namshkuru BWANA YESU maana alinipenda na akanichagua kumtumikia.
Namshukuru ROHO MTAKATIFU maana hunifundisha na kunielekeza na kunisahihisha na kunifunulia  ili nimjue MUNGU aliye hai na Neno lake.

Tangu nianze kuhubiri kwa njia ya mtandao sasa ni mwaka wa 4 unaenda, Nilipoanza sikuwa na kauli mbiu ya Mwaka bali kile ambacho MUNGU alinipa kusema nilikisema.
Mwaka jana mwishoni nilikuwa naangalia page za makanisa mbalimbali niliona kauli mbiu yao ya mwaka 2015. Nilibarikiwa sana na kauli mbiu hizo kutoka makanisa mbalimbali, nilitamani na mimi nifuate kauli mbiu mojawapo katika hizo za makanisa.
Lakini baadae nisukumwa kuomba juu ya kauli mbiu yangu ya mwaka mpya wa 2015, niliomba juu ya kupewa mwongozo wa kutembea katika huo kwa mwaka mzima wa 2015.

Nilipoomba sikujibiwa amapema, hadi ikabaki siku moja mwaka kuisha, Nilijisemea moyoni kwamba ''Hata kama BWANA hatanipa mwonozo wa 2015 basi akinipa neno tu hilo ndilo nitalisema''

Siku ya mwisho wa mwaka huwa kuna mkesha wa maombi wa kukaribisha mwaka, nilienda kwenye mkesha na baada ya mkesha nilirudi nyumbani na kulala.
Baada ya kulala tu hata kabla sijasinzia vizuri nilisika sauti ikisema ''Tubuni kwa maana ufalme wa MUNGU umekaribia'' Nikapewa na andiko la kusimamia kwa Mwaka mzima ambalo ni Mathayo 3:2 inayosema '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''
Nikaambiwa ''Fundisha hivyo''.
Sauti ile ilisema mara mbili ndipo nikajua hakika MUNGU amesema nami juu ya kuhubiri Toba iondoayo dhambi.

Baada ya kujua Mwongozo wangu wa mwaka 2015 unaosema ''TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA''
 Nilianza kufundisha masomo,  na hadi leo mwezi wa mwisho wa mwaka huu nimefundisha masomo kamili 183 huku masomo 50 nimeyaandaa nusu nikisubiri kuyamalizia na hayo sijayapost.

Masomo 7 ya kwanza katika mwanzo wa mwaka huu ni haya;


 1.TUBUNI KWA MAANA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA.


 2.MUNGU ANATAKA UFANYE HAYA MWAKA 2015.


 3.USIKUBALI KUPITWA NA UPENDO WA MUNGU.


 4.MIMI,NINYI NI NURU YA ULIMWENGU.


 5. NI KWELI UMEFANYA SIRI ILI WANADAMU WASIJUE, NA  MUNGU JE?


 6.MAJINA SABA YA HESHIMA YA WATEULE WA MUNGU.


 7. KUMKATAA YESU NI KUKATAA UZIMA WA MILELE.

Nina mengi sana ya kumshukuru MUNGU kwa mwaka huu.
=Kupitia jumbe zangu kuna watu wengi tu nimewaongoza sala ya toba kwa njia ya simu na kuwaelekeza makanisani kwenda kuabudu.
=Kupitia jumbe zangu wengi sana wamenipigia simu na kunitumia meseji wakisema wamebarikiwa na jumbe na pia kupitia jumbe hizo wameacha dhambi fulani fulani.
=Kuna wengi walikuwa na miaka mingi bila kwenda makanisani lakini kupitia masomo yangu wamerudi kanisani.
=Kuna ambao walidhani wana dhambi kubwa sana hivyo MUNGU hawezi kuwasamehe lakini kupitia kujifunza masomo yangu wamenihakikishia kwamba wanarudi kanisani na wanatubu na kuacha uovu. Shuhuda ni nyingi sana lakini muhimu kwangu ni kumshukuru MUNGU BABA kwa akile alichotoa kwa ajili yangu na rafiki zangu kwa mwaka mzima wa 2015.
=Mwenye sikio la kusikia hakika alisikia na mwenye kuuhitaji uzima wa BWANA YESU hakika aliufuata uzima huo kwenye nyumba za BWANA ambazo ziko kila eneo.

Namshukuru MUNGU maana pia blog yangu ya maisha ya ushindi aliipa kibali kikuuu maana kwa mwaka watu wameisoma zaidi ya mara laki 6.
Namshukuru MUNGU pia kwa group yangu ya Neno la MUNGU Facebook sasa ina marafiki zaidi ya Elfu 60.
Kote huko ni madhabahu ambazo MUNGU anatumia kupitia Neno lake kutoka kwa watumishi wengi na mimi pia nikiwa miongoni mwao.
Napenda pia kumshukuru kila ndugu aliyesoma ujumbe wangu wa aina yeyote kwa mwaka mzima.
Nawashukuru ndugu wale ambao wali-print baadhi ya masomo yangu na kuyasambaza mitaani ili watu wampokee BWANA YESU aliye pekee na uzima wao.

Namngoja BWANA YESU kwa ajili ya mwaka 2016 kama neema yake ingalipo.
Namngoja BWANA YESU pia kwa  baraka itakayowezesha kuchapishwa kwa vitabu vyangu  vitakavyorahisisha pia uinjilisti kwa watu wengi zaidi.
Asante kwa kila aliyeniombea na asante pia kwa kila aniyenishauri na kunisahihisha maana hakuna mwanadamu anayejua yote bali tunategemeana sana wote.
Kila mtu ni muhimu na kwa MUNGU hakuna upendeleo(Matendo 10:34).
Tushilikiane ndugu zangu kwa utukufu wa MUNGU.
Mwenye kutengeneza na MUNGU pia nafasi hiyo bado ipo maana makanisa yako kila kona na wachungaji wako kila mahali hivyo ni jukumu tu la kuwaendea na watatuombea na kutuongoza kiroho ili tukue kiroho.
Matendo 3:19 '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;''

Asante ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye msimamizi wa wokovu wetu ulio wa thamani sana aliotuletea BWANA YESU.
Namshukuru sana MUNGU wa mbinguni kwa ajili ya 2015.

''Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Wamchao BWANA na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. BWANA  yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa. Ni heri kumkimbilia BWANA Kuliko kuwatumainia wanadamu. Ni heri kumkimbilia BWANA. Kuliko kuwatumainia wakuu.-Zaburi 118:1-9''


MUNGU wa mbinguni akubariki sana na kama hujaokoka nakuomba mpokee BWANA YESU ili akuokoe.
Usikubali kuingia mwaka mpya ukiwa hujaokoka.
okoka na utafanya vyema sana.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
mabula1986@gmail.com
0714252292.
Asante sana kwa kusoma ujumbe wangu kwa mwaka mzima.

Comments