POLISI Kagera imewakamata watatu wanaotuhumiwa mauaji na uchomaji moto makanisa.

Moja ya makanisa lililochomwa moto mwezi wa 9, hapa ni wakati likiungua.
POLISI mkoani Kagera imewakamata watu watatu wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji na uchomaji moto makanisa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa matukio hayo yalikuwa yakifanyika mfululizo tangu mwaka 2013 hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Kamanda Ollomi alisema katika kipindi hicho, kulitokea matukio mauaji 12 na matukio ya uchomaji wa makanisa 14 na kufanya jumla ya matukio hayo ya uhalifu kuwa 26.

Times Fm TZ's photo.
Alisema sehemu zilizoathirika na matukio hayo ni wilaya za Bukoba, Missenyi na Muleba. Aliwataja watuhumiwa wa matukio hayo kuwa ni Rashid Athuman (28) mfanyabiashara ya urembo wa kuchora kucha mkazi wa Rwamishenye, Aliyu Hassan (35) muuza sufuria mkazi wa Kemondo na Ismail Ngesela ambaye kabla hajasilimishwa alikuwa akiitwa Joseph Mazumira (23), mfanyabiashara ya kuuza CD mkazi wa Rwamishenye.


Alisema Novemba 21, mwaka huu, Polisi mkoani Kagera kwa kushirikiana na Kikosi Kazi cha Taifa waliwakamata watuhumiwa hao baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa ndio wahusika wakuu wa matukio hayo.


Comments