SEMINA YA UPONYAJI SIKU YA TATU NA ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA.

Na ASKOFU MKUU DR JOSEPHAT GWAJIMA, UFUFUO NA UZIMA.


Tuliona sababu zinazo msababisha mtu kesho yake ikapiga kona kwamba mwili wa mtu ni udongo na unaweza ukapandikizwa vitu kama magonjwa, laana, balaa, matatizo, kansa, ukafungwa kizazi mtu asizae na mambo mengine mengi na sababu ya Pili tumeona mtu anaweza akaibiwa nyota yake na kesho yake ikapiga kona. Kila mtu anayo nyota yake, mfano mzuri ni Bwana Yesu alikuwa ananyota ya Ufalme na mamajusi(wachawi) kutoka mashariki waliiona nyota yake wakaifuata lakini kwa lengo la kuisujudia.
Mtu anaweza akaibiwa nyota ya uso(mvuto), nyota ya ufahamu, nyota ya akilii, nyota uongozi, mvuto, tumbo la kuzaa viongozi, utawala, mikono nk unaweza ukaibiwa na mtu mwingine akaitumia kujinufaisha kwenye siasa, michezo, muziki, utawala, urembo nk
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”Yeremia 1:1-
Kabla hujazaliwa Mungu alikujua na amekupa maisha unayotakiwa kuishi na jukumu ambalo limekuleta hapa duniani ili ilitimize ndipo urudi kwake mbinguni.
Sababu ya tatu inayofanya kesho ya mtu ipige kona na maisha ya mtu yaharibike ni mapepo/ mashetani.
Somo kubwa sana alilofundisha Bwana Yesu lilikuwa ni kukemea mashetani na kuyatoa ndani ya watu.
Neno mapepo ni Lugha ya kibiblia lakini kwenye lugha ya kawaida yanaitwa mashetani. Hii kazi ya kuyateketeza mapepo ndio kazi aliyoifundisha Yesu kubwa kuliko zote alipokuja duniani. Kwa habari ya kufundisha Yesu alifundisha habari ya Ufalme wa Mbinguni lakini kwa habari ya kazi alifanya kazi ya kuyatoa mapepo kwenye maisha ya watu na akatuachia sisi jukumu hilo.
“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake” Ufunuo 12:7

Mashetani ni majoka, walikua mbinguni wakamuasi Mungu wakalaaniwa wakawa majoka. Sifa ya mashetani hawa wanaijua Biblia na nguvu za Mungu, ndiomaana shetani alipomtokea Bwana Yesu alimwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajitupe chini sababu imeandikwa atawaagiza malaika zake wakudake. Wanalijua neno la Mungu.
“Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?” Mwanzo 3:1

Hawa ni wajanja sana wanaweza wakaja kama wanahubiri neno la Mungu lakini ukozubaa wanakuteka na kukupoteza.
Aina nyingine ya masheyani ni mizimu. Haya ni mashetani yanayofuatilia familia na ukoo na kusababisha matatizo yanayofanana kizazi baada ya kizazi. Mfano mzuri ni Baba wetu wa Imani Ibrahimu alikuwa anamatatizo ya kuzaa kwa mkewe, baadaye akaja mwanae Yakobo naye akapata tatizo hilohilo kwa mkewe, sio kwamba Baba wa Imani Ibrahimu alikuwa ana matatizo ya mizimu, HAPANA bali Biblia imetuonyesha jinsi matatizo yanavyoweza kutokea ndani ya familia kizazi baada ya kizazi.
Mizumu hii hujifanya kama ndugu wa familia waliofariki ambao wanakuja kuwatembelea, na hawa mizimu hutaka watoto wapewe majina yao, Mfano mtoto nyumbani anaweza akawa analia sana au anaugua sana mara kwa mara mkaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji na mganga huyo akawaambia motto anataka jina la babu au bibi aliyekwisha fariki mkimpa ananyamaza, kumbe ni mzimu umeingia kwenye familia ili ulete matatizo kupitia motto wenu.

Kuna watu hupenda kuomba makaburini na huamini kwamba watu waliokufa wanaweza kufufuka jambo ambalo sio kweli bali ni kuabudu mashetani. Mizimu hii inaweza kuongea lugha zote za kinyeji na kufanya mambo kama ya wafu waliofariki, hudanganya watu kwamba ni ndugu waliofariki. Hao ni aina mojawapo ya mashetani wajanja sana na hufahamu lugha ya familia, na wakati mwingine huweza kuigiza sauti ya mtu aliyefariki.
Mungu wetu sio Mungu wa wafu, mtu akishafariki ndio mwisho wake hawezi kurudi tena labda afufuliwe kwa jina la Yesu.
Aina nyingine ni majiini ambao hukaa kwenye sehemu za mila za kiarabu. Mashetani hawa hawajui Biblia na hawajui kwamba Mungu ana nguvu, wao huendana na mila za kiislam(si kwa maana mbaya) “Shehe falsie wa Zanzibar, kitabu chake kinasema majini ni viumbe wepesi wanokaa angani hawana viwiliwili lakini huweza kugeuka na kuvaa maumbo mbalimbali nao hufanana na mashetani” kwenye mila za kiislam husema kuna majini mazui na mabaya, sisi wakristo tunaamini wote ni mashetani. Hakuna jinni mzuri wala mbaya.
Kwenye nchi kama ya Tanzania kwenye maeneo ya mwambao wa bahari ya hindi ndipo majini haya hupatikana. Ukikutana na majini haya hujidai wana nguvu sana sababu hawazijui nguvu na Yehova.
Aina nyingine ya mashetani ni miungu ambayo huabudiwa sana kule bara la Asia. Kwenye kitabu cha matendo ya mitume Paulo alikwenda kule atemi akakutana na mungu mke anayeabudiwa Asia yote, Ulaya mungu huyohuyo anaabudiwa kwa jina lingine.
Hawa miungu walishaabudiwa muda mrefu, wakapewa sadaka muda mrefu, wakafukiziwa ubadi, wakapewa chakula sana kwa muda mrefu mpaka wakanenepa wakaitwa miungu na nchini india miungu ipo mingi sana.
Kuna sababu kuu Nne ambazo zinaonyesha jinsi mashetani yanaingia ndani ya mtu.
1. Sababu ya kwanza ni dhambi. “Dhambi ni kila lisilo haki”. Mtu anaweza akawa anakwenda kanisani lakini anaishi maisha ya dhambi, anaweza akawa anatoa sadaka lakini anaishi maisha ya dhambi, watu wengi sana kwenye makanisa wamepagwa mapepo lakini hawajijui. Mahala ambapo pana moto shetani hawezi kukaa.

2. Sababu nyingine ni mashetani yanaweza kutumwa. Waganga wa kienyeji wana leseni ya kuita mashetani na kuyatuma. Wanapiga ngoma na kufukiza ubani mpaka yanakuja na anayatuma kwa mtu Fulani yakamwingie ili yamtie udhaifu, magonjwa, roho ya kifo, balaa, kukataliwa, mikosi nk
Luka 13:10- “Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.”
Pepo anaweza kukufanya ukawa mdhaifu, pepo anaweza akamwingia mtu akakaa kwenye mgongo na kumfanya asitembee vizuri. Mapepo yanatumwa kwa watu sababu ya wivu, kuna mtu kazini, kwenye ukoo, jirani yako, ambaye hakupendi anaenda kwa mganga na kukutumia mapepo hayo, adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake.
3. Sababu nyingine ni mashetani humwingia mtu sio kwasababu ametumwa au umetenda dhambi bali ni kazi yao.
Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”

Kuna maeneo ambayo mashetani yanakaa kama kwenye miti mikubwa porini kama mibuyu, kwenye siku ya arobaini ya msiba, chakula vya aina hii hutolewa sadaka kwa miungu na huwa na mashetani ndani yake.
Mashetani yanaweza kukubeba yakabadilisha maisha yako mpaka ukawa unaishi sehemu ambayo sio nzuri, ukawa na tabia mbaya ambayo hata mwenyewe unajishangaa.
Shetani anaweza kufanya kazi akiwa ndani ya mtu, anaingia ndani anaongoza akili, hisia, anakuwa anakuongoza yeye. Pia anaweza kuwa nje ya mtu na kutenda kazi kumzuia mtu asifanikiwe.
Zakaria 3:1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.”

Hapa Askofu mkuu amesimama na shetani yupo nje yake lakini yupo pembeni anashindana naye , pia kuna namna mtu anaweza kuvaa ambapo anamkaribisha shetani. Unaweza ukawa unamfukuza shetani lakini unamkaribisha mwenyewe jinsi ulivyo.
Luka8:26 “Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa. Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.38 Na mtu yule aliyetokwa na pepo alimwomba ruhusa afuatane naye; lakini yeye alimwaga akisema,39 Rudi nyumbani kwako, ukahubiri yalivyo makuu Mungu aliyokutendea. Akaenda zake, akihubiri katika mji wote, yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu.”
Tumeona Bwana Yesu alimwambia mtu yule arudi kwenye mji wake akawahubirie watu matendo ambayo Mungu amemtendea.
Mathayo5:1- “Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao. Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.”

Tumeona mfano huo kwenye kitabu cha Marko na Luka kwamba mashetani yanaweza kumuingia mtu na makao yake yakabadilika , akawa na nguvu sana na kujikatakata, kukata minyororo na kufanya mambo ya ajabu sababu anakuwa anaongozwa na mashetani hayo.
Mtu huyu alitakiwa awe mhubiri mkubwa wa miji mikubwa kumi iitwayo Dekapoli maana ya Dekapoli ni Deka ni (kumi) na poli ni (mji) mfano mzuri ni mji mkuu wa Libya unaitwa Tripoli hivyo basi (Tri) ni tatu na (poli) ni mji uliounganika miji mitatu ndiomaana unaitwa Tripoli na mtu huyu alipofunguliwa na Yesu, aliambiwa akawahubirie watu wake Dekapoli maana yake akafanye kazi yake aliyotumwa kuja kuifanya hapa duniani ambayo ni kuwa mkuu wa makanisa ya miji kumi (Dekapoli).
Kumbe mtu unaweza kuwekewa mashetani yamkapindisha akawa anaishi maisha ambayo sio asili yake, ukawa umepindishwa kesho yako, kwamba ulitakiwa usafiri nje ya nchi ukutane na mtu ambaye atakusogeza kwenye maisha yako ya asili lakini unakwama unapindishwa na mashetani unaelekea kufanya mambo mengine kabisa tofauti na kusudi lako.

Unaweza ukawa unakula chakula ambacho sio kile unachotakiwa ule, unavaa mavazi usiyotakiwa uvae, unaishi maisha ambayo siyo yako ya asili lakini ni mashetani ndiyo yamekufanya uishi hivyo na kumbuka yanaweza yakawa ndani yako au nje yako.
Tumeona mtu huyu wa dekapoli alikaa kwa muda mrefu pale makaburini sababu alikuwa anajulikana na watu wote wa mji ule. mtu huyu alikuwa anajikatakata kwa mawe, anakata minyororo, lakini Yesu alipanda boti kwaajili yake akavuka ngambo akaenda kufumgua na kumrudisha kwenye kusudi lake lililopigishwa kona.
Ukiri:
“Palepale waliponifungia Moto wa Bwana unakuja Palepale nilipo na kunifungua”

Inawezekana wewe umepangiwa uwe waziri, mfanya biashara mkubwa au mkurugenzi lakini umepindishwa kona unaishi maisha ya tofauti lakini Yesu anakuja palepale ulipo na kukufungua urudi kwenye maisha yako kwa jina la Yesu.
Ukiri
“Kwa damu ya Yesu narudi kwenye maisha yangu ya asili niliyopewa na Mungu kwa jina la Yesu, ninakataa kubaki hivi nilivyo kwa jina la Yesu”

1Thesalonike 2:18 “Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.”
Paulo alizuiliwa na shetani na sio kwamba shetani alikuwa ndani ya Paulo, inawezekana alikuwa anataka kwenda mahali na mtoa visa akazuia asipate visa lakini Paulo kwenye macho yake ya rohoni aliona ni shetani ndiye aliyemzuia, kuna watu wengine wanatumiwa mashetani ndani yao na yanawaletea tabia wasizozipenda.
Mathayo 27:51-56 “Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu. Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, hao ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia. Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.”

Wakati Yesu anakufa tetemeko linatokea, dunia inakuwa giza na akida anakimbia na kusema hakika huyu alikuwa mwana wa Mungu, Yesu anaingizwa kaburini Mariamu Magdalena yupo anamwangalia Yesu kama Shuhuda, Bwana alimtokea akamwambia aende akawatangazie wanafunzi wa Yesu kwamba amefufuka kutoka katika wafu. Mariamu Magdalena alikuwa anampenda Bwana Yesu kiasi kwamba hakuona tatizo kuupaka mwili wake mafuta mpaka Bwana Yesu alipomtokea na kumtuma akawatangazie wanafunzi wake kuwa yu hai.
Luka 8:2 “Na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba”
Huyu mwanamke aliandaliwa na Mungu kuwa shuhuda wa mateso ya Bwana Yesu, kifo cha Bwana Yesu, mpaka kufufuka kwake Bwana Yesu awe shahidi wa ufufuo lakini ukiangalia kabla ya hayo kutokea alikuwa amejazwa mashetani ili asitimize hilo kusudi lake, alikuwa ni mwinjilisti wa kwanza kwa habari ya ufufuo wa Bwana Yesu.
Ukiri:
“Kwa Jina la Yesu mashetani yaliotumwa kuharibu kesho yangu ninakataa kwa jina la Yesu, ondoka ndani yangu kwa jina la Yesu”
Pengine una stress, umeambiwa una kansa utakufa, unamaisha Fulani ambayo unajiona hufai hata kuokoka huwezi tena lakini unatakiwa ujue kwamba shetani anaangalia watu wenye kusudi kubwa la maisha yao ili awazuie wasilifikie kusudi lao, angalia watumishi wa Mungu wakubwa wamepindishwa maisha yao lakini Mungu amesaidia wakafanikiwa.

Usikate tamaa kwa jinsi ulivyo au kwa jinsi unavyoonekana au kwa jinsi ulivyokosea au kwa jinsi ulivyotenda dhambi unatakiwa ukatae na kuyaondoa mashetani hayo kwa jina la Yesu. Unatakiwa umwamini Mungu na atakusaidia urudi kwenye kusudi la maisha yako kwa jina la Yesu.
Yesu kristo alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea. Mungu ni Mungu wa nafasi ya pili hatakama umepoteza mara nyingi utarudi kwenye kusudi lako na utafanikiwa kwa jina la Yesu.
Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”
AMEN

Comments