SIFA SABA MTU MWENYE KIBURI.

Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe.
karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo nazungumzia kiburi.

Mithali 16:18-20 ''Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi. Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri.'' 

Kiburi hakifai na kinatakiwa kiondoke kwa kila mtu.
Ukiona kiburi ujue maanguko ya ndugu huyo yako karibu ndivyo Biblia inavyosema hapo juu.
Kiburi wengi husema ni asili ya mtu lakini mimi nasema kwamba kiburi ni roho ya shetani inayowaingia watu na kuwatumikisha kipepo.
Wengi leo wakihubiriwa wanadharau ni kwa sababu ya kiburi kilicho ndani yao.
Hakuna ambaye anaweza kuchukia uzima wa milele, lakini kwanini watu wakiambiwa habari za uzima wa milele wanawatukana hata hao wahubiri? ni kwa sababu ya roho ya kiburi.
Hakuna asiyetaka kupona lakini kwanini mtu akiambiwa aende kwenye maombezi anaanza kuwatukana waombaji ambao hata hajawahi kuwaona? Ni roho ya kiburi inasumbua wengi.
Ndugu yangu, usikubali kuwa na roho ya kiburi.
Kama roho ya kiburi inakutesa hakika unaomba kwa MUNGU ili iondoke.
Wengi sana wamekosa mbingu kwa sababu ya roho ya kiburi.

 ''Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. - Mithali 29:23''

Kiburi hudhalisha;
=dharau.
1 Samweli 2:30 ''Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.'' 

=Matukano.
 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya KRISTO YESU;-Wafilipi 2:3-5'' 

=Dhambi zote.
Mithali 14:34 ''Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.'' 

=Kupuuzia jambo hata ambalo halitakiwi kupuuzwa.
 ''Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.-Isaya 66:2''
=Kujiona unafaa sana kumbe hufai mbele za MUNGU kwa sababu ya dhambi zako.
 ''Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza.-Yakobo 4:10''

=Kujuiona unajua kumbe hata hujui.
 ''Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke-1 Kor 10:12''

=Kufanya anasa. 

'' Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.-Yakobo 4:6''
 
=Tamaa ya dhambi N.k
 ''BWANA ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.-Mithali 15:25''

Kiburi ni mama wa dhambi zote.

Sifa saba za mtu mwenye Kiburi;

1. Hajui kujishusha hata kama amekosea.
 ''Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.-Mithali 13;10''

2. Maongezi yake mengi yamejaa kujisifia yeye.
'' Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni MUNGU  wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.-1 Samweli 2:3'' 

3. Hana utii pote panapohitaji utii.
 ''Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa-Luka 14:11''

4. Analofanya yeye tu ndilo sahihi lakini ya wengine yote hayafai.
 ''Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya KRISTO YESU ; -Wafilipi 2:3-5''

5. Halekebishiki.
 ''Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu.-Mithali 16:5'' 

6. Anajifanya anajua yote.
'' Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.-Mithali 16:25'' 

7. Hutaka kusikilizwa yeye tu huku yeye hayuko tayari kusikiliza wengine.
 ''Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.-Mithali 18:12''

Kiburi ni kibaya sana.
Kiburi ni mama wa dhambi zote maana kiburi ndicho kilimshusha shetani kutoka mbinguni.
Mtu Mwenye kiburi ni mfuasi wa shetani.
Ni muhimu kukataa kiburi kwa kuokoka na kutubu.


''Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu MUNGU huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa MUNGU ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.1 Petro 5:5-7''
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments