SOMO: Siri ya kifo cha ghafla (Kuchukuliwa msukule)

Na ASKOFU MKUU Dr JOSEPHAT GWAJIMA, Ufufuo na uzima.


Imeandikwa: Mambo ya walawi 19:26 "Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi."
Imeandikwa: Kumbukumbu la torati18:10-11"Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu."

Kwenye Biblia imeonyesha mtu anaweza akalogwa na wachawi wapo.
Imeandikwa: Wagalatia 3:1 "Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?"
Inamaanisha kuna mambo mtu anaweza akayafanya ikiwa tu amelogwa na wachawi. Mtu anaweza akawa amekufa kichawi kabisa na wachawi ndio wanaokuwa wamemchukua na kumfanya msukule. Huku duniani tunaweza tukawa tunafahamu fulani amefariki kumbe ameibiwa yupo mahali anafanya kazi fulani na nyota yake inatumika huko.
Wafalme wengi duniani wamejengwa na uchawi.
Imeandikwa: Danieli2: 1 "Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme. Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake."
Mfalme Nebkadreza aliishi miaka zaidi ya mia sita kabla ya kuzaliwa kristo. Alikuwa amejenga utawala wake kwa kutegemea waganga wa kienyeji na wachawi.
Imeandikwa: Kutoka 7: 11 "Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao."
Imeandikwa: Danieli 5:7 "Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme."
Mfalme Nebkadreza, Farao na Mfalme wa Babeli wote hawa walikuwa wanatumia uchawi kwenye tawala zao.
Kuna wachawi wanafanya vitu kwa ruhusa ya wafalme wa nchi. Ukiwa na Bwana Yesu ndani yako unakuwa huwezi kulogwa wala kuonewa na shetani na mawakala wake.
Wokovu sio dini wala dhehebu wala ulokole, wokovu ni kuingia ndani ya Ufalme wa Yesu na kutua mizigo yako sababu amesema njooni kwangu ninyi nyote mlemewao na mizigo nami nitawapumzisha. ukiwa na Yesu huwezi kulogwa iwe ni kwenye chakula, kwenye gari, kwenye kinywaji, kazini, kwenye biashara au mahala popote sababu unakuwa unaishi ndani ya Ufalme wa Mungu na unakuwa umezaliwa upya na kuwa mwana wa Mungu, kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu.
Imeandikwa: Hesabu 23:23 "Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!"
Duniani kuna biashara ya kuuza wanadamu ambao husafirishwa kwenda nchi mbalimbali, kwenye ulimwengu wa rohoni pia kuna biashara ya kuuza wanadamu inafanyika pia.
Imeandikwa: Nahumu 3:4 "Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake."
Taifa linaweza likauzwa likawa mali ya kuzimu, mapato yote yanayopatikana unakuwa huoni yanakwenda wapi.
Imeandikwa: Ufunuo 18: 11 "Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu. Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe."
Watu wanawinda roho za watu na kuziuza kama bidhaa kwa wafanya biashara. Mungu anasema atazitoa roho hizo mikononi mwao walioziiba kwa nguvu na kuzirudisha kwa watu.
Imeandikwa: Ezekiel 13: 20 "Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
Wachawi wanaweza wakaiba miili na roho za watu na pia wanaweza wakaiba viungo vya mtu kama moyo, akili, nyota, mikono kwenye ulimwengu wa rohoni huku mtu aliyeibiwa akiwa na mgonjwa mara kwa mara na kuwa na mikosi au wanaweza wakamchukua mtu mzima mzima na kumtumikisha kwa shughuli zao za kichawi huku akidhaniwa kwamba amekufa.
Imeandikwa: Isaya 42: 22 "Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha."
Mtu anaweza akaibiwa na kuuzwa, Yuda alimuuza Yesu kwenye ulimwengu wa mwili lakini kwenye ulimwengu wa rohoni mtu anaweza akaibiwa akaoneka amefariki kumbe ameibiwa na kupelekwa kutumikishwa mahali kufanya kazi fulani.
Imeandikwa: Mathayo 10: 7 "Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure."
Unaweza ukawa unaishi na mtu haeleweki kitabia au kiakili kumbe mtu huyo kiroho ameibiwa na anatumikishwa mahali na huyo uliye naye siyo yeye halisi unaye mfahamu. Mtu mwingine anaweza akawa amapatwa na ajali anakufa papo hapo lakini kuihalisia anakuwa hajafa ila amechukuliwa msukule na kupelekwa sehemu ili afanyishwe kazi.
Au mtu anaweza akawa amelala usingizi akafariki akiwa amelala , mtu huyu anakuwa ameibiwa msukule na mara nyingi watu wa nanaofariki namna hii huwa wanazikwa siku hiyohiyo ili iwe rahisi kuchukuliwa msukule wasije akarudishwa. Watu wa aina kama hizo ndio wanaitwa wameibiwa.
BAADA YA MAOMBI YA KUWARUDISHA WATU WALIOIBIWA NA KUTEKWA KULIKUWA NA SHUHUDA NYINGI LAKINI BAADHI YA SHUHUDA HIZO NI.
Dada mmoja ambaye amerudishwa ameeleza alikuwa anatumikishwa kwenye shughuli za kubeba mizigo na kufua nguo za watu pamoja na kulima na mkoani Morogoro. Alikuwa pamoja na watu wengi waliochukuliwa msukule. Anaeleza kwamba alisikia sauti ya watu wengi ikimuita njoo na ghafla akajikuta yupo kanisani na kuona watu wengi. Amemshukuru Mungu kwa kumwokoa na kuahidi kumtumikia maisha yake yote.
Dada mwingine ambaye amerudishwa ameeleza kwamba alikuwa amechukuliwa na Babu yake alifariki siku nyingi tangu akiwa mdogo ambaye alitaka amfanye malkia ili azae watoto wa kijini. Dada huyo ameelezea kwamba akiwa chini ya bahari alilishwa pete mbili na Babu yake ili akiwa mtu mzima azae watoto kutokana na pete hizo, ameelezea wakati akiwa huko kuzimu alisikia watu wakiita Njooo ndipo akaambiwa mwili wamke umeenda sehemu ambayo siyo na akawaona watu wawili weupe wenye mabawa anamfuata na kumchukua na ghafla akajikuta yupo kanisani. Amemshukuru Bwana Yesu kwa kumwokoa na kuamua kumtumikia maisha yake yote.
MAOMBI NA SHUHUDA ZOTE ZA WATU WALIORUDISHWA MSUKULE ZINAPATIKANA KWENYE DVD.

Comments