UKOMBOZI WA MJI KWA MIKONO YA WAKOMA


Ufufuo na uzima Morogoro.
 
Na:     STEVEN NAMPUNJU (RP)
& DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP
Utangulizi: Kwenye mji wapo watu wenye shughuli zao, makazi yao na ndipo watu wanaishi. Wakoma kwa mujibu wa Biblia ni watu waliokuwa wanatengwa na jamii kana kwamba wana laana ili kamwe wasiguswe na jamii yao. Mji unaweza kuwa umeharibiwa au umetekwa. Mji wa Yeriko mfano, uliwahi kufungwa kabisa kwa ajili ya wana wa Israeli. Upo uwezekano kabisa kwa mji kufungwa kabisa kwa sababu ya jamii fulani. Maana yake, jamii iliyofungiwa nje haiwezi kuendelea hadi huo mji ukombolewe kwa ajili yao katika Jina la Yesu.
Mji  Wagerasi pia ulikuwa siyo rahisi kuufikia kwa sababu ulifungwa ili watu wasiingie mle. Bahari ilichafuka sana siku ile Yesu alipotaka kuelekea kwenye Mji huu wa Wagerasi. Mtu huyo aliyewazuia watu kuingia humo alikuwa hakai nyumbani bali anaishi makabaurini na kuzuia watu waliotaka kuipita njia ile kuelekea humo mjini. Yesu aliyatoa mapepo yote yaliyokuwa yamemfunga huyu mtu na kumweka huru.

Imeandikwa katika LUKA 19:41-44…[Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.]… Yesu aliuona Mji na kuanza kuulilia. Hata sasa yamkini Yesu anaulilia mji wako, na kusema ”Laiti ungalijua ewe Morogoro, Laiti ungalijua ewe Mwanza, Laiti ungalijua ewe Dar es Salaam,”. Yesu anauombolezea mji ingawa wenyeji  wa ule mji hawajui ni kipi cha kufanya.

Mji unaweza kuutekwa na watu  kwa maslahi fulani fulani. Mfalme hana mamlaka tena kwa mji amboa tayari ulishatekwa na wenye nguvu.  
Imeandikwa katika 2 WAFALME 6:24-33…. [Ikawa baada ya hayo, Benhadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. 25 Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha. 26 Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita ukutani, mwanamke mmoja akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. 27 Akasema, Bwana asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni? 28 Mfalme akamwambia, Una nini? Akajibu, Mwanamke huyu aliniambia, Mtoe mtoto wako, tumle leo, na mtoto wangu tutamla kesho. 29 Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake. 30 Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake. 31 Ndipo akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, kikimbakia kichwa Elisha mwana wa Shafati juu yake leo. 32 Lakini Elisha alikuwa akikaa nyumbani mwake, na wazee wakikaa pamoja naye; na mfalme akamtuma mtu wa mbele yake; lakini hata kabla ya kufika kwake yule aliyetumwa, akawaambia wazee, Je! Mwaona jinsi huyu mwana wa mwuaji alivyotuma aniondolee kichwa changu? Angalieni, huyo aliyetumwa akifika, fungeni mlango, mkamzuie mlangoni; je! Sauti ya miguu ya bwana wake haiko nyuma yake? 33 Hata alipokuwa katika kusema nao, tazama, yule aliyetumwa akamshukia; naye akasema, Angalia, mabaya haya yatoka kwa Bwana; kwani mimi kumngojea Bwana tena?]…Uwepo wa njaa kali sana ulisababisha wamama wawili  kukubaliana kuzila nyama za watoto wao. Msaaada wa kweli unapatikana katika Bwana aliyeumba mbingu na nchi. Haupo  msaada utakaopata kutoka kwa mbunge au hata rais. Kumbuka imeandikwa “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu”. Elisha alikuwa na uwezo  wa kuzijua siri za mfalme wa Shamu alizojadiliana akiwa chumbani kwake. Wakati mfalme anaapa kumwangamiza Elisha, upande wa pili alikuwepo Elisha. Mungu ana uwezo wa kutupasha habari za siri zinazopangwa vyumbani mwa adui zetu. Kuna watu ulioruhusu waingie ndani na wakaleta madhara katika maisha yako. Ili muuaji asifanikiwe kukuchinja, njia nzuri ni kumfungia nje.
Mwuaji anavyotumwa kwako anakuja akiwa anajua sifa kuu mbili:

1.      Aliyetumwa haendi  peke yake,  bali  huambatana na sauti ya miguu ya bwana wake nyuma yake. Huu ni wakati wa kuwafungia nje wauaji wote ili  wasifanikiwe kuingia ndani na kutuchinja kwa Jina la Yesu. MARKO 16:19-20....[Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]…Yesu alilithibiitisha neno lile kwa ishara ingawa alikuwa mbinguni. Na hata yule mfalme alipomtuma kiongozi yule kwenda kwa Elisha, sauti ya miguu yake haikumuacha.

2.      Ukichukua hatua, uwezo wa utiisho vinakutangulia. Ili ufanikiwe lazima uwe na uthubutu. Imeandikwa katika LUKA 13:31-35…[Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. 32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika. 33 Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.]…. Kumbe waliokuja kumwambia Yesu atooke pale kwenye wito wake,  lengo lao  ni ili  Yesu asitoe pepo  na kuponya wagonjwa, asitimize wito wake. Wapo watu wanaokuja kwako kana kwamba wanataka kukupa msaada lakini kumbe ni kwa ajili ya kukutoa wewe kwenye wito wako. Kuna mahali pa kukaa na kufanyia kazi ili ukombozi utokee lakini wengine hawataki ufanye hivyo.
UKIRI
Mahali popote ambapo kwenye mji wangu wa mafanikio leo nakataa katika Jina la Yesu. Achia maisha yangu katika Jina la Yesu. Amen.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      
 
Imeandikwa katika 2WAFALME 7:1- …[Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.]…Kumbuka kuwa Mungu hupendezwa na watu wenye kuchukua hatua.
Imeandikwa katika 2WAFALME 7:3-11…[Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. 8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. 11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.]…Majadiliano ya wakoma yalionesha kuwa, walikaa nje kwa muda mrefu kwa sababu ya kutengwa na jamii.  Wakaona ni afadhali waliendee jeshi, kama nikufa wafe tu.  Mji unakombolewa usiku na mapema, kabla ya alfajiri. Majeshi ya Washami waliamua kutoroka. Waliokamata mi leo ni siku ya kuwakimbiza kwa Jina la Yesu.
Usiogope kuchukua hatua kwa sababu yoyote ile:  Kwamba haufahamiki, kwamba hauna cheo  au jina kubwa. Wanaohatarisha maisha yao huwa wa kwanza kufurahia matunda ya utajiri wa nchi yao.

Imeandikwa katika 2WAFALME 7:12-20… [Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini. 13 Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone. 14 Basi wakatwaa magari mawili na farasi zake; mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni, mkaangalie. 15 Wakawafuata mpaka Yordani; na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo, walivyovitupa Washami, wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme. 16 Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana. 17 Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia. 18 Ikatukia kama vile yule mtu wa Mungu alivyomwambia mfalme, Vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli, ndivyo vitakavyokuwa kesho, panapo saa hii, katika lango la Samaria; 19 na yule akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 20 Ikampata vivyo hivyo, kwa kuwa watu wakamkanyaga langoni, akafa.]…Mji unaweza kuwa ni wewe mwenyewe. Kukiwepo na vurugu rohoni mafanikio hayawezi kuonekana. Unapoona mtu hawezi kufanikiwa, upo uwezekano kuwa rohoni hakuna utulivu.
Ili ukombozi upatikane,  usitegemee akili  zako au uwezo wako. Hayupo  ambaye aliwahi kushindana na kanisa au Mungu mtu huyo akaishi. Walioshindana na Eliya na papo hapo wakaapa kumwangamiza Elisha, hawakutimiza azma zao. Maisha yako ya kiroho ili ufanikiwe, ni budi  kuukomboa mji. Ni hadi palemji unapoko,bolloewa na ndipo uhuru  timilifu uanpopatikana. Wanaotegemea akili zao hukanyagwa langoni. Leo kila akida wa kiroho anayezuia chakula kisitokee katika mji wako akanyagwe na kuangushwa katika Jina la Yesu.
Wewe ambaye hujaokoka leo ni siku  njema kwako  kutengeneza maisha yako na Yesu kwa kumpokea Yesu moyoni  mwako.

Comments