USHUHUDA WA KUTIKISIKA KWA UFALME WA GIZA KATIKA SHULE YA SEKONDARY.



Napenda kumshukuru sana Mungu Kwa ajili ya Utendaji kazi wake katika huduma aliyoniitia.
Mungu alinipa kibali cha kukanyaga katika shule moja ya sekondary iliyopo maeneo ya wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ambapo niliingia kwa mara ya kwanza mwezi wa nane na mara kwa mara nilikuwa naingia pale shuleni katika kufanya huduma ya kuifungua shule pamoja na wanafunzi waliofungwa na shetani kwa kutumia mamlaka ya Jina la Yesu Krsto.
Sasa katika hiyo shule ilikuwa kila mwaka ni lazima mwanafunzi mmoja afariki kumbe hao wanafunzi sio kuwa wanakufa kwa mpango wa Mungu bali walikuwa wanatolewa sadaka za kikafara za uchawi, sasa nipoingia kwa mara ya kwanza nikasema kwa sababu nimeikanyaga shule hii mwaka huu hakuna mwanafunzi atakaye kufa kabisa.
Basi nikawa nafanya huduma nikiwa nimekaribishwa na kikundi cha wana kasfeta nikishirikiana na rafiki yangu mwalimu Mwashambwa ambaye amefanyika kuwa daraja kubwa kwa mimi kuingia pale shuleni.
Nilikuta wanafunzi pia wamefungwa sana sana na nguvu za giza pia wanafunzi wakawa wanazimia sana shuleni na wengine kuumwa mara kwa mara na kulazwa kwenye chumba cha Ness wa shuleni. Lakini baada ya huduma tulizokuwa tunazifanya nikishirikiana na mwalimu wakawa wamefunguliwa wanafunzi wengi na kuponywa magonjwa mbalimbali na kupungua kwa idadi kubwa sana ya kuumwa wanafunzi, pia mwaka huu mpaka shule inafungwa kipindi hiki cha likizo ya mwisho wa mwaka hakuna mwanafunzi aliyefariki pamoja na kwamba upande wa giza walikuwa wanajitahidi sana kutoa kafara mwanafunzi.
Sasa leo hii kuna mwanafunzi aliyemaliza mwaka huu kidato cha Nne nilikuwa namuombea kwa simu mimi nikiwa huku mkoani mbeya na yeye akiwa mkoani arusha kutokana na kusumbuliwa na tumbo. Kwahiyo alizimia na wakati akiwa katika hali hiyo akatokewa na mwalimu mmoja wa shule hiyo na akamwambia tunakupa adhabu hii ya kuumwa na tumbo sio kwasababu yako wewe bali ni kwasababu y wewe kumleta yule mtumishi hapa shuleni ambaye ni mimi, kwasababu huyu mwanafunzi ndiye aliyenifanya niende kwenye hiyo shule kutokana na kuwa alikuwa anazimiaga mara kwa mara shuleni
Kwahiyo huyo mwalimu akamtuma aniambie mimi kwamba nanukuu alichomwambia
"Umuambie huyu mtu alionyeshwa picha yangu kwamba asije tena akakanyaga hapa shuleni kwetu tena, kwasababu tangia ameingia hapa shuleni ametuvurugia kazi zetu na tumeshindwa kutimiza malengo yetu mwaka huu ( malengo hayo waliokuwa nayo ni kumtoa kafara mwanafunzi sasa mwaka huu wameshindwa kumtoa kutokana na mimi kukanyaga hapo shuleni kwao ). Tena akamwambia kama atajaribu kuja tena tutapambana sana na yeye kwani tutaongezeka na kuwa wengi" hayo ni baadhi ya maagizo aliyomwambia anieleze.
Hii inanitia nguvu sana kwamba ufalme huo wa giza mwaka huu umeshindwa kutimiza mipango yao pia wameingiwa na hofu kuu kwaajili yangu na wanatafuta njia yoyote ile ili waweze kuniangamiza, ila najua kabisa kwamba hawataniweza kwani namtumikia Mungu wa miungu na mwenye nguvu kuliko tawala zote za giza.
Kama unakumbuka pia wakati nilipoingia kwenye ile familia iliyopo Mafinga Iringa na kuisaidia wachawi waliokuwa wameifunga walinitegea dawa ili waniue kwenye ajali wakashindwa pia wakaja mpaka nilipo kimwili kunitegea dawa mlangoni ili nife lakini pia wakashindwa
Hii inaonyesha kwamba nikiingia eneo kama uko utawala wa shetani huwa wanaogopa sana kwani Mungu ninayemtumikia akiingia mahali hapo utawala huo huvunjika kabisa.
Nakuomba tuzidi kuombeana kwani bado ninayosafari ndefu sana ya kuifanya kazi ya Mungu lakini na shetani nayeye akitumia mawakala zake nawao huniwinda kila siku ili waweze kuniangamiza nisiendelee kuhubiri Injili ya Ufalme wa Mungu. Ila nafahamu wazi kabisa kwamba shetani na mawakala zake hawataweza kulikatisha kusudi la Mungu aliloweka ndani yangu, bali bado nahitajika kusaidia maelfu ya watu wanaoteswa na shetani.
Kwa hayo matendo makuu Mungu aliyotenda katika hiyo shule ya sekondary mimi kwa Unyenyekevu namrudishia Heshima na Utukufu kwenye kiti chake cha Enzi.
Ubarikiwe kwa kusoma ushuhuda huu.
Mimi ni rafiki yako Mtumishi Samweli Kibiriti. Simu namba 0765 867574.

Comments