USHUHUDA WA KWELI KABISA,YESU KRISTO PEKEE NDIYE NJIA YA KWENDA MBINGUNI!!!........A TRUE TESTIMONY, JESUS CHRIST IS THE ONLY WAY TO HEAVEN, THERE IS ABSOLUTELY NO SUBSTITUTE!!!

Na Sergio Kipande ambaye ndiye anayeshuhudia.

Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 18:20 Lakini nabii yeyote, ambaye atajizulia toka katika nafsi yake kuzungumza neno lolote katika JINA langu, na ambalo sijamwamuru alizungumze, au yule atakayeongea katika jina la miungu wengine , huyo nabii atakufa...... Vile vile na tusome andiko toka katika Yeremia 28:15 Na. Ndipo nabii Yeremia akamwambia nabii (wa uongo)Hananiah, Sikiliza sasa, Hananiah; BWANA( JEHOVA) hajakutuma wewe; lakini unawafanya watu hawa kuamini mambo ya uongo. Yeremia 28:16 Kwa hiyo sasa hivi ndivyo BWANA (JEHOVA) anavyokuambia, Na tazama, Nitakutupilia mbali toka juu ya uso wa nchi : na mwaka huu huu utakufa, kwa sababu umewafundisha watu kuasi kinyume na BWANA (JEHOVAH.) Yeremia 28:17 Kwa hiyo nabii (wa uongo) huyo. Hananiah alikufa mwaka huo huo mnamo mwezi wa saba.........................................Wapendwa wote kaka zangu na dada zangu, mimi najua fika adhabu ya kusema uongo katika JINA la BWANA JEHOVA kwamba ni kifo, na kwa hiyo ushuhuda huu kuhusu Bwana YESU KRISTO ni ushuhuda wa kweli tupu na wale wote walioandikiwa kuupokea wataupokea lakini kwa wote ambao watauona si wa ukweli bali ni wa uzushi MUNGU mwenyewe atalihukumu, kwani dunia nzima hawakuamini ushuhuda wa Noah mtu wa MUNGU aliowatahadharisha kuhusu gharika kutoka kwa MUNGU na matokeo yake ulimwengu mzima uliangamia na wote walikufa kwa kutokuamini kwao kasoro Noah na familia yake watu nane. Watu hawakuwaamini manabii wa kweli wa MUNGU ila waliwaamini manabii wa uongo kwani waliongea mambo ya kufurahisha masikio yao, matokeo yake Israel wote waliendwa utumwani Babylon. Watu hadi leo hawataki kumwamini YESU KRISTO na aliye njia pekee kwenda mbinguni na watu wameamua kujipachika wenyewe unabii na MUNGU anawatizama. Hizi shuhuda zangu zote ni za kweli na ni za YESU KRISTO Mwenyewe Masiya na zimeonyeshwa kwangu kwa kipindi cha miaka 16 sasa na kila maono, neno au ndoto ninazoziota nakutwa zimeandikwa mstari kwenye Biblia Takatifu. .Wapendwa kaka zangu na dada zangu, hebu na tuache kusikiliza uongo na uzushi ambao mwisho wake ni kuziangamiza roho zetu. Jambo moja tu ambalo kwa sasa nataka kukuhakikishia ni kwamba HAKIKA kuna MUNGU, na kwamba YAHWEH au JEHOVA, MUNGU wa Israel ndiye pekee aliye Mungu wa kweli. Hakuna MUNGU mwingine zaidi yake, kwa hiyo hata tukikaa chini na kuanza kuwaonea wivu wana wa Israel na kuwachukia bila sababu hiyo haitusaidii kitu chochote ukweli unabakia uko pale pale kwamba MUNGU wa Israel ndiye pekee aliye MUNGU wa kweli na aliye hai. Na kuhusu maadui wote wa waisrael hivi ndivyo ilivyoandikwa katika maandiko, Mwanzo 12:3 Na nitawabariki wale wote watakaokubariki, na kumlaani yule akulaanie: na katika wewe familia zote za dunia zitabarikiwa. Na vile vile imeandikwa katika kitabu cha, Kutoka 3:6 Na zaidi ya hapo aliongeza kusema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Ni Mungu wa Abraham, Ni Mungu wa Isaka, Na ni Mungu wa Yakobo. Na Moses akauficha uso wake, kwa vile aliogopa kumtazama MUNGU................ Na tujue kwamba Moses huyo huyo mtumishi wa MUNGU ndiye aliyeona katika ulimwengu wa kiroho na akatabiri kuhusu kuja kwake MASIYA YESU KRISTO aliye Mwana wa MUNGU na ambaye alikuja akazaliwa miaka 1,400 baada ya utabiri huo wa Moses. Hebu na tusome andiko kutoka katika, Kumbukumbu la Torati 18:18 Na nitawainulia nabii toka kati yao , kama wewe, na nitatia maneno yangu kinywani mwake ; na ataongea kwao yale yote nitakayo muagiza Kumbukumbu la Torati 18:19 Na akitokea , mtu yeyote yule ambaye hatayasikiliza hayo maneno yangu atakayozungumza (huyo nabii)katika JINA langu, Nitalitaka toka kwake (Atapata adhabu kuu).
USHUHUDA:
Ilikuwa ni kipindi cha kiangazi cha mwaka 1998 nikiwa niko bado Dar es Salaam, Tanzania ambapo niliota ndoto; Na katika hiyo ndoto niliota nimesimama mbele ya kanisa na nilikuwa niko upande wa kaskazini wa hilo kanisa karibu kabisa na kizingiti cha mlango wake. Nikiwa nimesimama pale mbele ya kanisa mara ghafla nikasikia kishindo kikubwa sana cha mlipuko na ulimwengu mzima ukatikisika kutokana na mlio wa kile kishindo kilikuwa ni zaidi ya mlipuko wa bomu la "Neutron", Mara uso wangu ukainuliwa kuelekea juu mbinguni, na ndipo mara ghafla nikashuhudia kuona mbingu zikifunguliwa na katikati ya upenyo(mlango wa mbingu) nikaona amesimama Bwana YESU KRISTO, nilijua kabisa bila ya mashaka yoyote kwa sababu siku ya kwanza alivyoniokoa kwenye ndoto Novemba 1997 nikiwa simjui kabisa MUNGU alijitambulisha kwangu kwamba Yeye ni YESU KRISTO na kwamba nikimfuata yeye na kuliitia jina lake nitaishi. Kutoka mahali pale niliposimama mbele ya kanisa na yeye akiwa juu mbinguni kwenye ule mlango wa mbingu ulipofunguka ulikuwa ni umbali mkubwa, lakini hata hivyo nilimuona akiwa ni mkubwa zaidi ya unavyoweza kumwona mwanadamu wa kawaida. KRISTO YESU Mwokozi wetu alikuwa amesimama na huku akiwa amevaa joho lefu jeupe. Alikuwa amesimama alipo akiwa ameishusha mikono yake chini. Na ndipo kwa ghafla ukatoka mbele zake mwanga mkali mweupe toka pale alipo uikinielekea mimi pale mahali niliposimama mbele ya kanisa. Ndani ya hiyo nuru iliyotoka mbele yake YESU KRISTO kunijia kulikuwa na ndimi ndogo ndogo za moto kama za mshumaa...na ile nuru iliyokuwa imeambatana na zile ndimi za moto na viliponifikia mimi havikuwa na joto lolote ndani yake wala kuunguza kwa aina yoyote . Hilo tukio kutokana na jinsi nilivyoliona pamoja na nikilinganisha na maandiko katika Biblia lilikuwa ni sawa na lile tendo lililo wakuta wafuasi wa KRISTO Mwokozi siku ya Pentekoste kama isemavyo Biblia toka katika Matendo ya Mitume 2:3 Na ziliwatokea wao mfano kama wa ndimi za moto, na zile ndimi zikatua juu ya kichwa cha kila mmoja wao......................Baada ya tukio hilo kutokea nikaamka toka usingizini na katika ndoto yangu. Siku hiyo hiyo nikamtafuta mchungaji kiongozi wa kanisa langu lliitwalo Mwenge Assemblies of GOD Church lililoko katika mji wa Dar es Salaam, Mchungaji James Mboma. Nikamuelezea kuhusu ile ndoto yangu niliyoiota na jinsi nilivyosikia kishindo kikuu kilichofuatiwa na mbingu kufunguka pamoja na Bwana YESU KRISTO niliyemuona akiwa amesimama katika ule mlango wa mbingu, pamoja na ile nuru kali iliyochanganyika pamoja na zile ndimi za motoi zilizotokea mahali alipokuwa amesimama YESU KRISTO Na Jibu alilonipa mtumishi wa MUNGU mchungaji James Mboma kwa Neno la ufunuo alisema MUNGU Mwenyewe alinibatiza Mwenyewe kwa ROHO MTAKATIFU katika ile ndoto niliyoiota. ....................................Ushauri wangu kwa kila mmoja wetu alisomay ushuhuda huu ni kwamba YESU KRISTO ni kweli mkombozi kweli kabisa. Na Yeye ndiyo njia pekee ya kwenda mbinguni na hakuna mwingine yeyote akupelekaye wewe mbinguni zaidi yake, wengine wote watakupeleka motoni, hakika haya maneno ni ya kweli mbele za JEHOVA MUNGU wetu ...Na kama ilivyoandikwa katika Yohana 14:6 YESU akamwambia, MIMI ndiyo Njia, Ni Kweli, Na Uzima; Hakuna yeyote yule ajae kwa BABA pasipo kunipitia kwanza kwangu mimi............. Mimi ni chombo tu na najihesabu kama chombo kisichokuwa na thamani yoyote mbele za MUNGU kati ya mashahidi wengi hapa duniani walio watumishi wa MUNGU sikustahili hata kidogo kupata neema hii ya Mwokozi wetu YESU KRISTO kufunuliwa kwangu na macho yangu kuuona utukufu wake kwenye ndoto zangu, kwa neema ya macho yangu ya kiroho kumuona Yeye pamoja na mikono yangu ikumgusa miguu yake mimi niliye mwenye dhambi. Kuna mengi sambayo nimekwisha kuyaona katika ulimwengu wa kiroho na mpango mzima wa MUNGU wa maisha yangu katika huduma yake, na kwa neema zake MUNGU zisizo na kikomo nitaendelea kuzishuhudia kwenu kadri siku zinavyokwenda kwa rehema zake MUNGU( akitujaalia uhai . Ndugu zanguni tuishio maisha yetu kuwa na YESU KRISTO kama Bwana na Mwokozi wetu, mpokeeni YESU KRISTO, Kwa hakika kabisa Yeye pekee ndiyo njia ya kwenda mbinguni hakuna mwingine ila Yeye. YESU KRISTO peke yake ndiyo Mwokozi, hajafunuliwa kwangu mara hizi zote bure tu, MUNGU amefanya hivyo ili mimi niweze kuwa mmoja kati ya washuhuda wa Mwanaye YESU KRISTO kwa kizazi hiki. Utukufu wote wa huu ushuhuda ninampa MUNGU (JEHOVA) BABA na Bwana wetu YESU KRISTO, Amen!.......................................................................................................... .
The Bible says in Deuteronomy 18:20 But the prophet, which shall presume to speak a word in my name, which I have not commanded him to speak, or that shall speak in the name of other gods , even that prophet shall die. .......and now let us read another passage from, Jeremiah 28:15 Then said the prophet Jeremiah unto Hananiah the prophet , Hear now, Hananiah ; The LORD hath not sent thee, but thou makest this people to trust in a lie. Jeremiah 28:16 Therefore thus saith the LORD; Behold, I will cast thee from off the face of the earth : this year thou shall die, because thou hast taught rebellion against the LORD. Jeremiah 28:17 So Hananiah the prophet died the same year in the seventh month..............My beloved brothers and sisters let us stop believing on lies and tradition of men in which there is no truth, only religion's fables and fairly tales and which leads men into perdition. One thing I would like to tell you is that; truly, there is GOD! And GOD of Israel called YAHWEH(JEHOVAH) is the ONLY true living GOD. There is absolutely NO other god beside JEHOVAH. Therefore, even if we voluntarily decide to deride and hate the Jewish people, this doesn't help us much. And GOD of their fathers, the God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob remain the only true living GOD...So this hatred thing doesn't to us any good at all, let us live harmoniously with each other because altogether we are citizens of this earth. God of Israel is a true living GOD and there is no another!. It is also written in Genesis 12:3 And I will bless them that bless thee, and curse him that curseth thee: and in thee shall all families of the earth be blessed. Furthermore, it is written in Exodus 3:6 Moreover He said, I am the GOD of thy father, the God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob. And Moses hid his face ; for he was afraid to look upon GOD.......... This same Moses the man of GOD, is the same person who foresaw and prophesied the coming of the MESSIAH, JESUS CHRIST the Son of GOD in Deuteronomy 18:18 I will raise them up a prophet from among their brethren , like unto thee, and I will put my words in His mouth , and He shall speak unto them all that I shall command Him. Deuteronomy 18:19 And it shall come to pass, whosoever will not hearken unto my words which He shall speak in my name, I will require it of him. My beloved,, today I do have a testimony to share with you about this same JESUS CHRIST the MESSIAH and of whom Moses the man of GOD wrote more than 1,400 years before He (JESUS CHRIST) was born in Bethlehem, Judah .
THE TESTIMONY:
It was in the summer of 1998 when I was still in Dar es Salaam, Tanzania, when I had this dream. And In that dream I saw that I was standing infront of a church, on the north side. And as I was standing there suddenly I heard a very loud noise like an explosion which shook the whole earth. Then I lifted up my eyes towards the heaven, and when I looked up there I saw the heaven opening, and in the opening of the heaven I saw the Lord JESUS CHRIST standing there. The reason I knew it was Him is because He is the one who spoke to me the first day when He served me November 1997. Because the Lord JESUS had introduced Himself to me as JESUS CHRIST, and that If I follow JESUS I shall live. So after my face was lifted up towards the heaven, there He was. He was much bigger in statue than the size of a normal human being. When I saw Him He was wearing a long rob and the color of the rob was a shiny white. Then, while I was still standing there and in an amazement focusing all my attention on Him. Then suddenly there came from His presence towards me a very bright light towards me and within that light was cloven tongue like fires. This event was very similar to an event which happened during the Pentecoste to the disciples of JESUS CHRIST; as it is written in the holy Bible, the event which happened forty days after our Lord JESUS CHRIST ascended back to heaven. Acts 2:3 And there appeared unto them cloven tongues like as of fire , and it sat upon each of them. While all this was happening I was still standing there infront of a church and looking at the Lord JESUS CHRIST in the openings of the heaven. But what amazed me the most is that the cloven tongues like fire from His presence when touched me it didn't burn me and was not warm either. Then I woke up from my sleep and from that dream . And later on that same day I went to see my pastor, Pastor James Mboma of the Assemblies of GOD Church in Mwenge,Dar es Salaam. And soon as I finished telling him about my dream, Pastor James Mboma told me by the word of knowledge that, that was the act of GOD baptizing me with the HOLY GHOST. And this is my advise to anyone reading this testimony, go and find yourself any church, ministry or during crusades meeting that teaches their teachings based on the principles of the Bible, not any Bible but ONLY the Bible which has sixty six(66) books. Go there ask any pastor to see if you can be baptized the baptism of JESUS CHRIST., and receive the Lord JESUS CHRIST in your life as your Lord and Savior, then they will baptize you. Don't be afraid, and if there are some people or families who may be an obstacle to you , may the good Lord find a way for you to receive Him, and may He make a way where there is no way!. I pray about this prayer to our heavenly FATHER and ask Him in JESUS CHRIST name, Amen!........ There is only one true Living GOD, and the GOD of Israel is the ONLY GOD, Amen. This is a true testimony before the living GOD who have been showing me all the testimonies which I have testified on my facebook page, and there are many testimonies that I haven't shared with you yet! ALL the glory for this I give to GOD the FATHER and to our Lord JESUS CHRIST, Amen
.

Comments