VIKAO VYA UOVU.


Na: DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP
   AMOS KOMBA (RP), UFUFUO NA UZIMA.
Utangulizi wa Somo: Uovu ni mambo yoyote mabaya yanayotendwa na yanayofanywa na watu waovu.  Ikumbukwe kuwa 'Waovu ni Watu'. Anaweza akawa mtu yoyote yule awe ndugu, mama au baba.  Hawa watu wanaufanya uovu na siku haiishi bila kufanya uovu. Furaha ya muovu inaonekana pale anapofanya uovu wake!!.
Imeandikwa katika METHALI 2:14-15… [Wafurahio kutenda mabaya; Wapendezwao na upotoe wa waovu; 15 Waliopotoka katika njia zao; Walio wakaidi katika mapito yao.]…kwani Mungu aliwaumba watu ili wafanye uovu? Jibu ni hapana.  Ila kwa sababu ya hila za watu, kupotoka kwa watu na tamaa za watu wakaamua kumtafuta mfamle wa uovu wakaungana naye  ili wafanye uovu.
Imeandikwa katika YEREMIA 5:26… [Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu..]…

Imeandikwa pia katika 1TIMOTHEO 5:15….[Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.]..
Kinachosababisha ni tamaa za watu na chuki za watu.
Watu wengine huwa wanaamua waende kanisani wakisema ‘nikatafute kiti nikae kanisani,  niandae Bibilia yangu nimsikilize mchungaji nitoke nitakuwa sawa’… Hiyo ni sawa lakini si sawa sana…Lakini wakati wanaposoma neno  na kulitafakari ndipo watakaa sawa. Ni jukumu la kila mtu  kuwa na bidii ya kusikiliza mahubiri kwa bidii  na kuyatafakari. Kwenye hili, jitihada ya kuingia ndani ya neno  ni ya  kila mtu.
Kumbe sio lengo la Mungu kuwaumba watu ili wawe waovu, watu walipokuja duniani ila kwa hila zao, tamaa zao na chuki zao wakaaamua waungane na mfalme wa uovu ili waufanye uovu
Kabla ya kutuma uovu wanaanza kwanza kujadili uovu huu utakuwa upi na nani watakaoupeleka na namna ya kuupeleka wanakotaka uende. Lazima wanafahamu kwanza huyo mtu
Watu hawa wanaweza wakawa ni ndugu zako, wakati mwingine wanaweza wasiwe ndugu wa karibu, kama haajamfahamu huyu mtu wanatuma wapelelezi, wajue unachofanya kila wakati, baada ya hapo  wanarudisha taarifa kwenye vikao vyake, wakati wa bidii, wakati wa kuchoka na kila maneno wanayooongea, kwa hiyo  wakishafahamu  wanaamua kutuma saa ukiwa  na udhaifu.
UKIRI
Baba Mungu katika  jina la Yesu kama kuna wapelelezi wametumwa kwenye maisha yangu  nawakataa kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu ikiwa kuna wapepelezi wametumwa kutokea katika vikao vya waovu nawasambaratisha kwa jina la Yesu. Amen
 
Imeandikwa katika injili ya Luka kwamba kulikuwa na wapelelezi waliokuwa wanamviziavizia Yesu. Nakataa kwa jina la mtu yeyeyote anayenivizia  anayenipekeleza ili anijue mchana huu wa leo nakataa kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.
 Hawa wapelelezi hawaleti tukio ila wanatafuta kukujua. Baada ya hapo wanarudi kwenye kikao chao wanatoa taarifa. Mfano Musa  aliwatuma wapelelezi kwenye nchi ile ni nchi ya namna gani, watu wa namna gani,  wanapigana je n.k.  Kati ya hao kulikuwa na makundi mawili ambayo walirudisha majibu kwa namna ya rohoni na namna ya mwilini.
Hata wapelelezi wanachaguliwa wenye akili ya kuona mbali, nani ana uwezo wa kugeuka akaja kwako kama rafiki, au mtu wa karibu… wana akili sana. Na hawa wapelelezi wanaotumwa huwa wanalipwa. Mfano pepo unaweza ukaliambia toka likakataa  kwa sababu limeahidiwa malipo baada ya kazi hiyo.
 Hawa Wapelelezi wanatafuta kukufahamu. Mfano Hamani alikuwa na shida na Mordekai hivyo Hamani akatafuta watu akawalipa ili wampekeleze Mordekai.
Immeandikwa katika ESTA3:1-5..[Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye. 2 Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia. 3 Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme? 4 Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi. 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.]… Kumbuka Hata shetani alitaka Yesu amuainamie.  Hamani alipelekewa taarifa  kuwa Mordekai huwa hainami kila anapopita. Hamani akajaribu kupita wote waliinama lakini Mordekai hakuinama na Hamani akajua kuwa huyu Mordekai hayupo peke yake.
Wana wa Israel wametolewa Misri wanapekwa Kaanani wapetishwa jangwani nguo walizovaa hazikuisha wala kuchafuka wala viatu. Mungu huyu ni wa ajabu. Hamani aliamua ili  ainamiwe vizuri alimua na kupanga kuwaangamiza Wayahudi pamoja na Mordekai. Alifanya haya yote kwa sababu ya wivu na  kupenda sifa.  Kumbuka kuwa anayesimamisha mambo siyo Mordekai bali anayesimamisha mambo ni aliye nyuma ya Mordekai (Mzee wa siku.)
Wapo wale walioesema “tuone kama ataolewa”, “kama biashara yake itaendelea”, “kama atamaliza chuo” n.k….. Kumbbuka kuwa kuona wataona lakini hawatapata. Ni kweli utaona lakini sio yale unayoyawaza; ila utaona kivingine..
ESTA 3:5-13…[ 5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. 6 Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai. 7 Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari. 8 Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao. 9 Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. 10 Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. 11 Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. 12 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. 13 Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.]…
Hawa wapelelezi huwa wanalipwa.  Unaona Hamani alikuwa tayari kulipa watakaochaguliwa na mfamle Ahusuero kuwangamiza Wayuhudi…
Sio kila mtu huwa anakuwa katika vikao vya uovu…ila anachagua walio karibu na mkeo. Je Una mke bingwa wa kutoa mawazo.? Je yote huwa uanayafanyia kazi?
UKIRI
Kwa jina la Yesu ninaugeza mauovu waliyoyachilia kwangu urudi kwao walioutuma. Marafiki waliokusanya kwa  ajili yangu wakakaa ili kuniharibia kikao hicho nakisambaratisha kwa Jina la Yesu. Amen
 
Tunapoungumzia vikao  kuna vikao vya aina mbili  vya kiroho na kimwili.
UKIRI
Kwa mamlaka ya jina la Yesu nasambaratisha vikao vyote vya uovu kwa jina la Yesu na yote
yaliopangwa yawapate wao. Kwa jina la yesu kila aliye kaa kwenye kikao mabaya yote ywapate wao kwa jina la YESU. Amen
 

Comments