Waziri Nape Nnauye Mgeni rasmi Tamasha la Krismasi mwaka huu.

Waziri wa Habari,Utamaduni,
Michezo na Sanaa, Nape Nnauye

 WAZIRI wa Habari,Utamaduni,
Michezo na Sanaa, Nape Nnauye anatarajia kumwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Tamasha la Krismasi   linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini.Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha la Krisimasi, Alex Msama, maandalizi yanaendelea vizuri na ilitegemewa Mweshimiwa makamu wa rais Samia Suluhu kuwa mgemi rasmi katika tamasha hilo mwaka huu, Lakini kutokana na Mweshimiwa Makamu wa rais kuwa na majukumu mengine siku hiyo Mweshimiwa Nape Nnauye ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.

Kwa mujibu wa bwana Msama ni kwamba Waziri Nape Nnauye amekubali mwaliko huo wa kuhudhulia Tamasha la Krisimasi mwaka huu 2016 kama mgeni rasmi.
Tamasha hilo mwaka huu lina lengo la kumshukuru MUNGU kwa kuliwezesha taifa letu kufanya uchaguzi salama na kwa amani.
Kipindi cha uchaguzi wa october 25 kilikuwa kigumu lakini ashukuriwe MUNGU wa mbinguni kwa amani yake ambayo ilitawala.

bwana Msama pia amewaomba watanzania kuhudhulia kwa wingi katika Tamasha hilo la Krisimasi ambalo litafanyika tarehe 25 Desemba  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Rebeca Malope
Waimbaji watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Rebeca Malope kutoka Afrika kusini, Sarah k, Solomon Mukubwa na Faustin Munishi wote kutoka nchini Kenya. Kwa upande wa waimbaji kutoka Hata Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Joshua Mlelwa, KKKT Yombo na Kwaya ya Wakorintho wa Pili.





Joshua Mlelwa
Solomon Mkubwa na Rose Muhando.



Sarah K

Upendo Nkone

Jesca BM

Mwimbaji nguli Faustin Munishi.

Comments