YATIMA HANANASIFU WAKUMBUKWA.

BWANA YESU atukuzwe.
Kwa ajabu nyingi za MUNGU amewatumia watumishi wake mbalimbali ambao ni wana kikundi tu cha whatsapp ambao wameweza kuchanga pesa zaidi ya laki 4 ili kuweza kuwahudumiwa yatima katika siku maalum ambayo uongozi wa group hiyo ya whatsap walipanga.
Wana kikundi hawa ni kutoka makanisa mbalimbali walijumuika pamoja na kutoa pesa zao ili kutenda kazi ya MUNGU ya kuwasaidia yatima.
Biblia katika Yakobo 1:27 Inasema '' Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za MUNGU BABA ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.'' 

Ndugu hawa wamefanikiwa katika hili la kutii Neno la MUNGU.

Huwa ni vigumu sana watu waliojuana tu kupitia mitandao ya kijamii kama whatsap na kisha wanakuwa na maono mazuri kama haya.
Nasema ni ajabu kwa sababu watu ambao hawajuani na wanatoka maeneo tofauti tofauti lakini kupitia group ya Whatsap waliamua kushirikiana na kukusanya pesa hiyo kwa uaminifu na kisha kuipeleka katika lengo halisi la pesa hiyo.
Hawa ni group la Whatsap liitwalo SEMINA ZA NDOA ambalo kiongozi wa kikundi hicho ni Mtumishi wa MUNGU Andrew Shemson.
Hizi hapa picha chache katika tukio hilo la kutoa msaada kwa Yatima lililofanywa na kikundi hicho cha whatsap, ambapo walikwenda kutoa msaada katika kitua cha watoto yatima cha Munga center kilichopo Hananasifu kindondoni jijini Dar es salaam.






Comments