YESU KRISTO HAJAWAHI KUWA MUISLAMU(2)


Na Mtumishi Abel Suleiman Shiliwa.
Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza ya somo hili, ambapo niligusia vipengele viwili,
(1) Unyenyekevu
(2) Sinagogi

Tukaona kuwa Yesu Kristo hawezi kuwa muislamu kwa vigezo hivyo, basi leo, nitaangazia Vipengele vingine viwili
(1) KUVAA KANZU.
(2) KUSEMA AMANI IWE KWENU
Waislamu wamekuwa wakidai kwamba, Yesu alikuwa muislamu, kwa sababu tu ametajwa kuwa alikuwa akivaa Kanzu.
Yohana 19:23 Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.
Andiko hilo Waislamu wanalitumia katika kusema kwao kwamba, Yesu alikuwa muislamu mwenzao, kwa sababu alivaa kanzu kama wao, ukitaka kujua kwamba, watu hao ni wababishaji, andiko limesema Kanzu ya Yesu, ilipigiwa kura, baada ya Kusulubiwa, kabla ya Kusulubiwa, kanzu yake haikupigiwa kura, sasa wewe Waulize, "Je! wanakubali kwamba Yesu Kristo alisulubiwa msalabani akafa?" Utawasikia, "Yesu hakusulubiwa, wala hakufa" Sasa kama hakusulubiwa, inakuwaje mlitumie andiko la kanzu kusema ni muislamu mwenzenu, wakati hamkubali kwamba amesulubiwa? Inamaana kama hakusulubiwa kwa mujibu wa imani yenu, basi hilo andiko lilipaswa kuwa la uongo kwenu:- Na kama la uongo kwenu, hakuna sababu ya kulitumia.
Sasa tuangalie hoja hiyo ya kusema kwamba, Kuvaa kanzu hata kama watakubali Yesu amesulubiwa, je! linaweza kumfanya Yesu awe muislamu?
Katika Quran nzima hakuna andiko linalotaja Kanzu kama vazi la Kiislamu, au ni vazi special kwa ajili ya kufanyia Ibada, kama Waislamu wafanyavyo leo, bali Quran ina kazi 2 tu kwa mujibu wa Quran.
Quran 16 SURATUL NAHL
ﻭَﺍﻟﻠّﻪُ ﺟَﻌَﻞَ ﻟَﻜُﻢ
ﻣِّﻤَّﺎ ﺧَﻠَﻖَ ﻇِﻼَﻻً ﻭَﺟَﻌَﻞَ
ﻟَﻜُﻢ ﻣِّﻦَ ﺍﻟْﺠِﺒَﺎﻝِ ﺃَﻛْﻨَﺎﻧًﺎ
ﻭَﺟَﻌَﻞَ ﻟَﻜُﻢْ ﺳَﺮَﺍﺑِﻴﻞَ
ﺗَﻘِﻴﻜُﻢُ ﺍﻟْﺤَﺮَّ ﻭَﺳَﺮَﺍﺑِﻴﻞَ
ﺗَﻘِﻴﻜُﻢ ﺑَﺄْﺳَﻜُﻢْ ﻛَﺬَﻟِﻚَ
ﻳُﺘِﻢُّ ﻧِﻌْﻤَﺘَﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢْ
ﻟَﻌَﻠَّﻜُﻢْ ﺗُﺴْﻠِﻤُﻮﻥَ
81. Na Mwenyeezi
Mungu katika vitu alivyo viumba
amekufanyieni vitu vitiavyo
vivuli, na amekufanyieni makazi
katika milima, na amekufanyieni
kanzu zinakukingeni na joto, na (baridi) na amekufanyieni
nguo za chuma ndivyo hivyo
anavyokutimizieni neema zake
ili mpate kutii.

Kanzu kazi zake ni hizo mbili kama zilivyoanishwa ndani ya Quran.
(1) Kukinga na Joto
(2) Kukinga na baridi

Japo hapo sina uhakika kama kweli kanzu inaweza kugeuka A/c wakati wa Joto, au au Eater wakati wa Baridi, maana Dar e salaam kusingekuwa na haja ya kununua Feni, kwa ajili ya kupambana na Joto, watu tungekuwa tunavaa kanzu, ili tupate ubaridi.
Waislamu waishio MBEYA, Arusha, Iringa, Njombe, na sehemu zingine zenye baridi, wangekuwa wanavaa tu kanzu, ili kujikinga na baridi. Kwa hivyo hakuna andiko linalosema kwamba Kanzu ni vazi la kiislamu, au vazi la Ibada kwa ajili ya waislamu, ili Yesu awe muislamu! na isitoshe Kanzu Kibiblia matumizi yake ni tofauti na ya ndani ya Quran, kwani Iliandaliwa kwa ajili ya kazi ya Ukuhani.
Kutoka 28:40 Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.
41 Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.
42 Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;
43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.
Hiyo ndo ilikuwa kazi ya Kanzu, kwa ajili ya kazi ya Ukuhani, Waliivaa tu pale walipoingia katika hema za kukutania, na walipotoka, waliyavua, hayo yakaitwa mavazi Matakatifu, kwa sababu yalivaliwa kwa ajili ya kazi Takatifu.
Walawi 16:1 Bwana akasema na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni, walipokaribia mbele za Bwana, wakafa;
2 Bwana akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.
3 Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ng'ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa.
4 Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa.
Kanzu hizo za Kikuhani zilikuwa maalumu sana kwa ajili ya utumishi, mavazi ambayo yalikuwa na masharti katika kuyavaa, Hakuruhusiwa mtu mwingine asiye kuhani kuvaa mavazi hayo yaliyokuwa maalumu kwa ajili ya kazi ya Ukuhani, Haruni na wanae walipomaliza, waliyavua, kama Wafanyavyo mapadre, na Wachungaji wa Anglikani, Lutherani, na Moraviani, huyavaa wakati waingiapo Madhabahuni, na baada ya Ibada huyavua, hawatembei nayo, tofauti na Kanzu za waislamu leo, ambazo
Vibaka, Wapiga debe, wacheza music, Huzivaa, masokoni, Maguest house kwenye uasherati wanaingia nayo, yanauzwa kila kona, mpaka 3000 kwa sababu ni kanzu za kawaida, zisizo Takatifu, ambazo walikuwa wanavaa wanawake waliokuwa mabikira.
2 Samweli 13:18 Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake.
Kanzu zao hata misiba, tunawaona, wanazivaa, wakati Kanzu za Kikuhani, zilikuwa special kabisa, na Kanzu ya Yesu, Kuhani mkuu,
Waebrania 13:1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
Kanzu yake ilikuwa ya thamani zaidi, kuliko hata zile za wakati wa Haruni, Kanzu ambayo Ilikuwa na uponyaji.
Marko 5:25 Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,
26 na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya
27 aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.
Kanzu hiyo ya Yesu, huwezi kuifananisha na kanzu za waislamu, ambazo kazi yake ni kukinga na joto na baridi, kanzu ambazo hata zikiziguswa hazina cho chote, kanzu ambazo hazigombewi, marehemu akifa watu hawagombanii, Yesu Kanzu yake, imepigiwa kura, kwa sababu ya uthamani wake, Kwa hivyo Yesu hawezi kuwa muislamu kwa kigezo cha kanzu, kwa sababu Kanzu siyo vazi la kiislamu, na ni tofauti na wavaazo waislamu.
(2) YESU KUSEMA AMANI IWE KWENU
Waislamu hudai kwamba, Yesu alikuwa muislamu kwa sababu alisema, "Amani iwe kwenu.
Luka 24:36 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Hapo Waislamu hudai kwamba Yesu alikuwa muislamu, kwa sababu Neno Amani iwe kwenu, kiarabu ni As Salaam aleykum (السلام عليكم) Kwa sababu Wakristo wengi Kiarabu hawajui, basi wakiambiwa hivyo, huamini, na kujua kwamba Yesu alisema As salaam aleykum, ila nimeamua kutoa elimu hii ili kama wewe msomaji wangu, ulishawahi kukutana na hoja hiyo, basi leo jifunze.
Katika Biblia ya Kiarabu, Yesu alisema, Salaamun lakum (سلام لكم) Salaamun lakum, hiyo ni amani ambayo ni yake Yeye Yesu
لوقا
24: 36 و فيما هم يتكلمون بهذا وقف يسوع نفسه في وسطهم و قال لهم سلام لكم

Hapo Kuna Salaamun lakum (سلام لكم) Hakuna neno السلام عليكم (As salaam aleykum) Kwa kwa Sababu unaposema!
السلام عليكم 









As salaam aleykum, unamaanisha kwamba, amani ya allah (mungu muabudiwa na waislamu) iwe juu yenu, hiyo ni amani ya allah mungu wa waislamu, ambapo kirefu chake husema.
As salaam aleykum Wa-raham tullah wabara kaatuhu السلام عليكم ولترحمة الله وبركاته Tafsiri yake, ni Amani ya mwenyezi mungu iwe juu yenu, na rehema zake na baraka zake!
Lakini Salaamun lakum (سلام لكم) Amani iwe kwenu, ni amani ya Yesu mwenyewe, ambayo yeye mwenyewe amejitofautisha na amani ya mungu wa waislamu.
Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
14: 27 سلاما اترك لكم سلامي اعطيكم ليس كما يعطي العالم اعطيكم انا لا تضطرب قلوبكم و لا ترهب
Hapo Yesu سلاما (Salaama) Amani اترك لكم Nawaachineni, سلامي اعطيكم Amani yangu nawapa Amani yake ametupa, ila akasema, ليس كما يعطي العا لم Niwapavyo mimi ni tofauti na Ulimwengu utoavyo. akimaanisha kwamba, kuna amani itolewayo na Ulimwengu, na ulimwengu huo sifa yao kubwa ni hii.
1 Yohana 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Ulimwengu ni wale ambao wanakataa muwa Mungu siyo baba, na kwamba sisi siyo watoto wa Mungu, maana Ulimwengu huo, haukumtambua Baba, kama ambavyo haitutambui sisi kuwa tu watoto wa Mungu.
Na hao wenye sifa hizo ni Allah pamoja na Waislamu.

Quran 72 SURATUL JINN
ﻭَﺃَﻧَّﻪُ ﺗَﻌَﺎﻟَﻰ ﺟَﺪُّ
ﺭَﺑِّﻨَﺎ ﻣَﺎ ﺍﺗَّﺨَﺬَ ﺻَﺎﺣِﺒَﺔً
ﻭَﻟَﺎ ﻭَﻟَﺪًﺍ
3. Na kwa hakika
utukufu wa Mola wetu
umetukuka, hakujifanyia mke
wala mwana.

Ulimwengu, unapinga kupitia kauli ya majini kwamba Mungu hana mwana, na Allah, akakazia kauli ya majini aliposema.
Quran 18 Kahf
ﻭَﻳُﻨﺬِﺭَ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻗَﺎﻟُﻮﺍ
.ﺍﺗَّﺨَﺬَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻭَﻟَﺪًﺍ
4. Na kiwaonye wale
wanaosema: Mwenyeezi Mungu
amejifanyia mwana

Allah anasema Quran imekuja kutoa onyo kwa wale wanaosema Mungu ana wana, yote hiyo ni kwa sababu, Hawakumtambua Baba, wala sisi wana wa Mungu. Kwa hiyo Allah na Waislamu, ni ulimwengu ambao wanatoa Amani (السلام عليكم) As salaam aleykum, Amani ambayo ni toafuti na ile aliyoitoa Yesu. (سلام لكم) Salaamun Lakum.
Kwa hivyo Yesu hawezi kuwa muislamu, kwa sababu ya kusema Amani kwenu, kwa sababu amani ya Yesu ni tofauti na amani ya ulimwengu, yaani Allah pamoja na Waislamu, na kama huamini kwamba Waislamu ni Ulimwengu utoao amani tofauti na amani itolewayo na Yesu, wewe waulize, Je! Wanakubali kwamba sisi Wafuasi wa Kristo ni watoto wa Mungu, na kwamba Mungu, ni baba yetu?
Utawasikia tu majibu yao
Au waulize kwamba, Yesu amesema amani yangu nawapa, sasa Je! hiyo Amani wanayoitumia yaani As salaam aleykum, ni amani anayotoa Yesu, au amani ya allah mungu wao? Utayasikia majibu yao.
USIKOSE sehemu ya tatu ya somo hili, ambalo nitazungumzia vigezo vyao vingine ambavyo husema alikuwa muislamu kwa
Kwa kutawadha,
Kusujudu.
Kufunga.

Comments